Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

KILICHOTOKEA MPAKA KUFIKIA HAPO
1. Hoja ya kwanza "Sina mtaji"
Hoja hii imetokana na mambo yafuatayo;

a. Elimu aliyofundishwa huyo mtu tangu mdogo, aliyoyaona wazazi wake wanafanya, walimu waliomfundisha kwa zaidi ya miongo kadhaa ni kuwa "tegemezi". Kajifunza kuwa yeye hawezi kuwa na wazo na akalisimamia mwenyewe mpaka awepo mtu wa kumsukuma 'Mwajiri'.

b. Ana amini kuwa uwezo wa nje 'pesa' ndo una tafsiri utu wa mtu. Si kweli; ukitaka kuamini, mfilisi Mo*** au yule mwenzake Bakh*** waanze kwenye zero kabisaa kama wewe unayesema huna kitu; tuje tuwapime baada ya miaka 10, je, mtakuwa sawa? Kama una uhakika kuwa mtakuwa sawa basi kweli tatizo ni pesa, lakini uki-reason kuwa hamtaweza kuwa sawa basi ujue sababu ya hivyo ulivyo siyo pesa but something else!
Angalizo kwa wazazi; " Acheni kutufanya wanenu Human things, Tunaomba mtulee kama Mungu alivyotuumba Human beings"
-Mtoto atakuwa na degree au P.h.d lakini ataona hawezi kufanya chochote kwa sababu hana (Things: pesa, gari, somebody n.k)
-Mnafikiri wimbi la wapiga mizinga under 25 linalozungumzwa na kulalamikiwa huko mtaani limetokea wapi kama siyo hao tuliowalea kama Human things? Yeah they have education, and a lot of energy, but They need things!

2. Hoja ya pili; "Kuanza chini, mmmmh! Maana ya kukaaa darasani ilikuwa nini?"
Hoja hii inatokana na yafuatayo;

a. Uoga wa "nitaonekanaje kwa jamii inayonizunguka?" Ndg waalimu huko mashuleni, mtoto alikuwa akifeli, mnamfanya afeel au aone kuwa kufeli ni kitu kibaya sana.
Si kweli kuwa kufeli ni jambo baya, bali ni sehemu ya kujifunza, utajifunzaje kama hakuna makosa? Na shuleni nimekuja kufanya nini mpaka mnanifanya nione kuwa "perfect" ndo kujifunza khaaaa! Kama niko perfect nisingekuja kupanguswa kamasi class kwako. Mtoto wa mwenzio akikosa swali, acha kumkashifu, kumzomea na kumtenga hadi stream! Jamani!

Hiyo mentality ya (nitonekanaje) imetokea hapo, mtu wa hovyo ni yule aliyefeli, au mtu wa chini ni yule ambaye hakwenda shule. Mmewadanganya watoto wa watu na vi- stream vyenu weee, na vimaksi na viripoti vya nani kawa wa kwanza na ni nani kawa wa mwisho, matokeo yake ndo hayoooo! Wanaamini kuwa aliyefaulu ataenda mbele na kupata ajira mapemaaa! Haya sasa yuko mtaani.

NDUGU MHITIMU ZINGATIA HILI LITAKUSAIDIA; ukweli ni kwamba "Huko shuleni wenzako tulikuwa tunanoa shoka vizuri, ili ukifika muda wa kukata miti (mti wa umaskini, mti wa ujinga na mingineyo) shoka lisitusumbue kwa sababu ni butu.

