Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Nna mwaka sasa toka niache kazi na kufanya shughuli zangu binafsi

Kwa kweli Niko vizur sana na nna amani sana tena Sana,japo kujiajiri kunachangamoto zake lakini kuajiriwa zimezidi

Kwa nini niliacha kazi

Niliacha kazi baada ya mambo matatu makubwa

1#nilipokua naanza kazi kwenye ofisi flani ivi nilibahatika kupata rafiki yangu wa kichaga maeneo Yale yeye hakua na elimu yoyote alikua tu mfanyabiashara

Tena wakati uo ana mtaji wa miliona moja nakumbuka nilikua nikimwazima sana mshahara akunulie mzigo baadae anirudiahie

Baada ya miaka mitatu mtaji wake ukapanda toka milioni moja hadi milioni tisini

Wakati huo mwenzangu na Mimi ndo kwanza nimeongezwa kamshahara toka laki nane hadi laki Tisa

Baada ya mwaka moja kupita jamaa kajenga nyumba nzuri,anagar zur,na anaagiza mzigo kutoka China anamtaji ya milioni mia sita,wakati huo Mimi naangaika tu na laki Tisa yangu

Nikanza kujichukia nikaanza kuichukia elimu niliyoipata maana bado sijaona umuhimu wake kwenye maisha yangu

Dalasa LA saba ameweza kumanage business from 1m to 600m ndani ya miaka minne tu

Inaendelea
Inspirational
 
Binafsi nimepanga kuacha kazi 2020 (doctor)

Sababu

Uhuru sina na kama upo ni finyu sana.
Waajiriwa wengi ni maskini sana ,wanaishi maisha ya hovyo na mawazo ni finyu sana,hawana muda wa kupata mentors wa kuwapatia elimu ya biashara au vitu vya kufanya ili kupata kipato.

Nimeamua kufanya haya before sijaacha.

Now nipo na hekari 22.5 za Miti aina ya paini nahitaji zifike hekari 100 by 2020.

Then nashukua mkopo mrefu na kuacha kazi.

Nawasilisha.
 
Binafsi nimepanga kuacha kazi 2020 (doctor)

Sababu

Uhuru sina na kama upo ni finyu sana.
Waajiriwa wengi ni maskini sana ,wanaishi maisha ya hovyo na mawazo ni finyu sana,hawana muda wa kupata mentors wa kuwapatia elimu ya biashara au vitu vya kufanya ili kupata kipato.

Nimeamua kufanya haya before sijaacha.

Now nipo na hekari 22.5 za Miti aina ya paini nahitaji zifike hekari 100 by 2020.

Then nashukua mkopo mrefu na kuacha kazi.

Nawasilisha.
But am in research in kuhusu mkopo.

Nipo serikarini nawaza nikichukua mkopo na kuondoka watanitafuta?
 
Kutoka kwenye ajira inahitaji maamuzi magumu,kabla hujaacha kazi anzisha biashara au mradi ambao utausimamia na ukaona faida yake inakuwaje na kama umepata hasara urekebishe wapi.Kwa sababu Mara nyingi biashara haikuwi Mara moja,ni kusimama na kuanguka.Tafakari kabla.
 
Heshima kwenu viongozi

Nimeona ni vyema na sisi wenye lengo la kuacha kazi tukawa na uzi wetu kama wenye agenda nyingine walivyoanzisha uwanja wao.

Lengo la nyuzi hii ni kupeana mawazo, moyo na uzoefu wa mbinu bora tunazotumia katika maandalizi yetu ya kuachana na aina Mpya ya utumwa, yaani KUAJIRIWA.

Lengo lingine la uzi huu ni kuonesha sababu ya uamuzi wa kutaka kuacha kazi ili kila mtu apime kama sababu yake ni sababu tosha ya kufanya hivyo ama la, lakini hii pia inatoa fursa kwa wachangiaji wengine kufanya assessment ya maamuzi hayo.

Kuacha kazi na kujiajiri na pengine baadae kufikia hatua ya kuajiri ni uamuzi wa kuyatoa maisha yako mikononi mwa mtu mwingine (muajiri) na kuyakabidhi mikononi mwako mwenyewe. Ni kujitoa katika kutawaliwa na kuamua kujitawala mwenyewe. Ni vyema pia tukajulishana gharama za maamuzi hayo mazito ya kutoka Misri kuelekea Kanani. NI WAZI HAITAKUWA SAFARI NYEPESI.

Tushauriane time scale, mfano mimi ninakimbizana na miaka Mitatu kabla sijatoka kwenye hii Jela. Baada ya hapo ntarudi uraiani, nyumbani kuishi maisha yangu ya uhuru.

Tunaotaka tutoke hii Jela Tushauriane humu, je tukusanye mtaji sasa bila kufanya ujasiriamali na tutakapoacha tu kazi ndio tuanze rasmi ujasiriamali? Ama tuanze sasa hivi kufanya kazi na ujasiriamali ili tu-taste ladha ya ujasiriamali kabla hatujaacha kazi? (Ila hata mambo yakiwa magumu kwenye ujasiriamali kipindi tupo kazini na tunafanya ujasiriamali, kuendelea na kazi sio option). Kubaki Jela haiwezi kuwa option kisa kuna dona na maharage ya bure, bora kuwa uraiani ule mlo mmoja wa maharage na ugali kwa mwaka mmoja ili uje kula asali na maziwa kwa miaka mingi ijayo.

Kila mtu anaweza kuwa na sababu yake ya kuacha kazi. Wengine watakwambia kazini kipato kidogo, lakini amini nakwambia hata ukiajiri na kutoweka mwili, moyo na roho yako kwenye hiyo kazi, unaweza kupata kipato kidogo kuliko hata kile cha kazini. Katika swala la kipato, tofauti ya kipato cha kuajiriwa na kujiajiri ni kipato kimoja Anapanga mtu akulipe kiasi gani, na Kingine Unapanga wewe uingize kiasi gani.

