Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Kwa kweli nimesoma comment nyingi wewe umeeleza njia hongera kweli umejiandaa kuacha kazi.
Kuna mwalimu mmoja alikuwa na maono hayo huku morogoro ingawa hakuacha kazi lakini mradi wa miti unamlipa sana.
 
Kujiajiri kunawezekana kabisa. Tofauti ya kuajiriwa na kujiajiri ni kwamba kuajiriwa unalipwa mshahara na wote ni malipo ya faida.. Kujiajiri, faida kuipata ni changamoto. Je.. unafikiri utakuwa na kitu ambacho watu watakitaka na kitakupa faida kubwa? Bado kuna kodi, Brela nk? Kama unalipwa shs millioni 1, ni biashara gani itakupa hiyo faida chap chap?

Nashauri MSIACHE KAZI KWANZA. JARIBUNI KITU KWANZA. Unaweza kabisa kufanya biashara huku ukiwa umeajiriwa. Faida ikiongezeka.. ndio mtu unaacha kazi.
 
Mkuu kuacha kazi ni hatua ya kawaida

Shida sio million moja au mbili

Kujiari kunaweza kukuingizia hata laki saba na usiwe na deni na mtu

Ila kazini unaweza kuwa na madeni kama vile we ndio mrija wa kutolea hela

Kuna biashara zinalipa kutokana na ubunifu wako tu
 
Kama kazi yako itahitaji eneo la kudumu tafuta eneo lako husiache kazi ukafanyie biashara kwa watu, wakiona unapata kodi lazima ipande au utanyanganyw
 
Nakubaliana ww mkuu sana na njia uliyochukua ilikuwa ni sahihi asili mia 100. Ukisha ona mwenza wako anakutalia kitu kwa personal ishu zake mfano kuacha kazi kwakuwa atakosa huduma huyo sio mtu sahihi kwa maana huyo ni parasite. Ina maana kwamba yeye yuko kimasilai au yeye ni abiria tu kwenye safari yako badala ya yeye kuwa dereva msaidizi, konda au hata tanboy. Haya ndo makosa ya wadada zetu siku hizi na sis kama madereva nikuwashusa na kuendelea na safari. Huwa nashangaa sana alafu ukifanikiwa ndipo anaanza kujisogeza hawa ndo watu ninao wapiga vita kwa maana hata baba wa familia napo tangulia mbele za haki na akabaki mwanamke wa namna hiyo asilimia kubwa huwa familia zao huteseka kwa maana hakuwa na vision wala msukumo na hata elimu pengine. So ni muhimu kuwa na mwenza alienda hata kidato cha 4.

Msishangae kwanini mwanamke yupo kwenye hii mada na kwanini ninamuweka. Ni kwasababu mwanamke anamchango wake na mara nyingi anakuwepo pembeni pale kunako mafanikio ila pia yeye ni part of the equation kwa maana asipoenda kwa mahesabu, asipo kuwa na busara, asipo kuwa malkia wa ngome yake, asipo kuwa mke na asipo kuwa na vision ya kukuza familia yake economic wise na mwanamme wake then huyo ni kumtoa kwenye equation haraka sana maana 1 + 0=1 sio 2
 
Kuwa na mke alienda shule sio kigezo cha kufanikiwa

Na kuwa na mwanamke wa elimu ya kawaida napo pia sio kufanikiwa

Inatakiwa upate mwanamke anae kuwa na akili ya ziada

Ukiona mizinguo panga ramani zako mwenyewe songa mbele
 
Sasa hio laki saba utaipata mara tu ukifungua biashara mkuu? Ukiacha kazi hakikisha una hela ya kukizi mahitaji yako kwa mwaka mzima na mtaji juu yake. Manake uwe na mraji na pia uwe na hela kando ya mahitaji binafsi. Kama una familia, pia hivyo hivyo. Faida kupatikana hata ya laki 7 inachukua muda mkuu.
 
Mkuu unajua ukitaka kujiajiri tatizo sio hela

Hebu fikiria umefukuzwa kazi utaishije?

Kuna wakati tunga mtihani wenye majibu magumu ili uumize kichwa

Ukiogopa kwa kuwa huna hela za kulea familia na kuanzisha biashara unajikuta umekuwa mpenzi msikilizaji wa mafanikio ya wengne
 
Hongera mkuu, moyo wako umejaa ufahamu.
 
