Nimesafiri mara kadhaa na kupita kwa muda katika viwanja vya ndege vya Hamad International Airport (HIA) jijini Doha - Qatar na Dubai Airport - DXB pale Al Garhoud, Dubai ; UAE.
Licha ya ukubwa wa Viwanja hivi, jambo nililoona ni uwepo wa ndugu zetu Wakenya wakiwa kama wafanyakazi katika viwanja hivi vya ndege.
Kuna Wakenya wengi kwenye nafasi za udereva, ulinzi, wahudumu wa usafi, wahudumu wa maduka, wahudumu sehemu za ukaguzi, wahudumu sehemu za transfer na kadhalika.
Hapa kwetu huwa naona nafasi zinazotangazwa kwenda nchi za Mashariki ya kati ni nafasi za wasidizi wa kazi za nyumbani (housegirls).
Kwanini ipo hivyo?
Nafahamu kuna makampuni ya mawakala inafanya hizi kazi, badala ya kupeleka tu wadada wa kazi nadhani pia mngekuwa mnatoa pia fursa kwa vijana wa Kitanzania.