Vijana watakiwa kuwa nguzo ya maadili na ujenzi wa Taifa katika kumbukizi ya miaka 104 ya Baba wa Taifa

Vijana watakiwa kuwa nguzo ya maadili na ujenzi wa Taifa katika kumbukizi ya miaka 104 ya Baba wa Taifa

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
Dodoma, Aprili 11, 2026

IMG_2269.jpeg

Kongamano la vijana ya kumbukizi ya miaka 104 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Julius Nyerere, limefanyika leo Jumamosi katika Ukumbi wa Chimwaga, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kongamano hilo limewakutanisha viongozi wa serikali, wanafunzi na vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mgeni Rasmi katika kongamano hilo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ambaye amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda maadili, amani na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa madhubuti.

IMG_2271.jpeg

Akizungumza katika kongamano hilo, Mhe. Nchimbi amesema mafundisho ya Mwalimu Nyerere bado yana mchango mkubwa katika kuongoza kizazi cha sasa na kijacho, hasa katika kuimarisha umoja, uzalendo na uwajibikaji miongoni mwa vijana.

“Vijana wa leo ni viongozi wa kesho. Ni muhimu kuzingatia misingi ya maadili, kufanya kazi kwa bidii na kulinda amani ya nchi yetu,” alisisitiza.

“Tusimame na tuseme tunaulinda umoja wetu kwa nguvu zetu, tutatumia elimu na ubunifu katika kukuza maendeleo ya taifa letu,” aliongeza.

Kongamano hilo limebeba kauli mbiu isemayo: “Vijana na Mwalimu Nyerere: Imarisha vijana kwa ujenzi wa taifa madhubuti na maadili ya kitaifa,” ambayo imehamasisha mijadala kuhusu nafasi ya vijana katika maendeleo ya taifa.
IMG_2268.jpeg
IMG_2270.jpeg
 
Back
Top Bottom