Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Ambapo nitakuwa nimeitumikia serikali kwa muda wa miaka 10 tangu niajiriwe mnamo mwaka 2015
 
Tunaotaka tutoke hii Jela Tushauriane humu, je tukusanye mtaji sasa bila kufanya ujasiriamali na tutakapoacha tu kazi ndio tuanze rasmi ujasiriamali? Ama tuanze sasa hivi kufanya kazi na ujasiriamali ili tu-taste ladha ya ujasiriamali kabla hatujaacha kazi? (Ila hata mambo yakiwa magumu kwenye ujasiriamali kipindi tupo kazini na tunafanya ujasiriamali, kuendelea na kazi sio option). Kubaki Jela haiwezi kuwa option kisa kuna dona na maharage ya bure, bora kuwa uraiani ule mlo mmoja wa maharage na ugali kwa mwaka mmoja ili uje kula asali na maziwa kwa miaka mingi ijayo.
nadhani kama upo jela pambana kukusanya mtaji meanwhile anzisha ujasiriamari mdogo uendenao mpaka pale utakapoamua kuondoka jela
usitamani kukaa jela zaidi ya miaka mitano iwe pungufu ya mitano
 
Inasikitisha kuona wengine wanatamani kuingia angali wengine wanataka kutoka
 
Bado kitambo kidogo niachie kazi...ki ukweli nimechoka kufanya kazi huna amani ni sawa na kuishi na mke mliyeshindana bora nikafuge ngo'mbe wa maziwa miradi niipendayo!
 
Katika maisha yangu mpaka sasa na kwa umri huu niliajiriwa mara moja,.sikuwahi kufurahia maisha ya kazi yangu aisee nilijiona mtumwa waziwazi doh,.lakini katika hayo nilijifunza vitu..sasa niko kusimamia malengo/maono na ndoto zangu kwa muda mwingi na kwa nguvu zangu zote nikiwa nimezielekeza katika hayo..safari ni taaaam[emoji4][emoji4]nilijiona nimecheleeeewaa kumbe aah,..Ahsante Jehovah.
 
Umesema kitu sahihi, mara nyingi ukiwa kwenye ajira huku ujasiriamali watumishi wanakuumiza, hii ndiyo changamoto kubwa kwa aliyeajiriwa na kufanya uhasiriamali kwa sababu muda wa kusimamia uwekezaji wako unakuwa mdogo saana! Labda kama umeoa/kuolewa hivyo mmoja wenu ahusike kwa asilimia nyingi zaidi wakati mnajiandaa kuacha kuajiriwa. Haya yameshanikuta zaidi ya mara moja [emoji17]
 
Kingine ni nidhamu ya woga kwa tulio wengi, binafsi naandaa mazingira ya kujiajiri wakati bado nimeajiriwa, mambo si mepesi kiivyo lakini inawezekana ikiwa umefanya uchaguzi sahihi kulingana na wito unaousikia ndani yako. Binafsi napambana kuweka miundombinu itakayonipatia fedha ya kula na kujikimu mahitaji yangu muhimu kama baba anayetegemewa na familia na kisha nafanya uamuzi wangu mzima.
 
Hahaha asante, kiukweli ili uonekane ni lazima uwe umefanya kitu cha tofauti
 
Mkuu kukata tamaa ni kosa la jinai

Kuweka miundo mbinu ni kutengeneza njia sahihi

Kujiajiri ni sehemu ya kutimiza unacho kiamini

Kuajiriwa ni sehemu ya kutengeneza mandalizi ya kwenda unapo amini panatakiwa uwe

Amua kwa busara tekeleza kwa uafanisi
 
Ndugu zangu. Swala LA kuacha kazi linahitaji kujipanga sana, huwa siwashauri watu wakurupuke kwani yaliyonipata sipendagi na wengine yawapate
Kuna wazo huwa naliwaza kuhusu ajira na kujiajiri, kwanza kujiajiri kutokana na ujuzi ulionao mf:- dereva wa gari aliyeajiriwa kuamua kuacha kazi ya kuajiriwa na kununua gar yake na kufanya taxi (kuikodisha) na kuendesha mwenyewe (uber) au kujiboresha kwa kuongezea status ya fani yake na kuwa na ushindani mkubwa katika soko la ajira hivyo kuwa mchaguzi wa aina fulani ya kazi itakayo mpatia muda wa kusimamia mradi wake na bado ikamlipa vizuri [hii ni katika kutafuta ujasiri wa kifikra wa kuanza kujiajiri] na mwisho kuwa na mtaji wa kutosha na taarifa kamili ya kile unachotaka kukifanya.
 
Aisee, maandalizi umeyafanya kwa muda gani mkuu

Mkuu sijajiandaa kihivyo,

Nimekuwa mjasiliamali kwa muda sasa nikiwa kazini,

Nimekuwa nikijihusisha na kilimo cha matunda lakini napata hasara sana,

Lakini hiyo hasara haitokani na ubovu w bidhaa la hasha ni usimamizi mbovu

Watu wengi nnao waamin mpaka leo ndo wengi wao wananiliza,

Kimahesabu kwa nikifanya kilimo kwa mara moja naweza pata pesa ya mshahara wa mwaka mzima,

Kwanini niendelee kubaki kazini wakati naona kuna sehemu naweza kupata pesa ya kutosha nzuri tu,
 
Halafu kitu kingine kinachoweza kuwa ni changamoto wakati mwingine lakini, ni namna ya kuhamisha mazingira ya mwandishi wa kitabu kutoka kwao na kuyaleta katika mazingira ya kiafrika ama kitanzania ili mawazo hayo yaweze kuendena na wewe
 
Huyo Aunt yako hajui unayoyapitia. Anataka uendelee kubeba huo msalaba wa moto (kuajiriwa) shingoni.
 
Changamoto ingine ni mambo ya kuigana, unataka kuwa kama fulani wakati wewe siyo huyo fulani! Ni vizuri kufanya kile unasikia kabisa ndani yako hasa wakati ukiwa na utulivu ili upate kijitathimini mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…