Duuh ujumbe mzuri sana huu, ubarikiwe mkuu
 
M
Pamoja mkuu

Karibu kujiari
Mkuu USIDANGANYIKE.. Bila ya mtaji, hauna biashara. Narudia.. USIDANGANYIKE. Hata kama hauna hela yako binafsi, lazima uipate benki, kwa ndugu n.k. Fikiria hili.. unaanzisha biashara na tayari una wapinzani ambao wana biashara kama yako inaendelea.. kuna njia gani ya kuboresha huduma au bidhaa pasipo kuwa na mtaji? Ukifikiria utaweza bila hela..UTASHINDWA. Utakuwa na biashara yenye value ndogo, na wateja wapya kuwapata lazima uwe na biashara yenye value ambayo inaweza kushindana na zile za washindani. Na value ya biashara inaenda sambamba na mtaji ulio nao. Unafikiri utauza maneno matamu bila matendo na bidhaa na huduma bora?

MIMI NINA UJUZI SANA NA BIASHARA MKUU. Naona weee unaongelea kupitia vile vitabu vyenu vya ujasirismali mnavisomaga. Na vinawadanganya tu. Poleni sana.
 
Ukifukuzwa kazi.. sio kwamba utalisha familia maneno au hewa. Utatafuta hela kwa hali na mali ya kulisha familia. Na itakuwa ni mbinde kubwa.

Sasa NI KWA NINI USIJIANDAE KABISA BADALA YA KUSUBIRI HIYO MBINDE IJE? Ni kwa nini usiweke mambo sawa kimtaji ili kupunguza hayo matatizo? Kuacha tu kazi wakati hauna mtaji hata asilimia fulani ni KUKOSA MIPANGO. Na pasipo mipango mizuri, BIASHARA HAIFANIKIWI Mkuu.
 
Kama kazi yako itahitaji eneo la kudumu tafuta eneo lako husiache kazi ukafanyie biashara kwa watu, wakiona unapata kodi lazima ipande au utanyanganyw
Kabisa. Personally kujenga majengo ya biashara kulisaidia sana. Ni baada ya kunyanyaswa na mtu mara ya kwanza. In business inaitwa vertical integration. Personally nafanya tours, nimejenga lodge na ofisi binafsi. Magari nilianza kukodi, nikanyanyaswa pia. Sasa nina magari machache binafsi na nazidi kuongeza. Lengo ni kutokodi kabisa na kutumia vertical integration katika transport na lodging pia katika key areas
 
Kuwa na mke alienda shule sio kigezo cha kufanikiwa

Na kuwa na mwanamke wa elimu ya kawaida napo pia sio kufanikiwa

Inatakiwa upate mwanamke anae kuwa na akili ya ziada

Ukiona mizinguo panga ramani zako mwenyewe songa mbele
Wanawake asilimia kubwa hasa warembo tunaowapenda ni mizinguo leo. Mimi naona katika ujasiriamali kama mtu haujaoa, basi kaa hivyo hivyi kwanza. Pambana ufanikiwe ndio uoe. Na hata hapo, itakuwa ni kazi pia. Kwa ujumla NI MUHIMU KUPATA MSICHANA MWENYE MALENGO KAMA YAKO, MWENYE AKILI KAMA ZAKO, NA MOYO WA KUPAMBANA KAMA WAKO. Lakini kwa leo ni vigumu kumpata.

Wasichana wana gharama zao na sio za hela tu, hata za kukuchanganya akili ukashindwa kufocus katika kazi zako. Ila UKIPATA MZURI, sawa kabisa. Japo kwa leo ni kazi. Na wengine hata wanaua waume zao kama Msuya bilionea alivyofanyiwa. Kazi iko
 
Fake.hauna uthubutu.
 
Kwa kweli nimesoma comment nyingi wewe umeeleza njia hongera kweli umejiandaa kuacha kazi.
Kuna mwalimu mmoja alikuwa na maono hayo huku morogoro ingawa hakuacha kazi lakini mradi wa miti unamlipa sana.
Safi karibu mapambanoni .Tusiogope all because life needs us to experience alot.

Aluta continua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…