Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Pole sana ndugu. Kikubwa biashara usimamie mwenyewe
Nilichukua likizo yangu ya Mwezi nikiwa nimejiandaa kuanzisha biashara, na kweli nikafungua gori vizuri kabisa nilishiriki kwa asilimia 100 kuendesha biashara,kisha nikamuagiza kijana kutoka mkoani ili ajifunze kipindi nikiwepo na lengo langu ikisimama niache kazi.

Ilikaa poa mpaka raha kabisa, niliajiri kijana wa pili,wa kwanza nilimpangia chumba,nikamuwekea godoro analaa fresh na maisha yake yanaendelea vizuri

Aisee vijana wakaanza kushindwa kusimamia vizuri,wanafanya mambo yao, ghafla nilisikia kijana anasema anataka kwenda kijijini akawa mbogo nikampa nauri akaondoka na kwa kuwa tayari nilisharudi kazini nikaifunga biashara mtaji nikanunua kiwanja nikajenga kajumba, nikarudi utumwani.

Kwa changamoto nilizoziona sasa hivi narudi kwa gia kubwa zaidi .
 
Binadamu tunatofautiana,watu wote hawawezi kuwa ma-risk takers,ndio maana kuna masikini na matajiri,watumwa na mabwanyenye.Kuajiriwa kuna mwisho,na mara nyingi mwisho wake huwa sio mzuri.Kuna biashara nyingi sana za kufanya zinazohitaji mitaji midogo mfano;tafuta wamama wajane kama watano hivi,wafungulie genge kila mmoja;na kwa kila mmoja wekeza laki 2.Baada ya hapo anza kukusanya mapato.
Amakweli kufa kufaana....
Sikujua kuwa wajane ni fursa..
Anyway tatizo lolote linalomsibu mwanadamu huwa ni fursa kwa mtu mwingine mwenye upeo wa mbali.

Naunga mkono hoja kuajiriwa ni utumwa hapa nilipo nakamilisha mabo flani niachane na ajira za zama hizi.
 
Amakweli kufa kufaana....
Sikujua kuwa wajane ni fursa..
Anyway tatizo lolote linalomsibu mwanadamu huwa ni fursa kwa mtu mwingine mwenye upeo wa mbali.

Naunga mkono hoja kuajiriwa ni utumwa hapa nilipo nakamilisha mabo flani niachane na ajira za zama hizi.
ndio hivyo mkuu,maisha ndio yako hivyo : ukiwa na kesi ni fursa kwa wakili,ukipata magonjwa ni fursa kwa daktari,gari ikipata ajali ni fursa kwa makenika,ukifariki ni fursa kwa warithi na mchonga majeneza,n.k
 
kesho navuna
IMG_20181006_103250.jpeg
IMG_20181006_103242.jpeg
IMG_20181006_103246.jpeg
 
Mie natafta mchawi ambaye huwa anaingia nyumba za watu kuwachezea mara awashushe vitandani akawalaze bafuni, huyu nataka anipeleke benki nikabebe viroba vya noti
 
Wachangiaji wameongea mambo mengi muhimu. Mimi ninaona kuacha kazi na kufanya shughuli binafsi ujasiriamali au biashara ni njia ya kupiga hatua. Ila kuacha kazi iwe process yaani mchakato sio event yaani tukio la ghafla kama umeajiriwa.

Unatakiwa kuanzia siku ya kwanza ya kuajiriwa uazimie kujiajiri hivyo panga nini utafanya ili kujiajiri. Wakati wa ajira ufuatilia na kujifunza maarifa muhimu,kupata taarifa na rasilimali za kuanzisha biashara au ujasiriamali.

Ukipata maarifa,taarifa na rasilimali anza biashara. Unapoanza biashara unaweza kuacha kazi hapo hapo au baadae inategemea na Cost benefit Analys yako, yaani tafakari situation 1 nini unapoteza ukiacha biashara isimamiwe na mtu mwengine na nini unapata kwenye ajira. Situation 2 Nini utapata zaidi ukisimamia biashara mwenyewe na nini utapoteza ukiacha kazi.

Ila ieleweke katika biashara na ujasiriamali innovative ideas and supervision ni muhimu kwa mafanikio ya biashara, ingawa innovation ni kipaji lakini kupitia ICT platforms kama youtube unaweza kujifunza how to be innovative in business.
 
Kwa wale walioajiriwa,changamoto kubwa waliyonayo ni usimamizi, na hili ndilo linawarudisha nyuma.Na wengi kwa walioajiriwa wanaweza kuwa wanafikiria kuanzisha biashara ambazo haziitaji usimamizi mkubwa,mfano nyumba za upangaji n.k.kutokana na hali hiyo mtu anajikuta anaajiriwa mpaka mwisho wa uhai wake.
 
Back
Top Bottom