Vijana wa miaka 20-29 tukutane hapa

Vyema kabisa umenena, tena umegusia suala la Mfumo wa elimu..ni kweli kabisa elimu yetu Tanzania haimuandai mwanafunzi kuja kujitegemea vyema hapo baadae badala yake ni kumfanya asubiri kuajiriwa..

Hili jambo sema la ukweli sio zuri sana...Hii ni kutokana na kuwa wadau wengi walipendekeza mfumo wetu wa elimu ubadilishwe na sera zake lakini cha kushangaza hadi leo kila mwenye mamlaka akija anakuja na sera zake jambo ambalo linafanya taifa kutokuwa na SERA YA MADHUBUTI NA YA KUELEWEKA YA KIELIMU..

Katika dunia ya sasa masomo ya ufundi stadi na ujasiriamali ni muhimu sana katika kumsaidia mwanafunzi kwa siku za baadae kuwa na fani yake na kujitegemea, hivyo kuondoa ile kasumba ya kuzoea kuajiriwa kazi za ofisini
 
Reactions: Cyb
Hongera kwa ufafanuzi mzuri, nimependa maelezo yako[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kweli mpenzi mtaala wa elimu yetu ungetiliwa mkazo kwenye kujiajili ingesaidia sana
 
Kwakuwa nami kijana na nimjasiliamali mdogo na ninachofany mtu yoyot anaweza fanya na kikamletea faida kwa mtaji mdogo sana,ataekuwa tayari anitafute tugawane maujanja
 
Kwakuwa nami kijana na nimjasiliamali mdogo na ninachofany mtu yoyot anaweza fanya na kikamletea faida kwa mtaji mdogo sana,ataekuwa tayari anitafute tugawane maujanja
Mkuu kamaa hutojali ..Fanya kushare na sisi hayo maujanja, kwa ni itasaidia kujifunza jambo jipya.
 
Kwakuwa nami kijana na nimjasiliamali mdogo na ninachofany mtu yoyot anaweza fanya na kikamletea faida kwa mtaji mdogo sana,ataekuwa tayari anitafute tugawane maujanja
Mimi hapa naomba hayo maujanja,au ungeyaweka hapa ili kila mtu apate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…