Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Me mwajiriwa kwenye kampuni mmoja kubwa hapa mjini mshahara wangu ni milioni 4.2 nina miaka 15 mpaka sasa kazini ila sijajenga, wala sina kiwanja, nimepanga chumba cha 1 moja kwa mwezi hela pia benki nina laki 2 tu.... Mshahara nikipata namalizia kwa wanawake, kufanya starehe maeneo mbali mbali, kuvuta sigara na kunywa pombe za bei ghali, gari ninayo 2 ila mafuta yananifilisi...

Nishauri kwa sasa nina umri wa miaka 39. Naomba ushauri. [emoji16] [emoji51]
Inabidi uende sober house
 
'Acha kazi uone kazi kupata kazi'.
neno langu naomba liheshimiwe jamani wandugu plzzzzz
ila karibuni sana mtaani tunawapenda na tutawaonesha ushirikiano

usiishi kwa facts ambazo hazina kichwa wala miguu, uoga wako ndo umaskini wako!
 
Mkuu umewai kufanya biashara? au kuacha kazi na kuwa mtaani?

Ukweli ni kwamba kuacha kazi na kwenda mtaani 90% ni jinsi utakavyo control hisia zako na zawatu around (emotional). 10% ndio failure or success.

Mimi niliacha kazi yenye kipato cha juu sana. Niliamua tuu kwamba ikifika september naacha, nikaandika resignation letter nikawapa one week, sikutaka discussion. Nikaacha, nyumba ilukuwa bado kuisha na familia nzima wakasema huyu anaitaji mganga amtibu. Nilichokuwa nacho ni courage, ukiwa na courage (utashi) hata dunia nzima iende mashariki wewe peke yako uende magharib hautajutia.

La muhimu ni ujipange, andika chini kwamba unataka kufanya nini na mauzo ya kiasi gani kwa mwezi yatakufanya upate utulivu, yaweke yale mauzo kwa siku kisha anza mapambano.

You can do it.
Point
 
Binafsi nafikiria kuacha kazi ya ualimu miaka minne ijayo,kipindi ambacho shamba langu la kisarawe heka nane na nusu litakuwa tayari limeanza kutoa nazi za kutosha, kwa sasa tayari nna nyumba moja ya vyumba 11 ipo msongola, na nafanya biashara ndogondogo za food products ambazo zinaenda vizuri.
 
Binafsi nimeweka mkakati kuwa biashara yangu ikifikisha total income ninayopata kazini kwa mwaka nitakuwa tayari kuacha kazi. Kwa sasa nimeweka maximum time span ya kuendelea kuwepo kwenye ajira ni mwisho 2023. Hapo katikati naweza kuacha kazi siku yoyote ili mradi nimefikia lengo la Total Net Income from Employment =Total Business Cash Inflow with condition that net profit from the business should be greater or equal to Gross salary

Mbinu ninayotumia ni kuwa nishaweka malengo makubwa, kisha nimeyavunja yale malengo makubwa katika malengo madogo madogo ya kila mwaka. Kwa hiyo kila mwaka nimekuwa nikijifanyia tathmini kuangalia nimefikia wapi. Namshukuru Mwenyezi MUNGU ananifanyia wepesi na malengo yatafikiwa kwa neema yake
Hongera sana.
Kwangu ni hivohivo pia. Nilijiwekea lengo ifikapo 2020 niwe nishaacha. Namshukuru Mungu kunitia ujasiri kuacha rasmi mwezi uliopita. Tangu tarehe 1 April 2018 nimeingia mtaani mazima. Japo hakuna anayenielewa... Wanadhani nimechanganyikiwa.
 
