Vijana wa Kiume badilikeni

Sasa anaingia kuuza matunda mtaani bila mtaji?
Hakuna mtu anaeweza kukaa kwa kupenda bila kuingiza kitu watoto wa kiume sisi misoto yetu huwezi fananisha na watoto wa kike. Mwanaume unaweza kukaa huna hata buku wiki nzima na una hujui unaipata wapi na huna kazi na kwenu mabovu.

Huwezi fananisha nyinyi watoto wa kike na watoto wa wakiume hata kidogo, unavyosema wanacheza sijui vikoba tunawaona wengi tu wanalipiwa na vidume mitaji midogo midogo ya biashara pia mnapewa na masponsor wengine hata mpaka mpaka magari.

Kwa mwanaume tena uliekulia familia ya milo milwili na wawazi wanakutegemea hiyo hela ya kuuza matunda au mama lishe unaitoa wapi kama sio uzunguke na bahasha ili upate kazi ndio upate kianzio.

Wapeni vianzio basi kama mtu anatashindwa kufanya kitu huyo kweli atakuwa na shida sio mnawasema watu tu bila kuwasidia... Mtu kaja kwako siku moja tu umeashaanza kumjaji ulitaka afanye nini sasa kama ni mgeni hapo na hana wenyeji na wala hajaja kwa ajiri ya biashara?.

Mi ndio maana kwa ndugu siendagi kabisa bora uende kwa washikaji kama huna hela ya gest.
 

Juzi tena nimepita pale Arusha stendi kuu aisee nilishangaa akina mama siku izi ndio wanabeba chaja za simu, soda, biskuti, pawa benki, edifoni, miwani, majenereta, betri za magari, injini za bajaji, nk wanatembeza kwenye mabasi. Wakati huo kwa pembeni pale kuna benchi utakuta vijana wamekaa wanapiga stori tu na kuangalia wadada wenye misambwanda wakipita wanaanza kuwapigia miluzi.
 
Nyie ni wale wale,

Siezi enda kwa mtu nikalala mpaka saa tatu hata kama sina kazi

Uwezi kuamka ukasaidia hata kuchota maji, kufagia kumwagilia maua???
Acha kutetea Ujinga
 
Mimi pia nimepita Arusha siyo siku nyingi ukitazama pale stand kuna la kunifunza

Sasa kuna siku nilikuwa nashukia pale Arusha mjini nilikuwa nina mzigo kama wa kilo 30 nikashuka nao, jamani nilivamiwa na kundi la vijana wanataka wanibebee wote ni wala ganja (wahuni hatari) kazi zao ndo hizo simple simple tu akubebee mzigo umpe buku akanunue ganja imetola hiyo
 
Hii trend ikiendelea hivi ntamuolea mwanangu mke
 
Kwakweli hali ni mbaya mnoo ...
Sana, then kama hatuzibi UFA tunakwenda kujenga ukuta siku si nyingi, coz tumeandaa kina mama kwa muda wa kutosha ila vijana wakiume wamesahaulika, sasa mama akishakuwa na nguvu economical, social, na hata kifikra ni ngumu mwanaume kukubali hiyo hali kutokana na nature

Nature inataka mwanaume awe na nguvu kiuchumi, kifikra na kimawazo alafu mwanamke awe kawaida ili maisha yaende
Dunia tunayoelekea ni kinyume chache, sasa tayari TAASISI ya familia inaharibika kuanzia kwenye Mizizi yake
 
Nyie ni wale wale,

Siezi enda kwa mtu nikalala mpaka saa tatu hata kama sina kazi

Uwezi kuamka ukasaidia hata kuchota maji, kufagia kumwagilia maua???
Acha kutetea Ujinga
Ofcoz mimi ni mtu niliepitia msoto huo mpaka kufika nilipo sasa, But issue ya msingi wasidieni basi waache kudhurula na bahasha pengine nyie hamkubahatika kuteseka baada ya shule zenu.
 
Mkuu pengine ww unajitambua lakini wengi nisifuri mm nifundi kujenga tunakutana nao tatizo lipo ndugu
 
Mtoa mada ,mtoa mada umeangalia kwa makini au umeandika andika tu?, umeshawai kumuona mwanamke akiuza ice cleam za bakhresa kwa vile vibaiskeli? Umekwenda pale buguruni ukute vijana wangapi wa kiume wanafanya kazi za kupakia ngano , ushawai kukuta gari za pespi ,koka, au za kusambaza maji wanapakia au kushusha wanawake. Ushawai unajua waendesha bajaji asilimia kubwa ni wanaume, unajua boda boda wengi wanaume ,unajua makondacta na madeleva wa daladala wengi wanaume, ukija na hoja fanya tasmini kwanza sio unakuja kubwabwajatu, kama ulikuwa hujui mwaka huu ndio tumepata rais nwanamama huko kote tulikuwa na marais wa wanume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilitoka advance nikiwa nina mhemko balaa kwamba siwezi kufundisha shule bila kulipwa Tsh 150,000 ( enzi hizo shule za kata zimeshamiri sana na hazina walimu ). Na shule nyingi zilikuwa zinalipa laki 1 mpaka 120.

Nilivyofika home nikamkuta mama anafanya kazi ya kulipwa 1,500 kwa siku yaani Tsh 45,000 kwa mwezi. Nilijiona mpumbavu sana, nakataaje Tsh 100,000 wakati mama analipwa elfu 45.

Nikaamua kwenda kufundisha, mshahara ni Tsh 100,000 ila take home ni 95,000 baada ya kukatwa elfu 5 ya chai.

Vile vile, baada ya kuhitimu chuo 2016 nilijua tu hapa nikijifanya msomi uchwara nitajuta. Nilienda oufanya kazi za ulinzi ( kampuni niliyoenda recruitment yake utafikiri unaomba kazi usalama wa taifa wakati mshahara ni 250,000 )

Yaani baada ya muda ( wakati wengine bado wanasubiri kazi za ndoto zao wakiwa wamekaa ) mimi nina mambo yangu mengine tu. Vile vile huko NSSF tayari nina kama 3M.

Dunia haijawahi kuwa na huruma na mtu yeyote.

Kaa Dar uzeeke, urudi kijijini kuongea kiingereza kwenye vijiwe vya gongo na kuwasilimulia uliomaliza nao lasaba habari za Dar. Time flies so fast.
 
Mbona kama umepanic
Soma tena bandiko tena usome kwa kutulia sana nazungumzia zaidi waliosoma wasomi wangapi wanauza hizo ice crem

Sijabwabwaja kama usemavyo hili ni janga la kitaifa kama uoni basi kaa kwa kutulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…