Vijana wa kariakoo leo mmeniweza, nimewanyooshea mikono juu

Vijana wa kariakoo leo mmeniweza, nimewanyooshea mikono juu

huo ni wizi kama wizi mwingine, kazi ya laana hiyo
Mwisho wa siku inabidi umpe tu maana kashakuzungusha wakati anapoenda anapajua na kwa kua unaona kasumbuka inabidi umpe tu kumbe ndio mchezo wao Ila ukisubiri anaenda kuchukua palepale na yeye na huyo mwenye duka wanajuana yaan usione umeenda nae anauliza Bei ukahisi hawajuani kumbe ni mtu wake na ndio alipokua anaenda kuvifuata hapo baada ya kukupanga Mawawa alafu unaweza sema ni 18,000/- kumbe Bei ni chini ya hapo Ila muuzaji kagundua bwawa limeshaingia ruba dogo winga anaweza akakosa kila kitu, mwisho na wewe ukamuongeza kwa hio kule anapata na huku anapata ukijumlisha huku na huku 20,000/- hii hapa
 
😂😂😂😂 Mpaji Mungu njoo hapa umuombe msamaha huyu jamaa kwa kumzururisha wakati unajua fika huna store
🤣🤣Kuna maeneo ukileta upori pori watu tutakufundisha maisha!

Yaan mm na ujanja/ujinga wangu wote kama Kuna kitu nahitaji kufanya kariakoo afu sielewi elewi natafuta rafiki yangu wa angle hyo nampa ganji kidogo tunaishi kibingwa
 
Ndugu zangu nikiwa katika harakati za kununua vifaa kwa ajili ya tv yangu yaani Tv guard na Hd Tv cable 4k haya ndio yaliyonikuta.

Nikaenda moja kwa moja kwenye moja ya maduka yanauza tv, baada ya kufika pale nikauliza hivi vifaa wakaniambia vipo.

Tukaanza kubagain bei, tv guard wakanimbi 30,000 na Hd tv cable 20,000, nikatoa macho mbona bei kali hivyo? Jamaa akanikazia macho brothe hivi vitu ni og.

Nikasema hapana vyote nitawapa 25,000 Tukazozana pale bei mwisho siku tukakubaliana 30,000 kwa vyote, yaani tv guard kwa 20,000 na Hd tv cable kwa 10’000.

Wakaniambia brother lipia, nikawambia nipe kwanza bidhaa ndio nilipie, wakasema havipo hapa ngoja nifuate stoo, nikawambia tunaenda wote.

Hao tukaongozana cha ajabu tunazunguka tu stoo hatufiki, cha ajabu tena tunapita kwenye baadhi ya maduka kuulizia hizo bidhaa, kiujumla nikajua kinachoendelea kuwa kijana anatafuta ridhiki.
Nikamtahadharisha kuwa, nataka bidhaa yenyewe maana nimesha jua kuwa zile bidhaa walikuwa hawana ata ile ngoja nikachukue stoo ilikuwa nizugisha tu.

Basi tukafika kwenye moja ya duka akauliza akaambiwa zipo muuzaji akamtajia bei, nikastaajabu, guard tv 10,000 na Hd tv cable 8,000.

Kumbuka kule aliniambia vyote nitavipata kwa 50,000 na tukakubaliana kuwa nitampa vyote kwa 30,000 dah.[emoji3][emoji3]

Kwa kuwa tulikuwa tumeshazunguka sana, nikaona siyo kesi nikampa ile tuliyokubalia awali kisha nikatabasam.

View attachment 2832101

View attachment 2832102
Umefanya vzr sna kumpa hyo pesaa
 
Juzi pia niliona Fridge nzuri ktk moja ya mitandao. Nikamchek jamaa akasema anafanya delivery..

Ila akili ikanicheza nikamwambia nakuja dukani (nia yangu nipate risiti na pia nipajue just in case ikizingua, pia ninunue na kitu kingine nikipenda).

Kufika Pale kkoo jamaa kanifata naona ananipeleka sehem ambapo kwa kawaida kitu kama fridge si rahisi kukaa kwenye yale maduka.

Kumbe ni store huko kakosa ikabidi tuhame mtaa.. (hapa nikajua jamaa ni Winga) ikabidi niwe mpole...

Uzuri bei tuliyokubaliana ilikuwa rafiki sana maan nimeokoa kama laki 6 hivi ningenunua M.City au ktk Malls zingine.
 
Back
Top Bottom