Vijana wa Kenya wapo Doha na Dubai; Vijana wa Tanzania wapo wapi?

Si tu watoto wa 2000 hata vizazi vilivyopita hali ilikuwa hiyohiyo. Ukienda nchi kama Uingereza diaspora wa Kenya ni wengi kuliko hata diaspora wa Tanzania.
Vijana wa kitanzania wamelala sana ....na huu uchawa+kukata mauno ndiyo kunazidi kuwalemaza

Ova
 
Nakazia
 
Nilipo tupo watanzania wanne tu, wakenya ni wengi mno.
Serikali ya Tanzania inajari kupambana na chadema mambo mengine sio kipaumbele.
Watu watauliza imekuaje hoja hii;
Ni kwamba nasikia hata kupiga simu za kiofisi nchi za nje haiwezekani mpaka simu zisajiliwe sijui kivipi. Yaani ukitaka kupiga simu haiendi; hizi za kiofisi landline wamekaba zote, utapata ujumbe no connection mpaka ujisajili. Tumefika hapa kweli kama nchi? Tumeludi nyuma enzi za miaka ya 70 kupitia kwa operator ili akusikilize kama wewe ni chadema au ccm!!
 
Watanzania wengi wapo Oman na UAE (Dubai) ila sio kama Vibaraka bali watu wenye positions kubwa, atleast watu wa Pwani/Visiwani.

Kabla ya hawa jamaa wa unga Kutuharibia Nchi yetu ilikua Passport ya Tanzania Ina nguvu sana hizo Nchi
 
Mwaka juzi (2023) nilipata safari ya kwenda nje ya nchi,ila mchakato wa kupata passport sasa 😑 . Yaani ni kama maofsa hawataki raia wasafiri,nimelipa online nikaenda ofsini kwao kijana mmoja akaniuliza kwanini umelipia online . Hili swali lilifanya nikahairisha safari mpaka leo.
 
Utayari huo vijana wengi wa Sasa hawana,wameridhika na maisha ya hapa pamoja na uoga,miaka ya 2000 Mimi nakua Kaka zetu wote wanawaza safari Tena bila passport,nilikutana na brother ananiambia yupo ughaibuni since 1989..

Kuna sister alikua shirika la wakimbizi alitupa mchongo tukae uraia wa Tanzania tuchukue wa Somalia then atufanyie mpango wa Asylum.
 
Nimefanya hii kazi ya uwakala kwa muda mrefu sana. Nakiri kwamba vijana wa kitanzania bado wana changamoto nyingi sana . Nitaeleza wakati ukifika
Mkuu, kwa kifupi ni kwamba, hawauziki kutokana na ubabaishaji mwingi katika kupata document za kusafiria, mitala ya elimu isiyoeleweka na wengi suala la lugha kuu za kigeni ni tatizo kuu.
 
Najua itaonekana kama tunajichukua ila kulinganisha wakenya na waTanzania sio fair, bora kulinganisha watanzania wa miaka ya 80 mpaka 2000 mwanzoni na wa sasa.

Hawa washkaji washatupigaga gap kitambo, ni vile kwa sababu tumewashinda kuongea kiswahili na tuna wapelekea mahindi basi tuna amini tuko nao sawa.

Sio huko tu hata kwenye hizi freelancing platforms wao wamekuwa wakipata mashavu zaidi yetu, isishangae ingawa sisi tuna amini tunajua kiswahili zaidi ili gigs za translation, transcription na interpretation za Swahili to English and viceversa ni rahisi sana kwake kupewa kuliko wewe.
 
Hamjui lugha.
Kuomba passport ni uhaini TZ.

Kila siku kabla ya kulala nyosha mikono juu sema "nchi ya kipumbavu sana hii" mara tatu.
 

Wabongo gani wanajua sana kiswahili hawa wasiojua tofauti ya L na R? A na Ha? Za, Dha na Tha? Wabongo hawajui lugha yeyote ile Swa wala Eng.

Online gigs zitakuja vp bongo wakati BOT wanaona hata PayPal ni scam? Hii nchi ni bongolala kuanzia juu hadi chini.
 
Kwahiyo unataka utuambie hao wakenya wanamatumizi mazuri ya L and R, A na Ha, Za, Dha na Tha?
Kwenye Kiswahili bongo tupo vizuri ila English wengi wetu hatujui.
 
Kwahiyo unataka utuambie hao wakenya wanamatumizi mazuri ya L and R, A na Ha, Za, Dha na Tha?
Kwenye Kiswahili bongo tupo vizuri ila English wengi wetu hatujui.

Nenda popote pale online leta mkenya mmoja tu aliyekosa matumizi ya hizo herufi mimi nitakuletea 100. Imefika hatua kuona mitanganyika imefanya matumizi sahihi ndo nashangaa.
 
Naona kama hii nchi imelaaniwa sijui ...ulimwengu wa digitalization PayPal inaonekana scam? Kuna siku nilishindwa kumtumia mtu pesa ambaye Yuko nchi flan afrika kwa wakati ..ilinichukua wiki nzima
 
Nenda popote pale online leta mkenya mmoja tu aliyekosa matumizi ya hizo herufi mimi nitakuletea 100. Imefika hatua kuona mitanganyika imefanya matumizi sahihi ndo nashangaa.
Hao wa online wapo vizuri kwenye kuandika kiswahili na usikute wamesomea kiswahili vilevile. Ila kwenye kukiongea kiswahili watz tupo vizuri kuliko wakenya.

Kuna kukiandika Kiswahili na kukiongea kiswahili.
 
Naona kama hii nchi imelaaniwa sijui ...ulimwengu wa digitalization PayPal inaonekana scam? Kuna siku nilishindwa kumtumia mtu pesa ambaye Yuko nchi flan afrika kwa wakati ..ilinichukua wiki nzima

Nchi ya kipumbavu hii. Maza yupo busy na comedians wenzake anapewa umbea wa Manara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…