Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Mkuu hili group halipo mbona?
 
Ndugu, this is the good thread umeleta, nakupongeza kwa hilo, Nimekuwa nikifanya pia kama freelancer hasa kwenye translations na transriptions from English to Swahili and the vice versa, ukiwa na fursa pia usisite kuni PM tuone ni jinsi gani tunaeza ifanya.
 
Yes ukijiunga unapewa mwez mmoja free na baada ya hapo utakuwa unalipa monthly fee kila mwezi kutegemea na aina ya akaunti uliyo nayo mfano mm nalipa dollar kumi kila mwez
Mkuu nmeshajiregister fiverr.. But bado cjajuaaa naanzaje kupata kaz mkuu... Msaada tafadhalli
 
Nilichukua likizo yangu ya Mwezi nikiwa nimejiandaa kuanzisha biashara, na kweli nikafungua gori vizuri kabisa nilishiriki kwa asilimia 100 kuendesha biashara,kisha nikamuagiza kijana kutoka mkoani ili ajifunze kipindi nikiwepo na lengo langu ikisimama niache kazi.

Ilikaa poa mpaka raha kabisa, niliajiri kijana wa pili,wa kwanza nilimpangia chumba,nikamuwekea godoro analaa fresh na maisha yake yanaendelea vizuri

Aisee vijana wakaanza kushindwa kusimamia vizuri,wanafanya mambo yao, ghafla nilisikia kijana anasema anataka kwenda kijijini akawa mbogo nikampa nauri akaondoka na kwa kuwa tayari nilisharudi kazini nikaifunga biashara mtaji nikanunua kiwanja nikajenga kajumba, nikarudi utumwani.

Kwa changamoto nilizoziona sasa hivi narudi kwa gia kubwa zaidi .
 
Mwanangu usiache komaa, ila cha msingi anzisha biashara yoyote unayoona inalipa
 
Binadamu tunatofautiana,watu wote hawawezi kuwa ma-risk takers,ndio maana kuna masikini na matajiri,watumwa na mabwanyenye.Kuajiriwa kuna mwisho,na mara nyingi mwisho wake huwa sio mzuri.Kuna biashara nyingi sana za kufanya zinazohitaji mitaji midogo mfano;tafuta wamama wajane kama watano hivi,wafungulie genge kila mmoja;na kwa kila mmoja wekeza laki 2.Baada ya hapo anza kukusanya mapato.
 
Mkuu tunashinndwa kujiunga na group link yako inasema group halipo msaada tafadhali
 
Hizi kazi nzuri sana japo zinahitaji kujituma sana Uaminifu sana, nimefanya kazi Elence na Odesk kipindi hicho now inaitwa upwork, ukijituma vema na ukapangilia vitu vizuri kwa mwezi waweza pata $ 1000 + , vijana mliopo chuo na wale wasio na kazi changamkieni fursa hizo pesa ipo
 
Mkuu nimekuelewa vip wewe ulifanyaje mpaka ukawa unapata hizo kazi maana nimeona ukiwa new member ni changamoto kupata
 
Mi naomba unipe hints ya nini cha kufanya mpaka kuwa na account ili niwe na access za hizo kazi? MixedFrank TAVEATT
Mkuu ni rahisi, Just go to www.upwork.com then register kama mtu Job secker the tengeneza profile yako vema, baadae wataaprove profile yako pamoja na detail zako then unaanza kuomba kazi kulingana na upeo wako, mimi ilinichukua wiki moja baada ya kuomba kazi kama 10 hivi kupata kazi ya kwanza baada ya hapo ikawa rahisi kupata kazi
 
Mkuu tunaomba msaada wako kwenye profile unaweka vitu gani vya muhimu kwa mfano mtu wa taaluma ya takwimu
 
Mkuu nimekuelewa vip wewe ulifanyaje mpaka ukawa unapata hizo kazi maana nimeona ukiwa new member ni changamoto kupata
Siri kubwa kwa upande wangu kipindi naanza nilikuwa naomba kazi ambazo zimepostiwa na wazungu hasa UK na USA ambazo zinatakiwa kufanyika hapa Tanzania wakati wao hawapo huku bongo, competitor wangu wengi walikuwa wakenya na wachache sana watanzania, (TZ Tupogi nyuma vitu vingi), hivyo tu mkuu. Pia unapomba kazi uoneshe kuwa unaweza bila shaka na usidanganye
 

Ningependa unipe maujuzi kidogo kuhusu money wire, fevvr payoneer, nataka kuzitumia, na je ni rahisi kwa hapa tanzania kupata malipo yako.?
 
Mkuu tunaomba msaada wako kwenye profile unaweka vitu gani vya muhimu kwa mfano mtu wa taaluma ya takwimu
Mkuu Just tengeneza uoneshe ujuzi wako, na elimu yako, sample ya kazi zako ulizowai kufanya, videos, reports etc, zaidi check PM yako nimekutumia sample
 
Mkuu Just tengeneza uoneshe ujuzi wako, na elimu yako, sample ya kazi zako ulizowai kufanya, videos, reports etc, zaidi check PM yako nimekutumia sample
Naomba nami ntumie mkuu pm kama hutojali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…