Vijana Wamegeuzwa Watumwa wa Mfumo Uliokufa – Ni Wakati wa Kuishtaki Akili ya Taifa!

Vijana Wamegeuzwa Watumwa wa Mfumo Uliokufa – Ni Wakati wa Kuishtaki Akili ya Taifa!

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Ni aibu, ni fedheha, ni upuuzi wa hali ya juu kabisa kuona taifa linaloitwa “lenye dira na maendeleo” linaendelea kubeba mizigo ya wazee vilaza wanaoshikilia vyeo kana kwamba ofisi za umma ni milki zao za kifamilia! Vijana wasomi, wenye critical thinking, innovation mindset, na uwezo mkubwa wa kuendesha mifumo ya karne ya 21, wanasota mitaani – wakibuni njia za kuishi ilhali serikali hiyo hiyo inawakamua kodi kila siku bila hata aibu!

Jamani, where is the logic? Serikali inakusanya kodi kutoka kwa vijana ambao haina hata mpango wa kuwapa nafasi za kufanya kazi. Huu ni unyonyaji wa kiakili, kiuchumi, na kimaadili. Ni kama kuwanyima nafasi ya kupumua halafu unawatoza kodi kwa hewa wanayopumua!

Kuna vijana wamesoma Data Science, Artificial Intelligence, Renewable Energy, Public Policy, Cybersecurity lakini waliopo ofisini ni wale wanaoshindwa hata kuandika email bila kuuliza “hii inatumwa vipi?”. Hawa ndio wanaotengeneza policy decisions za taifa. Hawa ndio wanaopewa nafasi za “ushauri wa kitaalamu”! Sasa kweli, unategemea taifa litokeje gizani?

Vijana wamejazwa potential energy isiyotumika, wakati wazee wamekuwa dead weight ndani ya mfumo. Wamekalia vyeo kama viti vya enzi, hawataki kustaafu, hawataki kuachia, hawataki kujifunza. Wengine hawasomi tena vitabu, hawafuatilii dunia inavyoenda, hawana capacity for innovation lakini bado ndio “decision-makers”!

Tafakari: vijana wanateseka, wanakatishwa tamaa, wanageuzwa vichekesho. Hata fursa ndogo ya internship inakuwa kama kupigania urais!
Na cha kushangaza zaidi, serikali inajifanya kama kila kitu kiko sawa. Inazungumza kuhusu “ajira kwa vijana” kwenye makongamano yenye air condition na snacks za bure, huku vijana walioita “wahusika wakuu” hawana hata nauli ya kufika ukumbini!

Enough is enough. Wakati umefika wa kuvunja huu mfumo wa ukiritimba wa wazee vilaza waliokatazwa na dunia lakini wanakimbilia ofisini kama mapacha wa urasimu. Vijana wa Tanzania si wajinga. Tunajua, tunaona, tunachoka.

If the system cannot reform itself, then the youth will reform the system by force of intellect, resilience, and historical necessity.
 
Kuna fear of competence karibu kila mahali, kwa sababu dunia inahama sasa hivi kwenda kwenye competence based performance.
 
Back
Top Bottom