Hongera sana.
Kwangu ni hivohivo pia. Nilijiwekea lengo ifikapo 2020 niwe nishaacha. Namshukuru Mungu kunitia ujasiri kuacha rasmi mwezi uliopita. Tangu tarehe 1 April 2018 nimeingia mtaani mazima. Japo hakuna anayenielewa... Wanadhani nimechanganyikiwa.
Hongera mkuu. Najua changamoto ya kwanza ni ndani ya nyumba yako mwenyewe na ndugu wa karibu lazima watakupinga. Uwe na msimamo na ujasiri. Kumbuka kuwa haitakuwa rahisi na wala hutapita kwa haraka but eventually you will get through all the difficulties of this transition phase.

Mwisho watakuelewa tu. Mimi bado naendelea kupambana na malengo na muda. Naamin kwa jina la mwenyezi MUNGU ndoto yangu itatimia sawa sawa na mapenzi yake.
 
Nilifanya kazi miaka 10 mafanikio hakuna nilistuka nakuuamua kuacha maana mafanikio yangu yalikua hakuna zaidi ya kula na kuwa smart kimavazi na kulipa kodi za nyumba tuu,
Namshukuru Mungu kwa yale maamuzi
 
Wengi wanafanyia kazi ile tunaita addiction..yaani mazoea,lakini amini nakuambia ajira nyingi utalipwa ili uendelee kuwa tegemezi! Tukija Kwenye kujiajiri wengi ni waoga na kushikiwa akili..siku zote sipendi kumshirikisha dili zangu mtu muoga coz najua atazingua tu..
Masikini wengi wanamiliki liabilities badala ya assets kwa maana ya vitu vinavyowamalizia pesa badala ya kuwa na vitu vinavyoingiza pesa....trust me maisha ni kuamua..you should be a risk taker in order to be Rich!
 
Wanajukwaa wenzangu habari, mada hii imenigusa sana ninakama mwaka mmoja sasa mtaani toka niache kazi nikiwa nimefail katika kujiajiri kwa mara hii ya kwanza wakati nipo kwenye ajira kupitia mkopo niliweza kununua bodaboda 2 ambazo ziliniingiza pesa ilinipa jeuri ya kuacha kazi nikiwa na wazo kwamba niache kazi niende kujiajiri kwa kufungua biashara hata ya kibanda lakini nilifungua saluni ya kiume licha ya kwamba biashara mpya eturn yake kwa mwanzoni ni ndogo lakini changamoto ikawa kinyozi sikudumu naye alifanya kazi kwa mwezi moja tu nikamtafuta wa pili naye alikaa mwezi wiki tu sikuwana option nikafunga na kurudisha chumba cha mtu vinginevyo kodi inanihusu, nimejifunza na naendelea kujifunza kuwa katika kutaka kujiajiri sio tu mtaji ni tatizo lakini pia usimamizi wa biashara zenyewe ni ngumu.
Kama hukubahatika kupata watu sahihi lazima uone usimamizi ni ngumu lakini kuna ngumu zaidi ya usimamizi fikiri sana!
 
Hongera sana.
Kwangu ni hivohivo pia. Nilijiwekea lengo ifikapo 2020 niwe nishaacha. Namshukuru Mungu kunitia ujasiri kuacha rasmi mwezi uliopita. Tangu tarehe 1 April 2018 nimeingia mtaani mazima. Japo hakuna anayenielewa... Wanadhani nimechanganyikiwa.
Tupe experience mkuu. Vip kuhusu ule mkopo wa benki
 
kwa usawa wa maisha unaweza. Ukitoka kazini saa tisa, unaingia shambani, unalima, unakagua mifugo n.k
Unaweza kufanya hivyo kwa mradi au biashara ndogo lakini kadri mradi au biashara yako itakavyopanuka na kukua ndivyo utahitaji muda mwingi wa kumanage mambo mbalimbali ya hiyo biashara yako. Kama umeajiriwa na biashara yako ikahitaji muda zaidi wa kui operate lazima tu utaanza kukwazana na mabosi wako. Labda kama malengo ya biashara yako ni kukuwezesha kupata hela ya kununua kiberiti na chumvi, lakini kama una malengo ya kuwa na biashara au mradi mkubwa kuajiriwa lazima utupe kule!
 
Back
Top Bottom