Wengine watakwambia, wanataka waache kazi sababu ya Mateso kazini,ubabe wa mwajiri, kutojali kwa mwajiri. Yote hayo yanakupa HASIRA, geuza hasira zako kuwa DRIVES, zigeuze kuwa USONGO.

Kwanini nataka niache kazi, nataka kuwa huru, nataka kusafiri huku na kule bila kujali bosi atahesabu siku tatu sipo kazini anifute kazi. Sitaki kumpigia mtu mmoja Magoti (bosi) ili kipato changu kiendelea kutiririka. Bora nipigie magoti watu wengi (wateja) ili kipato kiingie, kwani mteja mmoja akiamua kunifukuza kazi ntakuwa na option kwa mteja mwingine.

Uzi wetu TUNAOPANGA KUACHA KAZI, the clock is clicking....LET'S DO IT, LET'S GO.... Tunapenda pia kuchota busara za wale walioacha kazi na wapo wanaendelea kupambana.
Mimi ni mmoja kati ya watu walioacha kazi mwaka mmoja sasa,jiandae na:

1) kusikiliza moyo wako kuliko mtu mwingine yeyote.

2) jiandae kupambana kwa bidii zaidi kuliko bidii uliyonayo ktk kazi ya kuajiliwa

3) jiandae kutumia pesa kidogo sana kukidhi mahitaji yako lakini pia uingize kingi zaidi ya utumiacho

4) jiandae kua muaminifu zaidi na mkweli kwa watu ili kusafisha njia ya wewe kupita,sambamba na hilo jiandae kua mkorofi pia pale utakapo dhurumiwa kwa sababu ya upole wako

5) jiandae kuiepuka tamaa ya vitu vingi vya anasa ulivyozoea kuvifanya kwa uzembe ukitegemea mwisho wa mwezi utapata tena pesa

Uwe na siku njema.
 
Kujiajiri ni kuzuri lakini uhakikishe umeagana na nyonga. Usipochukua risks basi ujue hautafanikiwa siku moja. Ni kuamua, lakini ujue kuwa "ajira uliyonayo leo ni mtaji kwa ujasiriamali wako unaoufikiria kwa sasa hivyo anza ujasiriamali ukiwa kazini usiache kazi kabla ya kujua mwelekeo wa huo ujasiriamali. "
 
Wakuu.. nimekutana na changamoto moja,
Mi ni electrical engineer sina mda mwingi mtaani... na ndoto zangu ni kujiajiri kwenye fani yangu.... lakin kabla hata sijaanza hizo harakati... ametokea mjomba... anataka kunipeleka jeshin... ndugu, marafiki woote wananisukuma niingie huko.... lakin mi roho inaniuma, maana sijajaribu ndoto yangu.
Nikijaribu kuwashirikisha ninachotaka kukifanya, kila mtu ananiambia nikijiajiri ntashindwa maisha.... jesh ndo nafas pekee ya kufanya maisha... nikishapata nyota zangu ntalipwa ela ndefu..
Kimsingi sielewi nifanye nin kwenye kona hii...
 
Wakuu.. nimekutana na changamoto moja,
Mi ni electrical engineer sina mda mwingi mtaani... na ndoto zangu ni kujiajiri kwenye fani yangu.... lakin kabla hata sijaanza hizo harakati... ametokea mjomba... anataka kunipeleka jeshin... ndugu, marafiki woote wananisukuma niingie huko.... lakin mi roho inaniuma, maana sijajaribu ndoto yangu.
Nikijaribu kuwashirikisha ninachotaka kukifanya, kila mtu ananiambia nikijiajiri ntashindwa maisha.... jesh ndo nafas pekee ya kufanya maisha... nikishapata nyota zangu ntalipwa ela ndefu..
Kimsingi sielewi nifanye nin kwenye kona hii...
Mkuu kwanza hongera kwa dhamira yako uliyonayo.

Kwa maoni yangu naona, ili mtu akushauri vizuri, kwamba uendelee kufanya kazi jeshini ama laa inabidi ajue mambo mengi kuhusu wewe mfano kwa jinsi familia yako ilivyo, yaani kama una pa kuanzia? Kwa maana ya mtaji ulionao. Tumeshafahamu maarifa ya huo ujuzi unayo.

Let's say una mtaji wa kuanzia, au yupo mtu wa kukupa mtaji wa kuanzia..... Utakuwa na haja gani ya kwenda huko kwenye amri ambapo haparuhusu mdogo ku reason na mkubwa, hata kama mkubwa anaenda chaka. So kama una pa kuanzia financially go direct for your dream Broo, ingawa inabidi utafiti hiyo industry ya electrical engineering kama ina lipa ama laa.

Option ya pili ni kuingia jeshini, hii njia nakushauri Ifuate kama tu huna pa kuanzia, hapa namaanisha mtaji. Kwani wewe hautakuwa boss of yourself wa kwanza kuanza kwa kuajiriwa na kisha kutoka na Kujiajiri mwenyewe. Hapa pia sijajua kwa jeshini ipoje, kama once you are in..... there is no way you get out and become a a normal civilian au inaruhusiwa kuacha kazi ya jeshi kama zilivyo kazi nyingine.

Kama jeshini inarusiwakuacha kazi jipe miaka 5, kusanya mtaji, kisha rudi uraiani kupiga mishe. Ila be careful, usinogewe na ka mshahara ka vimilioni na ration ya laki nne ukasahau ndoto yako. BEST LUCK FRIEND.
 
Back
Top Bottom