Aisee,
Mimi ni moja ya watu niliyefanya maamuzi magumu ya kuacha kazi nzuri na kwenda kujiajiri...
Ofcoz nakiri kwamba, Utoto na uharaka wa kupata mafanikio kwa mura mfupi ulichangia.
Niliajiriwa soon after school, nikafanya kazi kama mwaka na nusu kwenye makampuni mawili, moja ni kampuni kubwa tu hapa nchini.
Nilisave ela nyingi na nyingine nikaongezewa, then nikapiga kazi chini.
Kuna kabiashara nilikuwa nakiendesha nikiwa kazini, baada ya kuona inalipa kwa kiasi fulani bila ya kuwa commitment sana nikapiga kazi chini niwekeze nguvu huko.
Aisee,
Niligundua makosa niliofanya,
1. Fedha niliyowekeza ndio nilitegemea inipe mahitaji yote yangu.
2. Sikuweka akiba, na sikuwa na source nyingine ya kipato
3. Matumizi ya hela yalikuwa rafu sanaa, yani viwanja, totoz, pambaz ilikuwa sanaa tu.
Pamoja na makosa hayo, Mziki ukaja wa TRA,
Nilikula fine za maana na ndo ukawa mwisho wangu.
Japo biashara ile ilikuwa inalipa, ila vikwazo vikawa mipakani, yani mwaka mpya wa kodi ukaja na kodi zake kwa hizo bidhaa.
Ushauri.
1. Usiache kazi kabla ujajidhihirisha biashara unayofanya inakulikulipa kuliko mshahara
2. Kabla ya kuacha kazi hakikisha unatenga fedha ya matumizi yako ya kila siku kwa mwaka mzima, kuanzia malazi, makazi na chakula na mengineyo.
3. Hakikisha trend ya biashara ni nzuri na unaona future yake,
4. Acha kazi kwa amani na mahusiano mazuri, siku mambo yakiharibika bado unanafasi ya kurudi.
Kwasasa nimerudi mzigoni na kwakua bado sijachoka kutake risk, bado naweka pesa kwenye ishu moja. Nimehamia kwenye Tech investment, naamini kwa mbeleni italipa.
Ila mawazo ya kuacha kazi yapo pale palee.
Alamsiki!!