Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

salute mkuu. Nimekusoma vyema sana. Vp una muda gan kazini
 
acha na jiajiri,ila hakikisha ile sehem utakoyofungua kiwanda au kampuni weka bendera ya ccm,
ukienda kinyume na wao huchukui muda watakufilisi.

akina wenzenu wameanza kuhamia nchi jilani.

WEWE KAMA UMEBAHATIKA UNA KAZI,USIACHE CHUKUA MKWANJA ANZISHA BIASHARA ,KAZI IBAKI KAMA DHAMANA.

HUKU UWE.ANASILIZIA KWANZA HADI HUU UPEPO MCHAFU ULIOBAKIZA MIAKA KADHAA UPITE.

MAANA NCHI IPO KWENYE GUNDU LA HALI YA JUU KABISA.
 
Na kwa hivi sasa huu mfumo unaokuja si mchezo. Mpaka uje upate unachokitarajia mgongo umeshapinda na nguvu zimekwisha
 
hongereni,mie cha kuwashauri kabla hujaingia mazima kwenye kujiajiri,uwe kama mtoto anayeachishwa ziwa,unaintroduce vyakula vingine taratibu,fanya uchunguzi wa biashara unayotaka kufanya,ujue nini cha ku expect ,changamoto zake,nakushauri uchukue hata likizo isiyo na malipo,ambapo utaangalia unachojiajiri kiko na mashiko,sitaki muache kazi kabisa,afu ukute changamoto za kujiajiri huziwezi....utakua umepotea sana..
 
Saa zingine ikiongea kwa uchungu namna hii unawaamsha wengi! Kwa sababu ndiyo uhalisia ulivyo. Kazi kubwa mapato kidogo! Ila kuacha kazi si jambo la hisia tu, linatakiwa kuwa jambo halisi lenye uhakika wa kile utakachoenda kukifanya
 
Kuacha kazi utegemea mazingira ya mwajiriwa na wanaomzunguka, ikiwa mwajiriwa atazungukwa na wajasiriamali basi uwezekano wa kuacha kazi na kufanikiwa ni mkubwa kinyume na hapo uwezekano ni kama kucheza kamali ya ku-bet!
 
Ushauri wako uko vizuri
Asante mkuu
 
Mm pia niko katika plan ya kuancha kazi nilikuwa bank kutokana na kifanyishwa kazi kama punda kila siku nikaacha sasa nikapata kwa government na sasa nimechoka napoke 400,000/= na point ukichanganya na posho 300,000/= jumla kama 700,000/= mkopo wanakata 200, 000/= take home 500,000/=
Nauli kwa siku 6000/*30 Msoc kwa siku ofcn 6000/ *30 matumizi mengine kama 3000 ukipiga kwa mwezi 450,000/ nabakiwa na 50,000
Watu tunafanya miujiza

CHALLENGE
NIna carwash ambayo kwa siku inaingiza 25000/ per day nilipo kuwa likizo nikaona inaingiza haidi 40 per day nakuwa naweza kusave nyingi tu nyingi kama 30000/ sasa naona kabisa nahitaji kuwa huru ili niweze kuweka pesa yakutosha na mambo yakenda
 
Mbona sijaelewa maana kuna misamiati migumu kwa mfano umetumia "walinipandilia" ndo nini?
 
Mku Jimmy Mzigo wa Kuni tani kama mbili kwa Maeneo ya Mwenge utaniletea kwa bei gani
Ni ndg sana hizo .. Gar itayokutoa faida kiwango cha chini n tani tatu na nusu ...mizigo 60 had 70 kuni 1600 na kuendelea
 
Hivi siku hizi bado kuna likizo za bila malipo??
 
Asante sana mkuu, nimeichukua hiyo, pole pia na wewe hakuna kukata tamaa
Kwenye biashara ndugu kushindwa ndo kuweza.. Mm niliye shindwa kutokana na huyo dogo nime jifunza kitu tuyari kwa nn huyo dogo alinifanyia hivyo katika biashara yangu so amenipa somo tayari.. Badala ya kunipa pole ulitakiwa unipe hongera kwa kujifunza kitu kipya.. Mm niliye anza na kushindwa n bora sana kuliko yule anaye ghairisha kufanya biashara kila siku Kiyosaki Robert ana kwambia ktk kitabu chake kuwa ushindwe kwanza.. Kuna mwingine jina lime nitoka kidogo yeye ana kwambia siku zote ukitaka kujifunza jambo jema kwenye biashara pendelea kusoma story za watu walio shindwa na sio walio fanikiwa.. Ukisoma za walio shindwa kuna masomo mengi utajifunza mazuri zaidi kwann wao wakishindwa na wewe ufanyeje ili ucwe kama wao
 
Kwa mtazamo wangu inawezekana kabisa kufanya biashara fulani hata ukiwa kazini wengi wetu tunajisahau tukipata kazi then siku ukija kitaa ndo tunajilaumu kwamba pengine ningekuwa bado kazini ningeweza kufanya jambo fulani,,,, tuchukue hatua leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…