Vijana wa Kenya wapo Doha na Dubai; Vijana wa Tanzania wapo wapi?

Vijana wa Kenya wapo Doha na Dubai; Vijana wa Tanzania wapo wapi?

Vijana wa kitanzania wengi ni wavivu, waoga na wanaopenda sana kitonga , sijui ni elimu duni au nini lakini vijana wa kibongo huwezi walinganisha na vijana wowote wa kiafrika. Yaani hata hapa tu JF ukiangalia comments zao kuhusu ughaibuni utajua bongo hamna vijana wa shoka kama zamani, wengi lege lege jamii ya kina juma lokole.
 
Sio wavivu bali waoga na kupenda Kitonga.

Mtu ukimwambia kuna kazi kenya anaanza kuwaza ataachaje mademu zake akina Khadija😀😀
 
Wakenya wanaijeria ni watu wako siriaz na maisha sana na wanasaidiana na wanainuana sana na wanapendana sana na wanajua definition ya umaskin ni nini...ni tofaut na huku kwetu..kwanza ubinafsi, chuki na roho mbaya, hatupendani, Yan kuona wewe umetoboa ntachukia sana ,, uchawa ..ndio mana si ajabu kukuta mtanzania mmoja kati ya wakenya 50 ama wanaijeria 70...ni LAANA ya nchi hii
 
Watanzania sio wavivu ila nafikiri wengi wetu ni waoga na wabinafsi. Leo ukimwambia kijana wa kitanzania aende Marekani kitu kitakachomjia kuchwani ni ushoga na magenge ya uhalifu afikirii kuhusu opportunities.
Na pia kwenye maswala ya visa na passport tunazungushwa sana.
 
Wakenya wanaijeria ni watu wako siriaz na maisha sana na wanasaidiana na wanainuana sana na wanajua definition ya umaskin ni nini...ni tofaut na huku kwetu..kwanza ubinafsi, chuki na roho mbaya, uchawa ..ndio mana si ajabu kukuta mtanzania mmoja kati ya wakenya 50 ama wanaijeria 70...ni LAANA ya nchi hii
Ni kweli aisee, watanzania wana chuki na roho mbaya, anaweza kukuchukia kisa tu comment😇😇😇🤣🤣🤣
 
Ndio mana sisi mabongolala hua tunakalisha mapumbu na kusema sjui wanaijeria matapeli n.k, ila Sasa ndio tujue akili za Hawa jamaa wako bize sana kuishuhulisha akili namna ya kutoboa..Kuna wakati nilikaa na mnaijeria mmoja nilijiona kama fara tu Yan jamaa akili zao kama kompyuta vile Yan mipango michongo ya kutoboa kashaiandaa na anatekeleza Moja baada ya nyingine na hawajui kukwama sjui kukata tamaa...sisi Sasa tumekalisha mapumbu mtaani tunajikuna Kuna tu na kupiga soga , wengine mtu unazunguka tu hata haujui unaenda wapi
 
Watanzania sio wavivu ila nafikiri wengi wetu ni waoga na wabinafsi. Leo ukimwambia kijana wa kitanzania aende Marekani kitu kitakachomjia kuchwani ni ushoga na magenge ya uhalifu afikirii kuhusu opportunities.
Na pia kwenye maswala ya visa na passport tunazungushwa sana.
Kwenye ubinafsi hapo...mtu aliyetoboa anakuambia
"Dah mwanangu ngumu sana kukusaidia pambana tu , mim mwenyewe nilisota sana ila huku kugumu mwanangu"
 
Nimesafiri mara kadhaa na kupita kwa muda katika viwanja vya ndege vya Hamad International Airport (HIA) jijini Doha - Qatar na Dubai Airport - DXB pale Al Garhoud, Dubai ; UAE.

Licha ya ukubwa wa Viwanja hivi, jambo nililoona ni uwepo wa ndugu zetu Wakenya wakiwa kama wafanyakazi katika viwanja hivi vya ndege.

Kuna Wakenya wengi kwenye nafasi za udereva, ulinzi, wahudumu wa usafi, wahudumu wa maduka, wahudumu sehemu za ukaguzi, wahudumu sehemu za transfer na kadhalika.

