Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

UpWork na Fiverr ni vitu viwili tofauti.

Business model wanazotumia ni tofauti.

Ukijisajili na Fiverr basi wewe ndiyo una-post offer kwa potential client. Na kila huduma unayotoa inaitwa Gig.

Gig inathamani ya $5. Yaani upo tayari kumfanyia mtu kazi yake kwa $5.

Lakini haiishii hapo. Fiverr allows you to offer extra services.

Kwamfano client anayenunua huduma yako ya kumtengenezea logo kwa $5 basi anaweza pia akawa anahitaji huduma ya kutengenezewa blog.

Kwahiyo ukiwa umeandaa gig yako utaona sehemu ya chini ya kuelezea extra service unatoa zaidi ya hiyo ya huduma ya logo design.

Vilevile kwa translators. Unasema "I will translate English to Swahili for $5 (300 word count)

Chini yake unaweza andika "for words more than 300 to 1000 I charge $20)

UpWork ni kama freelance platform nyingine yoyote.

Client ndiye anayetoa offer.

Kwa mfano, "I need someone to translate legal document from English to Swahili"

Chini yake anaweka budget aliyonayo. Labda $10. Inategemea na ukubwa wa kazi.

Mimi ni freelancer wa muda mrefu. Nimefanya kazi nyingi. Kuanzia data entry, translation, proofreading, short story writing, nimekuwa tutor wa lugha ya Kiswahili.

Sasa hivi naelekeza nguvu zangu kwenye online marketing, email marketing, Social engine Optimization, FacebookAd, AdWord.

Lakini pia nipo kwenye hatua za mwisho kutengeza the first Swahili platform. Hapa watu wataweza kuuza ujuzi wao kuanzia Tsh 3,000 hadi Tsh 50,000.

Nimeona hii ni jambo jema kwasababu lugha ya kiingereza ni changamoto kwa vijana wengi.

Wengi hawawezi kujieleza kwenye majukwaa niliyoyataja. Na kama unavyojua kule ni English. Na kupata kazi inabidi uwe fluent in English na pia uwe competent sana.

Je, vijana wangapi hapa JF ni fluent kwenye Kiingereza?

Wengi hata conversation level ni shida. Wataweza kumshawishi potential client kutafsiri article yake kwenda Kiswahili hata kama wanazungumza Kiswahili fasaha? Unaona hapo ndiyo ugumu unaanzia.

Mimi nimeona nisaidie vijana wenzangu kuanzisha platform ya namna hii kwa lugha ya Kiswahili. Na inalenga watu wa Tanzania na nchi jirani zinazotumia Kiswahili.

Lugha ya mawasiliano itakuwa Kiswahili ili kuwapa wanachama wengi nafasi ya kujipatia kipato.

Nahitaji maoni au swali. .

Unaweza uliza hapa hapa au email wiserastarising@gmail.com
 
Mkuu hongera sana endelea hivyo hivyo Mungu atakulipa.
 
Mkuu hongera sana endelea hivyo hivyo Mungu atakulipa.
Shukrani mkuu.

Siku chache kuanzia leo nita-post uzi kuelezea hili wazo nipo nalo ili watu waone namna gani wanaweza tumia platform yangu kujiingizia kipato.

Mimi ni mjasiriamali kwahiyo jambo la kwanza kabisa nikijua potential clients wanataka nini.

Nitaleta hapa JF.
 
Mnasahau kuna wenye gundu /nuksi ambao hata ufanyaje biashara haikubali wanakufa utumwani,hawa mnawashauri nini?...nimejionea mwenyewe miaka 25
 

Hapo utasikia jiunge na Forever Living....What the https://jamii.app/JFUserGuide people!?
 
Ajira ikitumiwa vzr kama daraja la kupata mtaji au uzoefu, ni vzr.

Kuna watu wana mawazo mazuri ya biashara lkn wanashindwa kuanzisha biashara kwa kukosa fedha kiasi kdg tu. Watu wa kundi hili wakipata ajira inasaidia, maana wanaeza pata mitaji kirahisi, tena bila riba.

Tatizo ni pale mwajiriwa anapochukulia ajira kama suala la kudumu na akajisahau
 
Ajiriwa kwa lengo la kutafta mtaji lakini kujiajiri ni vema zaidi,
NB:kuna baadhi ya ajira zina maslahi mazuri Kuliko kujiajiri


Hakuna ajira yyt dunian yenye maslahi mazur kuliko kujiajiri ukiona hvyo basi uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo[emoji777]
 
Hakuna ajira yyt dunian yenye maslahi mazur kuliko kujiajiri ukiona hvyo basi uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo[emoji777]
Ivi unajua Mchechu wa national housing alikuwa analipwa shilingi ngapi? Ndo uje umfananishe na mamantilie alie jiajiri
 
Ivi unajua Mchechu wa national housing alikuwa analipwa shilingi ngapi? Ndo uje umfananishe na mamantilie alie jiajiri
Hahahaha jamaa anafanya masihara, upate kazi ya kukulipa 25m kwa mwezi uache kweli? Watu wanaokula take home ya 1m tu kwa mwezi hawataki kusikia story za kujiajiri wewe unasema nini! Ukweli usemwe tu wabongo kujiajiri is not our thing kabisa ila ndio tunafanya ile kusaka tonge tu maana ajira hamna!
 
Upo sahihi mkuu wabongo hatujalelewa katika misingi ya kujiajiri hvo inakuwaga ni option baada ya kukosa plan A
 
Ujasiliamari unahitaji muda (time) na dhamira (dertimination) But wengi wanachanganya mjariliamari na watu waliojiajili.
 
Kichwa cha habari na maelezo vinakinzana, umeishia kunichanganya tu hapa!

Na umenipa gharama za bure tu hapa inabidi nikaonane na mtaalamu wa afya!
 
Kikubwa tusikariri maisha na kufata mkumbo muhimu ni kufanya kile unachopenda na kukiamini
 
utajiri ni kuwa na nyumba mbili na gari na kula kuku upendapo
 
You need to hustle to make $$$

Jitahidi uwe na vyanzo vingi vya income kadiri iwezekanavyo.

Acha kabisa pesa tamu bana. When you have money it means you can have more choices in life. Rich people don't worry about money when they in vacation. They eat what they want, fly business class, they send children to better schools. Aisee nani hapendi kuwa mwenye mafanikio?

Ok, wakati naandika hayo this idea comes to mind. Maybe you are interested.

Hebu angalia hii freelancer platform. Unaweza jisajili nakupost project yako if you want people to buy and make money.

KaziYako Tanzania | Freelancers Online

Not time to waste lazima u-hustle if you want to make $$$$
 
You will never be a rich working in some else. If you want be a rich you must in business of your self
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…