Vijana wa Kiume badilikeni

Wanataka kuamka wajikute ni diamond i.e kutoboa kirahisi, wakati hata diamond ana history ndefu yaliyofuchwa nyuma ya mafanikio yake
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kumbe siongeagi point
 
Mie 99.99% ya watu wanaohitaji msaada ni wanaume...! Sijui lakini!
 
Nafikiri wazazi nawalezi wanachangia sana kwenye hili
 
Wakati ukuta... mambo mawili hayakumbatiwi pamoja. Mkono wa kushoto ukiupa kazi, wa kulia ulegea, na kinyume chake. Hizi ni zama za -ke waliodhani -me wanafaidi maisha huko nyuma.
Kwa hiyo wamechukuwa nafasi ya ke
 
Sawa kwa hio umekuja kunisema huku.
Sio vizuri ni bora ungeniambia tu mzee. Si kwa ubaya. Sasa wewe unataka niamke saa 12 niwe nafanya nini mzee. Napunguza masaa ya kuteseka.

Ila siku nyingine nichane live. Sio kunisengenya huku mtandaoni tabia za kike hizo😡
 
Naomba kukuliza pia.. kwenye kikundi chenu cha vikoba wengi hutoa pesa kutoka kwenye biashara na sio kwa kuhongwa na wanaume?..

Maana ninajua list ya wadada ambao wanamaduka lakini still mtaji wao mkubwa ni kutoka kwa wanaume na biashara husika zimekuwa kama bosheni tu, maana wanaume wengine wanaamini ukimuweka mwanamke kwenye frame unamfunga miguu asichepuke kirahisi.. kuna wadada wangapi mjini ambao wauza matunda na degree zao?!
 
Wewe ndio umenena. Wazazi wanowaruhusu wapo. Shida ndio ipo kwenye jamii wanakuonea huruma sijui kama wao ndio wanafanya.
 
Hii hoja niyakitaifa
 
Mimi binafsi ni afadhali mtu anayefanya chochote kuliko mkaaji, kikubwa mazngira ya kazi yawe salama tu

Mimi binafsi mdogo wangu anayenifata amesomea nursing amefanya kazi hospital binafsi kama miaka mitano akashindwa kutokana na uonevu na kubanwa

Kaenda kuazisha mgahawa wake mahali anauza na yuko happy tu

Mimi dadake siwezi sema kazi yake anazalilika eti kisa msomi, madam ni mtu mzima ameamua mwenyewe na anapata hela afanye tu
 
Wapo hao wanaopata za kikoba kwa wanaume sikatai kila mahali wapo

Ila kuna wadada wengi tu wanapata pesa zao kwenye kaz zao

Mimi nimewaona wengi tu wengine juice, matunda, ubuyu karanga, peanut etc siyo mmoja wala wawili ni wengi mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…