Vijana wa zamani tukutane hapa - old school

Pool side(k'njaro Hotel), Whitesands Hotel Disco
 
Kibonde huyu wa clouds...?
 
waigizaji kama fred williamson, jim kelly,mwana dada pam grier,bo sevenson, amita,hema malin,vinod,ponam walikuwa juu, sinema kama black ceaser, three the hardway,enter the dragon,black samurai,amar akbar antony,dilwale,sholay nk.
Umemsahau Chuck Norris
 
Naona umemsahau na Dj Chriss Phaby, pale msasani club,kuhusu matangazo hata 1900,nao walikuwa juu kwa matangazo, ma mchoraji wao aliyekiwa akiwa chorea matangazo ni mchagaa mmoja akiitwa Mwitori nakumbika alikuwa akiishi Sea view,nakumbuka kipindi kile madisco yote yalikuwa na grade na kuna watu ilikuwa huwezi kuwa kuta pale Continental au Keys,ila watu wa keys na continental utawakuta kote,kipindi hicho Dar ilikuwa bandari salama kweli mwanamke alikuwa almasi,ukipaki gari nje ukumbi mzima utajua wewe ndio mwenye gari.
 

Haaaa haaa umenikumbusha

Enzi hizo SPACE 1900 na kipindi hicho Break Dance kwa kwenda mbele na Funks kibao.

Nakumbuka kuna siku Chris Phabby alikuwa amerudi toka Zimbabwe basi akutuambia mashabiki kuna style ya kucheza amekuja nayo toka bondeni. Basi akaigia mtu kati, alipiga shoo balaa.

Wapi siku hizi hii mtu Chriss Phabby?
 
Umemsahau Chris Phabby the lover
 
Nakumbuka Baltimora-WimboTarzan Boy (oh oh oh oh oh hoh ooooh...) nikiwa Form one 1986 tulikuwa tunacheza Funky hatari
 
Dhaaaa!!!! Madisco ya
Primary n hatar aiseee
Stak hata kuyakumbuka
 
Dah! umenikumbusha mbali sana aisee ntarudi muda si mrefu.
 
Nakumbuka Baltimora-WimboTarzan Boy (oh oh oh oh oh hoh ooooh...) nikiwa Form one 1986 tulikuwa tunacheza Funky hatari
Tarzan Boy ulikuwa ni moja ya nyimbo pendwa sana kutoka kundi hilo la Baltimora. Wimbo mwingine mkali kutoka kundi hilo ni Woody Woogie.

Ni bahati mbaya sana kwamba mwimbaji kiongozi wa kundi hilo na katika nyimbo hizo alifariki katika umri mdogo baada ya kupata maambukizi ya ukimwi yaliyosababishwa na ushiriki wake katika mapenzi ya jinsia moja. Alifariki zaidi ya miaka 20 iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…