Mwelewa
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 2,343
- 3,284
UpWork na Fiverr ni vitu viwili tofauti.Kwanini nyinyi wacahche mlioanza kujisajili msikutane mkaeleweshana physically naona hii bora zaidi. Kuna skill nyingi sana za kupeana ktk kusaidiana. Au mambo ya usiri yatawasumbua? Ukiamua kufanya jambo ulufanye kwa nguvu zako zote.
Hii inaonekana ni real deal unafanya kazi unapata malipo nimeipenda sana hii.
Business model wanazotumia ni tofauti.
Ukijisajili na Fiverr basi wewe ndiyo una-post offer kwa potential client. Na kila huduma unayotoa inaitwa Gig.
Gig inathamani ya $5. Yaani upo tayari kumfanyia mtu kazi yake kwa $5.
Lakini haiishii hapo. Fiverr allows you to offer extra services.
Kwamfano client anayenunua huduma yako ya kumtengenezea logo kwa $5 basi anaweza pia akawa anahitaji huduma ya kutengenezewa blog.
Kwahiyo ukiwa umeandaa gig yako utaona sehemu ya chini ya kuelezea extra service unatoa zaidi ya hiyo ya huduma ya logo design.
Vilevile kwa translators. Unasema "I will translate English to Swahili for $5 (300 word count)
Chini yake unaweza andika "for words more than 300 to 1000 I charge $20)
UpWork ni kama freelance platform nyingine yoyote.
Client ndiye anayetoa offer.
Kwa mfano, "I need someone to translate legal document from English to Swahili"
Chini yake anaweka budget aliyonayo. Labda $10. Inategemea na ukubwa wa kazi.
Mimi ni freelancer wa muda mrefu. Nimefanya kazi nyingi. Kuanzia data entry, translation, proofreading, short story writing, nimekuwa tutor wa lugha ya Kiswahili.
Sasa hivi naelekeza nguvu zangu kwenye online marketing, email marketing, Social engine Optimization, FacebookAd, AdWord.
Lakini pia nipo kwenye hatua za mwisho kutengeza the first Swahili platform. Hapa watu wataweza kuuza ujuzi wao kuanzia Tsh 3,000 hadi Tsh 50,000.
Nimeona hii ni jambo jema kwasababu lugha ya kiingereza ni changamoto kwa vijana wengi.
Wengi hawawezi kujieleza kwenye majukwaa niliyoyataja. Na kama unavyojua kule ni English. Na kupata kazi inabidi uwe fluent in English na pia uwe competent sana.
Je, vijana wangapi hapa JF ni fluent kwenye Kiingereza?
Wengi hata conversation level ni shida. Wataweza kumshawishi potential client kutafsiri article yake kwenda Kiswahili hata kama wanazungumza Kiswahili fasaha? Unaona hapo ndiyo ugumu unaanzia.
Mimi nimeona nisaidie vijana wenzangu kuanzisha platform ya namna hii kwa lugha ya Kiswahili. Na inalenga watu wa Tanzania na nchi jirani zinazotumia Kiswahili.
Lugha ya mawasiliano itakuwa Kiswahili ili kuwapa wanachama wengi nafasi ya kujipatia kipato.
Nahitaji maoni au swali. .
Unaweza uliza hapa hapa au email wiserastarising@gmail.com