Hayo mashoka unayoyaona mtaani na unahisi " they don't make any progress, look at them, i went to school and now I'm back, what have they done?"
Ni kwa sababu hayako sharp, au pengine hayafahamu wajibu wao. Lakini wewe mwenzetu tayari umenolewa hebu anza kuonesha ufanisi wako, ili na wale wenzako ambao hawakujaaliwa kupata kauwezo kama kako, waone kwa vitendo. "The way you take thing's from zero to hero"

Jamaani! Umefika uwanja wa kazi unauliza 'miti ilokatwa iko wapi?' Wakati sisi tunakusubiri wewe ndo utoneshe wenzio jinsi ya kuiangusha hiyo mipingo?

b. Watoto wengi wanasomea vitu wasivyovipenda, kamwona mjomba mwalimu anafundisha baasi naye anataka kuwa mwalimu, kasikia shangazi kawa engineer basi naye anataka.
Siyo hivyo tu; ndugu, Jamaa, wazazi na marafiki walipiga debe kweli kweli; "Acha ujinga wewe, somea kitu fulani kwani humuoni fulani?"
A problem!
Huwezi kumlazimisha mtu kama huyo a "start small". Hana passion, hana purpose hana dream na hicho alichosomea, anachotaka pesa tu. Unaona madhara ya kulea "HUMAN THINGS?"
congrats I can see some sense of wise in your touches , may god bless independent wise minded people like you
 
Umemaliza mkuu, hongera sana kwa hii analysis.
 
Well said
 
Habari Watanzania wenzangu. Poleni kwa uchovu na mvua za hapa na pale. Nchi hii bwana ni nzuri sana maana hakuna ardhi na nchi nzuri kama Tanzania dunia hii.

Niende katika mada husika.

1. Serikali
Napenda kuikumbusha Serikali kuhusu kutoa ajira za kutosha katika nchi kwani wao ndio namba moja kuchagiza maendeleo kiuchumi. Katika utaalamu wa uchumi panapotokea nguvu dhaifu au ndogo ya manunuzi "weak or low purchasing power" Serikali inatakiwa ibuni aidha mradi mkubwa utakaogusa jamii kwa ujumla wake wananchi washike na kutumia pesa, rejea Bunge la Katiba.

Pia, wanashauriwa watengeneze ajira za kutosha za moja kwa moja katika jamii ili kuchochea vyanzo vingine vya mapato, rejea Ualimu Voda Fasta. Hii mifano niliyoitaja ilitumika kipindi ambacho wananchi uwezo wao wa kufanya manunuzi ulikuwa mdogo au dhaifu kwa wakati huo ukilinganisha na hali ilivyo sasa tunapitia mtikisiko wa uchumi wa kidunia.

Kiashiria kimojawapo cha uchumi kukua sio mfumuko wa bei kwa bidhaa za kilimo hapana pekee haijalishi % kubwa ya wananchi Tanzania ni wakulima bali tunaangalia uwezo wa kila mwananchi katika kufanya manunuzi mfano mwepesi jichunguze wewe mwenyewe.

Hitimisho; Utoaji wa ajira kwa Serikali haukwepeki hata kidogo, tuache ile zana kuwashurutisha watu wajiajiri ikiwa Serikali kutoa ajira ni njia ya kuboresha na kustawisha uchumi wake sio hisani wala sio utamaduni.

2. Wananchi
Napenda pia kuwakumbusha wananchi kuwa wapende kuwekeza katika vitu vya uzalishaji waachane kuwekeza kwenye elimu butu za wototo wao kwa kufuata upepo wa kisiasa. Ifikie hatua wewe mwananchi au mzazi mpeleke mwanao akasomee taaluma itakayomfaa maishani mwake na sio maishani mwake ateseke kwa taaluma aliyoisomea kwa kuwekeza muda na mali pasipokuwepo na matokeo chanya. Hii itakusaidia kuacha lawama kwa taasisi kama shule na serikali kwa ujumla mwishoe mwanao atajikuta anafanya kitu/ kazi/jambo linalomsaidia hapa duniani.

Ufupisho:
Hizi kampeni za kujiajiri zikifanikiwa hapa nchini mfumo wa kijamaa utapotea kabisa hasa vijijini na hakuna hata mwananchi atakuwa na mapenzi mema na mwenzie tutatengeneza taifa la kibepari ambalo litazaa matabaka makubwa sana mwishoe masikini ndie atakayeumia.

