Vijana wa HALAIKI huwa wananufaika na kipi baada ya mafunzo na shughuli ya kiserikali kupita?

Vijana wa HALAIKI huwa wananufaika na kipi baada ya mafunzo na shughuli ya kiserikali kupita?

Huwa wanapewa

Pilau ,Soda na maji buleysafiri kutoka shuleni na kurudi shuleni Bure pamoja na 10,000 kifuta machozi.

Vipi hapo?
Hawa hawakuwa na usafiri, walipewa usafiri siku moja tu ya tukio. Kifuta machozi nacho ngoja tuone.
 
Yaani unafananisha izo kids activities za Feza wanaposoma watoto wa mwigulu na mafunzo wanayopewa watoto ya kukimbiza mwenge na kwenda kushinda kwenye mikutano ya CCM seriously.! Maelezo yako yote ni blah blah tu, ishu ni kwamba hizi events hazina faida ndio maana viongozi wanatanguliza watoto wa wanyonge, ziingekua na positive income kwa ubinafsi wa viongozi wangepeleka watoto wao, period.
Upo sahihi kabisa zingekuwa zina maslahi mapana wangejazana watoto wa viongozi.
 
Mara nyingi zawadi ni hizo truck suit wanazopewa na mara chache vipesa vya matumizi ... niliwahi shiriki back then
Pole mkuu, kwa zawadi hizo na ile pilikapilika ya mafunzo uliyopitia unaweza kukubali mwanao ashiriki?

umefaidika na nini?
 
Mwanao kashiriki au?
Mbona unang'ang'ania vyeti mi nshashiriki hayo sana utotoni hayahitaji ujuzi wowote sasa hicho cheti kitamsaidia nini
Ni mapendekezo kama itafaa wawe wanapewa vyeti vya mafunzo hayo, watoto wamesoma nusu siku, siku nyingine hawasomi kabisa(kuna ambao itawaathiri darasani), kuchoka na kupitia changamoto nyingine kuwapa pongezi ya track suti, raba over size, miamvuli na pilau sidhani kama ni sahihi. Sasa tofauti yao na ambao hawajashiriki ni nini? Waangalie waweke utaratibu wa kuwareward kwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo.
 
Wanapandikizwa elements za kizalendo wangali watoto.
CAG kila siku anareport matrilion kupotea NO ACTION TAKEN
Hao wanaotafuna hayo matrilion wengine wamepita mpaka jeshi ila hawajali huo uzalendo.
 
Nilikua chipikizi mwaka 1987, baada ya kua mkubwa aiseeee nilijiona bonge la fala sana nikiwaza walivyo tufanya wapuuzi wakati wao watoto wao walikua wakisoma Kenya na Uganda miaka hiyo
😂 pole sana mkuu si ulinufaika lakini?
 
Kitu kizuri sana hiki Kwa watoto, Kwa mazingira yetu watoto wakipata exposure Kama hii kushiriki michezo na activity kubwa Kama hizi huwaongezea confidence na hu unlock potentials zao. Si ajabu kwetu sisi kukuta mtu kamaliza chuo lakini bado ana uoga uoga ila kwa wenzetu mtoto wa 15 ni mkubwa sana maana ameshakuwa exposed sehem mbali mbali. Hata bila vyeti ile tu ku take responsibility inamkuza mtoto ile kuwa sehem ya mafanikio ya jambo flan Ina instill kitu flan Kwa mtoto na kujiamini pia. Watoto wanajifunza mambo mengi sana kwa njia hizi kuliko kukaa tu darasani
Hao ndiyo kina Lucas Mwashambwa wa baadae

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Pole mkuu, kwa zawadi hizo na ile pilikapilika ya mafunzo uliyopitia unaweza kukubali mwanao ashiriki?

umefaidika na nini?
Nilifurahi tu nilipo chaguliwa sikujali zawadi pia sehemu ya mazoezi na kumbukumbu nzuri ktk safari yangu ya utoto.

Yes mtoto wangu nitakubali ashiriki ila akipenda yeye coz myself sikuona kama adhabu bali ni sehemu ya burudani na ukakamavu
 
Nenda stationery print cheti umpe mwanao. Mbona rahisi sana?.... Acheni ulalamishi wa kipuuzi. Wazazi kama wewe ndo mnafanya watoto wanakuwa na tabia za kijinga kwa kudhani kukaa darasani peke yake ndo maisha. Mtoto anakaa shuleni masaa ya kutosha na akirudi nyumbani anaenda tena tuition badala ya kufanya kazi za nyumbani. Hata wakati wa likizo badala ya kufanya kazi unampeleka tuition. Wazazi wengi tuna mchango mkubwa kwenye kutengeneza kizazi cha hovyo.
 
Habari zenu wakuu.

Tarehe 02/04/2024 kulikuwa na tukio la kuwasha mwenge wa uhuru mkoani kilimanjaro na mgeni rasmi alikuwa ni waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa.

Kama ilivyo kawaida kwa shughuli yeyote ile lazima yawepo maandalizi mazuri ili kuweza kufanikisha kwa ufanisi mkubwa.

Moja ya maandalizi ni pamoja na mafunzo ya halaiki kwa vijana waliochaguliwa kutoka shule mbalimbali ndani ya mkoa/wilaya husika. Zoezi la mafunzo kwa waliochaguliwa lilidumu kwa zaidi ya miezi miwili.

Je hawa vijana wa halaiki wananufaika na nini kitakachowatofautisha na vijana ambao hawakuchaguliwa baada ya shughuli ya kiserikali kufanyika? Kuna vyeti vitakavyowapa utambulisho kuwa walishiriki mafunzo hayo?

Kama hakuna nashauri kuwe na utaratibu huo wa kuwazawadia hata vyeti maana mpaka sasa naona vijana wameambulia kupewa track suti, raba na miamvuli. Ukizingatia walilazimika kusoma nusu siku na wakati mwingine kutokuingia darasani kabisa ili kushiriki mafunzo hayo ya halaiki.

Mheshimiwa Dkt. Gwajima D wizara yako inahusika na watoto naomba kama unaweza kutoa muongozo/maelekezo yoyote kwenye hili utusaidie. Tunaomba ufikishe na haya mapendekezo yetu kwa faida ya watoto. Ahsante.

NAWASILISHA....
View attachment 2963115View attachment 2963116View attachment 2963117
MACCM WANAWAPA ELF TANO TANO
 
Nenda stationery print cheti umpe mwanao. Mbona rahisi sana?.... Acheni ulalamishi wa kipuuzi. Wazazi kama wewe ndo mnafanya watoto wanakuwa na tabia za kijinga kwa kudhani kukaa darasani peke yake ndo maisha. Mtoto anakaa shuleni masaa ya kutosha na akirudi nyumbani anaenda tena tuition badala ya kufanya kazi za nyumbani. Hata wakati wa likizo badala ya kufanya kazi unampeleka tuition. Wazazi wengi tuna mchango mkubwa kwenye kutengeneza kizazi cha hovyo.
sawa mkuu
 
Nilifurahi tu nilipo chaguliwa sikujali zawadi pia sehemu ya mazoezi na kumbukumbu nzuri ktk safari yangu ya utoto.

Yes mtoto wangu nitakubali ashiriki ila akipenda yeye coz myself sikuona kama adhabu bali ni sehemu ya burudani na ukakamavu
Hongera sana mkuu
 
Back
Top Bottom