Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

Ulikosa frugality na matumizi mazuri ya pesa.

Wenye hizo sifa na ngozi ngumu bado wanasonga mdogomdogo ila kwa uhakika.
 
Kuoa ni muhimu mkielewama na mke wako mmoja anapiga mzigo mwinge anafanya biashara. Biashara ikiyumba kazi inakuwa dhamana ya kupata mkopo wa ku boost biashara.
Nimekuelewa Sky,
Nafikiria hivyoo!!

Ila sasa, kupata mwenye spirit hiyo,
Ukioa msomi nae anataka kutafuta kazi,
 
Ungechukua likizo ya miezi mitatu bila malipo na mwezi mmoja wa likizo yako ya mwaka. Miezi minne ingesaidia kuona muelekeo wa biashara.
Sio kila ofisi ina utaratibu huu, ofisi nyingi za private hakunaga kitu kama hichi, pia sharti namba moja la kuacha kazi ni pale kipato cha biashara kinapozidi kipato chako cha unachokipata toka kwenye ajira rasmi hapo unaweza kuacha kazi ila tofauti na hapo inabidi labda ufukuzwe kazi...
 
Mnaoa elimu, oa unaweza elewana nae lakini asiwe chini sana. Matatizo akifika form six na yeye atataka aende chuo hata baada ya kuzaa watoto wawili.
Ngoja nitafute Manka huko Uchagani,
Najua katoto ka Form 4 au 6 failure ni zaidi ya degree au nichukue kaliko ishia diploma niweke ndani
 
Kwanini uache kazi?
hela ya kuchukua tu mwisho wa mwezi ni tamu.tafuta watu makini waendeshe miradi yako.
mkuu hujakutana na kazi zenye maboss wa hovyo...
Jinsi tu wanavyokutreat hutatamani kuendelea na hiyo kazi!!!
 
Sasa mkuu umepigwa majanga kidogo tu umekimbia...
Hata ukirudi utakimbia tena...

Changamoto haziishi, mi mwenyewe nimeacha kazi toka 2013 Julai... mpaka leo nakomaa, kuna wakati mambo yanayumba na kuna muda napiga mamilioni... ko ni kawaida!!
 
Ungechukua likizo ya miezi mitatu bila malipo na mwezi mmoja wa likizo yako ya mwaka. Miezi minne ingesaidia kuona muelekeo wa biashara.

Sio kila mwajiri anatoa hiyo fursa ya kuchukua likizo bila malipo, hasa kwa sekta binafsi.
 
Sio kila ofisi ina utaratibu huu, ofisi nyingi za private hakunaga kitu kama hichi, pia sharti namba moja la kuacha kazi ni pale kipato cha biashara kinapozidi kipato chako cha unachokipata toka kwenye ajira rasmi hapo unaweza kuacha kazi ila tofauti na hapo inabidi labda ufukuzwe kazi...


Hapo ndio draft linapoanzia sasa. Kipato cha kila mwezi, kijumuishe mambo ya bima za afya pia.

Kwa mtu uliyezoea kuajiriwa maisha yako yote leo hii unaambiwa tengeneza faida ya 8M kwa mwezi si unaweza kuokota makopo?
 
Aisee,
Mimi ni moja ya watu niliyefanya maamuzi magumu ya kuacha kazi nzuri na kwenda kujiajiri...

Ofcoz nakiri kwamba, Utoto na uharaka wa kupata mafanikio kwa mura mfupi ulichangia.

Niliajiriwa soon after school, nikafanya kazi kama mwaka na nusu kwenye makampuni mawili, moja ni kampuni kubwa tu hapa nchini.

Nilisave ela nyingi na nyingine nikaongezewa, then nikapiga kazi chini.
Kuna kabiashara nilikuwa nakiendesha nikiwa kazini, baada ya kuona inalipa kwa kiasi fulani bila ya kuwa commitment sana nikapiga kazi chini niwekeze nguvu huko.

Aisee,
Niligundua makosa niliofanya,
1. Fedha niliyowekeza ndio nilitegemea inipe mahitaji yote yangu.

2. Sikuweka akiba, na sikuwa na source nyingine ya kipato

3. Matumizi ya hela yalikuwa rafu sanaa, yani viwanja, totoz, pambaz ilikuwa sanaa tu.

Pamoja na makosa hayo, Mziki ukaja wa TRA,
Nilikula fine za maana na ndo ukawa mwisho wangu.

Japo biashara ile ilikuwa inalipa, ila vikwazo vikawa mipakani, yani mwaka mpya wa kodi ukaja na kodi zake kwa hizo bidhaa.

Ushauri.
1. Usiache kazi kabla ujajidhihirisha biashara unayofanya inakulikulipa kuliko mshahara

2. Kabla ya kuacha kazi hakikisha unatenga fedha ya matumizi yako ya kila siku kwa mwaka mzima, kuanzia malazi, makazi na chakula na mengineyo.

3. Hakikisha trend ya biashara ni nzuri na unaona future yake,

4. Acha kazi kwa amani na mahusiano mazuri, siku mambo yakiharibika bado unanafasi ya kurudi.

Kwasasa nimerudi mzigoni na kwakua bado sijachoka kutake risk, bado naweka pesa kwenye ishu moja. Nimehamia kwenye Tech investment, naamini kwa mbeleni italipa.

Ila mawazo ya kuacha kazi yapo pale palee.

Alamsiki!!
Shukran kwa ushauri
Ila bado nina wazo la kuacha kazi na kujiajiri,
 
Mnavobebelea kuajiriwa mnadhan cc ambao hatujaariwa hatuendeshi familia zetu, ajira ni kama kua na mzazi akishadead unapambana kwa kila hali na hakuna lisilowezekana
 
Hhahahah
Hapo ndio draft linapoanzia sasa. Kipato cha kila mwezi, kijumuishe mambo ya bima za afya pia.

Kwa mtu uliyezoea kuajiriwa maisha yako yote leo hii unaambiwa tengeneza faida ya 8M kwa mwezi si unaweza kuokota makopo?
 
Back
Top Bottom