Naona kabisa hakutakuwa na uchungu wa mali za umma maana watu mtakuwa mmewafungulia mlango wa unyang'anyi na kujipatia mali ambazo itakuwa ngumu kuhoji uhalali wake.

Nawaomba kila mmoja kwa nafasi yake atimize wajibu wake tuache mazoea na tukubali kubadilika.
 
Hivi kweli naweza kujiajiri mwenyewe?Hili nadhani ni swali ambalo litakuwa linakuja kwako kila utakapokuwa unalalamika kukosa kazi uliyoisomea. Kila mmoja wetu amezaliwa na uwezo huu wa kujiajiri, ingawa wengi wetu huwa siyo rahisi kutambua uwezo huo na kujikuta ni watu wa kukimbilia kazi za wengine.

Ikumbukwe kuwa tumezaliwa na shauku, kiu, kufanya mambo ya hatari, uvumbuzi, akili na vitu vingine vingi ambavyo huonyesha wazi kuwa mtu hawezi kufundishwa ujasiliamali bali uko ndani yake kiasili, kinachohitajika ni yeye tu kujiweka katika mazingira ya kuruhusu akili yake kutatua tatizo lililojitokeza sehemu husika.

Kwa kadiri jinsi mtu anavyoifikirisha akili yake katika kutaka kujiajiri, ndivyo anavyapata majibu na mafanikio zaidi. Kwa nini uteseke kwa kujiajiri wakati uwezo wakujiajiri unao na unaweza kufanikiwa sana. Hapa katika makala hii utajifunza mfululizo wa mambo unayotakiwa kuyazingatia kama kweli una nia ya kujiajiri na kuiamsha hamasa ya ujasiriamali iliyo ndani yako:-

1. Jenga nidhamu
Unapotaka kuwa mjasiriamali,ni lazima utengeneze nidhamu ya kazi,
ili uepuke hatari ya kupoteza kila kitu.Jiulize pia kama una nidhamu ya kutosha kuingia katika hiyo shughuli. Huwezi ukawa mjasiriamali ambaye huheshimu hata muda wako wa kazi. Hii itakuwa ngumu sana kwako kufanikiwa. Kujenga nidhamu ndilo jambo la kwanza la kuzingatia kama unataka kujiajiri.

2. Tambua jamii inahitaji nini
Kama unataka kuwa mjasiriamali ni lazima uwe na uwezo wa kuchemsha akili yako ili uweze kujua mazingira uliyopo yanahitaji kitu gani. Lenga eneo moja ambalo unaona kweli lina uhitaji na unaweza ukaja na utatuzi wake.

Toa huduma ile muhimu ambayo jamii yako inaihitaji na siyo kinyume chake. Kwa kufanya hivyo utakuwa unajitengenezea sifa halisi ambayo mjasiriamali wa kweli anatakiwa kuwa nayo.

3. Tengeneza lengo
Kutengeneza lengo la biashara ni hatua muhimu katika hatua za kuwa mjasiriamali. Lengo hili uliweke katika maandishi na litakusaidia katika kuwashawishi watu kukusaidia mtaji. Mara utakapokuwa umeandika lengo la biashara unayotaka kufanya usiweke maandishi hayo kabatini, anza kuyatafutia njia ya kuwa kitu halisi kutokana na hayo maandishi.Na pia lengo hili litakusaidia wewe usiyumbe na kutoka katika mstari wa lengo ulilojiwekea na litakuwa ni muongozo wako.

4. Jiunge na wajasiriamali
Ikiwa unataka kuwa mjasiliamali ni muhimu kutafuta eneo ambalo wajasiriamali wengi wanakutana kujadiliana.Katika mazingira kama haya utakuwa kama yai linaloatamiwa na kuku ili lije kutoa kifaranga. Wengi wao huwa wamepitia magumu kufika walipofika na hivyo wakiwa wanasimulia habari zao watakufanya ujiamini kuwa na wewe unaweza.

