Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Inabidi uende sober house
 
'Acha kazi uone kazi kupata kazi'.
neno langu naomba liheshimiwe jamani wandugu plzzzzz
ila karibuni sana mtaani tunawapenda na tutawaonesha ushirikiano

usiishi kwa facts ambazo hazina kichwa wala miguu, uoga wako ndo umaskini wako!
 
Point
 
Binafsi nafikiria kuacha kazi ya ualimu miaka minne ijayo,kipindi ambacho shamba langu la kisarawe heka nane na nusu litakuwa tayari limeanza kutoa nazi za kutosha, kwa sasa tayari nna nyumba moja ya vyumba 11 ipo msongola, na nafanya biashara ndogondogo za food products ambazo zinaenda vizuri.
 
Hongera sana.
Kwangu ni hivohivo pia. Nilijiwekea lengo ifikapo 2020 niwe nishaacha. Namshukuru Mungu kunitia ujasiri kuacha rasmi mwezi uliopita. Tangu tarehe 1 April 2018 nimeingia mtaani mazima. Japo hakuna anayenielewa... Wanadhani nimechanganyikiwa.
 
Hongera mkuu. Najua changamoto ya kwanza ni ndani ya nyumba yako mwenyewe na ndugu wa karibu lazima watakupinga. Uwe na msimamo na ujasiri. Kumbuka kuwa haitakuwa rahisi na wala hutapita kwa haraka but eventually you will get through all the difficulties of this transition phase.

Mwisho watakuelewa tu. Mimi bado naendelea kupambana na malengo na muda. Naamin kwa jina la mwenyezi MUNGU ndoto yangu itatimia sawa sawa na mapenzi yake.
 
Nilifanya kazi miaka 10 mafanikio hakuna nilistuka nakuuamua kuacha maana mafanikio yangu yalikua hakuna zaidi ya kula na kuwa smart kimavazi na kulipa kodi za nyumba tuu,
Namshukuru Mungu kwa yale maamuzi
 
Wengi wanafanyia kazi ile tunaita addiction..yaani mazoea,lakini amini nakuambia ajira nyingi utalipwa ili uendelee kuwa tegemezi! Tukija Kwenye kujiajiri wengi ni waoga na kushikiwa akili..siku zote sipendi kumshirikisha dili zangu mtu muoga coz najua atazingua tu..
Masikini wengi wanamiliki liabilities badala ya assets kwa maana ya vitu vinavyowamalizia pesa badala ya kuwa na vitu vinavyoingiza pesa....trust me maisha ni kuamua..you should be a risk taker in order to be Rich!
 
Kama hukubahatika kupata watu sahihi lazima uone usimamizi ni ngumu lakini kuna ngumu zaidi ya usimamizi fikiri sana!
 
Tupe experience mkuu. Vip kuhusu ule mkopo wa benki
 
kwa usawa wa maisha unaweza. Ukitoka kazini saa tisa, unaingia shambani, unalima, unakagua mifugo n.k
Unaweza kufanya hivyo kwa mradi au biashara ndogo lakini kadri mradi au biashara yako itakavyopanuka na kukua ndivyo utahitaji muda mwingi wa kumanage mambo mbalimbali ya hiyo biashara yako. Kama umeajiriwa na biashara yako ikahitaji muda zaidi wa kui operate lazima tu utaanza kukwazana na mabosi wako. Labda kama malengo ya biashara yako ni kukuwezesha kupata hela ya kununua kiberiti na chumvi, lakini kama una malengo ya kuwa na biashara au mradi mkubwa kuajiriwa lazima utupe kule!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…