Hapa kwetu huwa naona nafasi zinazotangazwa kwenda nchi za Mashariki ya kati ni nafasi za wasidizi wa kazi za nyumbani (housegirls).

Kwanini ipo hivyo?

Nafahamu kuna makampuni ya mawakala inafanya hizi kazi, badala ya kupeleka tu wadada wa kazi nadhani pia mngekuwa mnatoa pia fursa kwa vijana wa Kitanzania.
Benjamin Mkapa wameanza udalali.

Wataanza kwenda huko Arabuni na Saudia.

Hatutaki vilio tu vikianza
 
Ndio mana sisi mabongolala hua tunakalisha mapumbu na kusema sjui wanaijeria matapeli n.k, ila Sasa ndio tujue akili za Hawa jamaa wako bize sana kuishuhulisha akili namna ya kutoboa..Kuna wakati nilikaa na mnaijeria mmoja nilijiona kama fara tu Yan jamaa akili zao kama kompyuta vile Yan mipango michongo ya kutoboa kashaiandaa na anatekeleza Moja baada ya nyingine na hawajui kukwama sjui kukata tamaa...sisi Sasa tumekalisha mapumbu mtaani tunajikuna Kuna tu na kupiga soga , wengine mtu unazunguka tu hata haujui unaenda wapi
Ukweli mtupu huu. Sie wabongo wengine huku wenye marafiki wa kinigeria jamaa uwa wanatushangaa maana wanadai wabongo hawako hivyo. Tunacheza miguu yote mpaka wanatuheshimu.
 
Kwenye ubinafsi hapo...mtu aliyetoboa anakuambia
"Dah mwanangu ngumu sana kukusaidia pambana tu , mim mwenyewe nilisota sana ila huku kugumu mwanangu"
Huu ubinafsi unatokana na kwamba mbongo ukimsaidia baadae anakuja kukuchoma wewe uliemsaidia. Hii ipo sana kwa wabongo. Wenzetu wanigeria na wakenya wanasaidiana lakini ni kimakabila.. Yoruba atamsaidia myoruba, Igbo atamsaidia muigbo., mkikuyu kwa mkikuyu, mjaluo kwa mjaluo, hawa jamaa hawaingiliani kabisa.
 
Kwa sababu huko Dubai, Qatar hakuna mawakala wakitanzania waliofungua ofisi za manpower ili kuwapa watanzania kazi hizo.
Wengi wa mawakala wanafanya third-party.
Yaani unakuta wakala wa kinaijeria au kikenya, au Ghana, au wakala wa Dubai muarabu anatafuta Wakala aliyeko Tanzania.

Wakala mnaijeria au mkenya au mghana hawezi kumpa KAZI ya maana mtanzania zaidi ya uhousegirl akamuacha mnaijeria mwenzake.
Amezungumzia Wafanyakazi wa Airport bro,hakuna House girls pale,kubari kuna sehemu wanatupiga sio kubisha au kuleta upinzani ni kila kitu.na kwenye ma supermarket pia ni hivo wakenya waganda.
 
Ulichoandika ni kweli kabisa, niliona hata pale Riyadh Saudi Arabia kuna wakenya wengi sana wanafanya kazi.

Tanzania tuna namna ya kuwafanya vijana kuishi bila kupambana kabisa. Yaani wachache wanakomaa kwenye elimu na wachache ni kwenye biashara za maana. Kundi kubwa ni la kubaki wakiomba muujiza wa maisha.
 
Wed
Amezungumzia Wafanyakazi wa Airport bro,hakuna House girls pale,kubari kuna sehemu wanatupiga sio kubisha au kuleta upinzani ni kila kitu.na kwenye ma supermarket pia ni hivo wakenya waganda.

Nafikiri huna uelewa na mambo ya kazi huko mashariki ya kati.
Nilichoeleza kwa wanaojua wanaelewa. Sijampinga mtoa masa ila nimetoa sehemu ya majibu
 
Labda kizaz cha watoto wa 2000

Ova
 
Back
Top Bottom