Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Pole sana ndugu. Kikubwa biashara usimamie mwenyewe
 
Acha kabisa kwanza ukisha acha cha kufanya utakijua tu
 
Amakweli kufa kufaana....
Sikujua kuwa wajane ni fursa..
Anyway tatizo lolote linalomsibu mwanadamu huwa ni fursa kwa mtu mwingine mwenye upeo wa mbali.

Naunga mkono hoja kuajiriwa ni utumwa hapa nilipo nakamilisha mabo flani niachane na ajira za zama hizi.
 
ndio hivyo mkuu,maisha ndio yako hivyo : ukiwa na kesi ni fursa kwa wakili,ukipata magonjwa ni fursa kwa daktari,gari ikipata ajali ni fursa kwa makenika,ukifariki ni fursa kwa warithi na mchonga majeneza,n.k
 
Mie natafta mchawi ambaye huwa anaingia nyumba za watu kuwachezea mara awashushe vitandani akawalaze bafuni, huyu nataka anipeleke benki nikabebe viroba vya noti
 
Wachangiaji wameongea mambo mengi muhimu. Mimi ninaona kuacha kazi na kufanya shughuli binafsi ujasiriamali au biashara ni njia ya kupiga hatua. Ila kuacha kazi iwe process yaani mchakato sio event yaani tukio la ghafla kama umeajiriwa.

Unatakiwa kuanzia siku ya kwanza ya kuajiriwa uazimie kujiajiri hivyo panga nini utafanya ili kujiajiri. Wakati wa ajira ufuatilia na kujifunza maarifa muhimu,kupata taarifa na rasilimali za kuanzisha biashara au ujasiriamali.

Ukipata maarifa,taarifa na rasilimali anza biashara. Unapoanza biashara unaweza kuacha kazi hapo hapo au baadae inategemea na Cost benefit Analys yako, yaani tafakari situation 1 nini unapoteza ukiacha biashara isimamiwe na mtu mwengine na nini unapata kwenye ajira. Situation 2 Nini utapata zaidi ukisimamia biashara mwenyewe na nini utapoteza ukiacha kazi.

Ila ieleweke katika biashara na ujasiriamali innovative ideas and supervision ni muhimu kwa mafanikio ya biashara, ingawa innovation ni kipaji lakini kupitia ICT platforms kama youtube unaweza kujifunza how to be innovative in business.
 
Kwa wale walioajiriwa,changamoto kubwa waliyonayo ni usimamizi, na hili ndilo linawarudisha nyuma.Na wengi kwa walioajiriwa wanaweza kuwa wanafikiria kuanzisha biashara ambazo haziitaji usimamizi mkubwa,mfano nyumba za upangaji n.k.kutokana na hali hiyo mtu anajikuta anaajiriwa mpaka mwisho wa uhai wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…