5. Hojiana na wajasiriamali waliokutangulia
Kama unataka kuwa mjasiriamali utapata faida kubwa sana kuzungumza na watu ambao tayari wanafanya ujasiriamali. Ukiwa na bahati kumpata mwenye moyo wa dhati wa ujasiliamali hatokuficha kitu ili kukusaidia ufikie ndoto yako. Kwani kiasili mjasiriamali huwa anajitoa kuisadia jamii yake na hana haja ya kuwa mchoyo wa maarifa.

6. Tengeneza marafiki
Yeyote anayetaka kuwa mjasiriamali ni lazima atengeneze marafiki wengi wenye mtazamo chanya kama yeye. Usiwe na marafiki ambao unatofautiana nao mtazamo, watakuwa wanakukatisha tamaa kwani kwao hilo wazo wanaona haliwezekani na watakwambia huwezi.

Kauli kama hizo zitakukatisha tamaa na ukizingatia wazo lolote mwanzo huwa gumu na haliwezekani mpaka uanze kulifanyia kazi. Ndio ule msemo wa ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi unaingia hapa.

7. Tengeneza wazo rahisi kutekelezeka
Kama unataka kuwa mjasiliamali ni vyema ukawa umechagua eneo moja maalumu la kulitafutia ufumbuzi na ambalo rahisi kutekelezeka na pia kuwa makini na hilo jambo unalotaka kulifanyia kazi uwe na uzoefu nalo japo kidogo, kwani huwezi kutibu ugonjwa usijua hata unakaa wapi.

8. Fanya bidii kuliko wengine
Hapa lazima utambue kuwa kila mtu anaweza kuwa mjasiriamali, lakini tofauti huja katika bidii wanayoweka katika shughuli waliyochagua. Kama umejitolea kuwa mjasiriamali ni lazima ujitoe kufanya kazi kwa bidii kuliko mtu yeyote yule.

9. Tafuta mshauri.
Ukitaka kuwa mjasiriamali ni vizuri ukawa na mtu anayekuongoza kwa mawazo kwani si kila wakati utakuwa unawazo sahihi. Si kwamba yeye ndio awe anakutengenezea wazo bali anaweza akawa anapitia wazo lako na kukushauri kama uboreshe au kuna vitu uondoe. Ikiwa utampata mshauri mzuri itakusaidia kupunguza hatari ya kuumia mapema. Kuwa makini na mtu utakayemchagua, uwe unamuamini na awe hana ushindani na wewe.

10. Hakikisha unafurahia
Hapa ni lazima ujue, kama unataka kuwa mjasiriamali mzuri na utakayefanikiwa ni lazima ufanye kitu unachokipenda. Unapokuwa unafanya kitu unachokipenda unajitengenezea mazingira ya kufanikiwa na kuwa na furaha muda mwingi.

11. Fanyia kazi hatari (risk)unayoifahamu
Sifa ya mjasiriamali wa kweli, ni yule asiyeingia kichwa kichwa kutaka kutatua tatizo pasipo kupiga hesabu za kutosha za hatari iliyopo. Mjasiriamali wa kweli huwa anachukua hatari za jamii na kujibebesha yeye lakini anapaswa achukue hatari (risk) ambayo hesabu zake anazifahamu.

12. Hudhuria semina na makongamano
Wewe kama unataka kuwa mjasiriamali ni lazima utenge muda wako kuhudhuria semina mbali mbali, zinazohusiana na shughuli unazotaka kuja kufanya. Unapohudhuria maeneo kama hayo itakusaidia kutengeneza mtandao na watu wengine na hata kukutana na watu wanaoweza kukusaidia kufika unapotaka.

Kwa wale wote wenye mawazo ya kutaka kujiajiri, hizo ni baadhi ya hatua ambazo wanaweza kuzitumia katika kufikia ndoto zao. Wanaweza kuvitumia vidokezo hivyo kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

Nawatakia kila la kheri katika safari yenu ya kuelekea kwenye mafanikio ya kibiashara.
 
Wacha nimalizie kulisha mifugo ya nzengo nitarejea kusoma hizi nondo.
 
Back
Top Bottom