Sema mimi, il kuna wanaume wavivu balaa, hawataki kabisa kuchosha mwili
Tembea uone kaka
Ulichoongea ni kweli,,,janga lipo,,,ila tatizo sio hao vijana,,,,ndio ndani yao kuna wazembe,,,sikatai,,ila ndani yao kuna wengine wanamachungu sana,,,na wapo teyari kupambana,,,lakini je wazazi wao au jamii inawapa vipi support ya wao kukubaliana na ukweli kwamba elimu waliosotea miaka yote hiyo haikuwa na guarantee??!!! Koz tatizo kubwa linaanzia hapo,,,nadhani wazazi,,ndugu na jamaa wakibadirisha muonekano kwamba ukienda fanya kazi tofauti na hizi kazi rasmi basi umepotea...cause mfano ni mimi tu,,nakumbuka nilipomaliza chuo,,niliomba gari ya nyumbani aina ya IST,,nianze nayo kufanya uber,,,lakini nilipata vita kubwa sana toka kwa wajomba na ndugu wengine wakisema kazi gani hiyo ya watu wasiosoma,,na wajomba walileta vita kali kwa bibi ili anipokonye ile gari,,nikajitafutie mwenyewe koz kunisomesha inatosha...na kweli ilifika point ilibidi niirudishe tu ile gari,,nikarudi kwenye ulofa....kuna kipindi pia nilianza uza viatu online,,kupitia page ya instagram,,nikawa topic upya kwa familia,,,mama akaona nimefeli kabisa maisha,,cause I could sense it in her talks....So usitupe lawama kaka,,mwite pembeni,,muulize biashara gani ambayo angeweza ifanya,,then mpe mtaji au mchongo utaomuwezesha kupata mtaji,,then uone kama ataboronga au vipi