Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Inspirational
 
Binafsi nimepanga kuacha kazi 2020 (doctor)

Sababu

Uhuru sina na kama upo ni finyu sana.
Waajiriwa wengi ni maskini sana ,wanaishi maisha ya hovyo na mawazo ni finyu sana,hawana muda wa kupata mentors wa kuwapatia elimu ya biashara au vitu vya kufanya ili kupata kipato.

Nimeamua kufanya haya before sijaacha.

Now nipo na hekari 22.5 za Miti aina ya paini nahitaji zifike hekari 100 by 2020.

Then nashukua mkopo mrefu na kuacha kazi.

Nawasilisha.
 
But am in research in kuhusu mkopo.

Nipo serikarini nawaza nikichukua mkopo na kuondoka watanitafuta?
 
Kutoka kwenye ajira inahitaji maamuzi magumu,kabla hujaacha kazi anzisha biashara au mradi ambao utausimamia na ukaona faida yake inakuwaje na kama umepata hasara urekebishe wapi.Kwa sababu Mara nyingi biashara haikuwi Mara moja,ni kusimama na kuanguka.Tafakari kabla.
 
Mimi ni mmoja kati ya watu walioacha kazi mwaka mmoja sasa,jiandae na:

1) kusikiliza moyo wako kuliko mtu mwingine yeyote.

2) jiandae kupambana kwa bidii zaidi kuliko bidii uliyonayo ktk kazi ya kuajiliwa

3) jiandae kutumia pesa kidogo sana kukidhi mahitaji yako lakini pia uingize kingi zaidi ya utumiacho

4) jiandae kua muaminifu zaidi na mkweli kwa watu ili kusafisha njia ya wewe kupita,sambamba na hilo jiandae kua mkorofi pia pale utakapo dhurumiwa kwa sababu ya upole wako

5) jiandae kuiepuka tamaa ya vitu vingi vya anasa ulivyozoea kuvifanya kwa uzembe ukitegemea mwisho wa mwezi utapata tena pesa

Uwe na siku njema.
 
Kujiajiri ni kuzuri lakini uhakikishe umeagana na nyonga. Usipochukua risks basi ujue hautafanikiwa siku moja. Ni kuamua, lakini ujue kuwa "ajira uliyonayo leo ni mtaji kwa ujasiriamali wako unaoufikiria kwa sasa hivyo anza ujasiriamali ukiwa kazini usiache kazi kabla ya kujua mwelekeo wa huo ujasiriamali. "
 
Wakuu.. nimekutana na changamoto moja,
Mi ni electrical engineer sina mda mwingi mtaani... na ndoto zangu ni kujiajiri kwenye fani yangu.... lakin kabla hata sijaanza hizo harakati... ametokea mjomba... anataka kunipeleka jeshin... ndugu, marafiki woote wananisukuma niingie huko.... lakin mi roho inaniuma, maana sijajaribu ndoto yangu.
Nikijaribu kuwashirikisha ninachotaka kukifanya, kila mtu ananiambia nikijiajiri ntashindwa maisha.... jesh ndo nafas pekee ya kufanya maisha... nikishapata nyota zangu ntalipwa ela ndefu..
Kimsingi sielewi nifanye nin kwenye kona hii...
 
Mkuu kwanza hongera kwa dhamira yako uliyonayo.

Kwa maoni yangu naona, ili mtu akushauri vizuri, kwamba uendelee kufanya kazi jeshini ama laa inabidi ajue mambo mengi kuhusu wewe mfano kwa jinsi familia yako ilivyo, yaani kama una pa kuanzia? Kwa maana ya mtaji ulionao. Tumeshafahamu maarifa ya huo ujuzi unayo.

Let's say una mtaji wa kuanzia, au yupo mtu wa kukupa mtaji wa kuanzia..... Utakuwa na haja gani ya kwenda huko kwenye amri ambapo haparuhusu mdogo ku reason na mkubwa, hata kama mkubwa anaenda chaka. So kama una pa kuanzia financially go direct for your dream Broo, ingawa inabidi utafiti hiyo industry ya electrical engineering kama ina lipa ama laa.

Option ya pili ni kuingia jeshini, hii njia nakushauri Ifuate kama tu huna pa kuanzia, hapa namaanisha mtaji. Kwani wewe hautakuwa boss of yourself wa kwanza kuanza kwa kuajiriwa na kisha kutoka na Kujiajiri mwenyewe. Hapa pia sijajua kwa jeshini ipoje, kama once you are in..... there is no way you get out and become a a normal civilian au inaruhusiwa kuacha kazi ya jeshi kama zilivyo kazi nyingine.

Kama jeshini inarusiwakuacha kazi jipe miaka 5, kusanya mtaji, kisha rudi uraiani kupiga mishe. Ila be careful, usinogewe na ka mshahara ka vimilioni na ration ya laki nne ukasahau ndoto yako. BEST LUCK FRIEND.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…