Vijana wazuiwa kujiunga na Shirika la Serikali kwa kuwa na Tattoo

Mkuu,

Unaelewa kuwa haya mazungumzo yetu tu, tunavyojibizana hapa JF, inawezekana kuna watu yanawafungua macho kuhusu mambo mengi?

Na hilo linafanya kwamba, tukiweza hata kuzungumza tu kutoka gia namba 1 ya hapo juu na kwenda gia namba 2, tutakuwa tushaanza ku normalize mambo mengine superficial kama tattoo?

Inawezekana kuna bosi anasoma hapa, baadaye kidogo atakutana na candidate mwenye tattoo kwenye interview, na pengine mazungumzo haya yakamfungua macho bosi aangalie vitu vya msingi zaidi, ujuzi, uadilifu etc, kutoka kwa candidate, kuliko kuishia kwenye tattoo tu?

Huoni kama ikiwa kuna chance ya watu kuelimika kidogo tu hapa, mazungumzo ya abstract kuangalia gia namba 2 yataweza kutufaa sana kuliko kuishia gia namba 1 tu na default shortcut ya ape like thinking kwamba "tattoo = bad" ?
 

Kwa wenzetu yes but inategemeana, mfano us army prohibits tattoos on the head, face, neck above the t-shirt collar, wrists or hands other than one ring tattoo per hand that must rest where a normal ring would
But ukienda Us marines ni almost impossible

Na nadhani kwa taasis za majeshi wana restriction
Nys ni youth service kama ilivyo JKT

Kwa taasis za kiraia nadhani restriction ndio kidogo. It depends na nchi
 
Hapo pia kuna kitu kingine muhinu sana umekitaja.

Nuance. Calibration. Negotiation.

Wenzetu wanaweka vitu kwenye mizani sana.

Unaweza kuweka tattoo, lakini usiweke kwenye sura, unaweza kufanya hivi, lakini kwa kiasi hiki.

Na sheria zao wanazirejea na kuzi update kulingana na mazingira na muda.

Sisi huko tunapenda sana "all or nothing at all".

Yani ukiwa na tattoo hata kwenye korodani watakuchunguza waione mradi wakukatalie tu.

Mwishowe unamkataa bonge la commando, kwa sababu ana tattoo ambayo akivaa chupi huioni.
 
Kabisa ni kweli kabisa mkuu.

Tattoo uzuri wake sio kilevi, hakiathiri akili ya mtu kwa namna yoyote ile.

Tatizo ni hii Tanzania yetu ya ajabu mkuu.
Mfano mimi ilinichukua muda kidogo mpaka kuja kunyoa vile mimi napenda, utoto wangu nilikua nanyoa flat kitu ambacho nilikua sipendi kabisa ila ni shule ndio ililazimisha.

Kunyoa kunaaffect vipi akili ya mtoto?? Imagine shuleni hata kunyoa upara ilikatazwa!! Upara unaathiri vipi perfomance yako kama ndio style unayopenda??

Ukivaa suruali iliyokubana (modo) inachanwa hadharani, sasa hapo kinachoathiri perfomance ni kuchaniwa suruari hadharani au mimi kuvaa kitu ninachopenda.
 
Kuna siku nilikaa na dogo mmoja hapa, kazaliwa US. Nikawa namuelezea jinsi tulivyosoma shule Tanzania, discipline, mavazi, nywele.

Alikuwa na nywele dreads. Nikawa namwambia enzi zetu Tanzania mwalimu akikukuta na nywele kama hivi anakunyoa, halafu hakunyoi zote, anakunyoa mbele tu ukamalizie mwenyewe.

Akasema that is a gross violation of self expression. Yani mtoto mdogo anatetea haki zake za self expression.

Alikuwa anashangaa kila kitu. Kabla ya kufika kwenye nywele kwanza alikuwa anashangaa watu wamesomaje kwa kuvaa uniform bila kuchagua nguo zao wenyewe?

Yani nikiona kitu sikipendi tu wameachiwa shuleni, nasema "enzi zetu Africa ilikuwa huruhusiwi kufanya hivyo".

Na yeye anacheka anasema huo ukoloni ni moja ya sababu Afrika inashindwa kuendelea.
 
Acha tu mkuu.

Hamna kitu napenda kama nikiona mtoto mdogo anajiamini.
Sisi kwenye malezi yetu hatukupewa nafasi ya kujiamin, hatukuruhusiwa kua sisi, utajuaje kipaji chako huku unaishi maisha ya baba/mama yako na si yako.

Sasa hivi kidogo madogo wanahoji, japo bado changamoto ni kua kina baba wengi walilelewa kizamani, kumjibu anataka ila hajui amjibu nini.

Bila shaka huko mbele jamii yetu itabadili mitazamo mingi, japo inakuja na changamoto nyingi wapo watakaoimudu.
 
Naam.

Mimi kwangu nimekataa mtoyo akiuliza kitu kumjibu jibu la "kwa sababu mini nimesema hivyo".

Kila kitu kinatakiwa kijibiwe kwa logical explanation, bila kutumia turufu ya "because I said so".

Jibu hili ni logical fallacy ya "argument for authority" na linajenga ukondoo sana.
 
Tatoo ni sehemu ya utamaduni wa makabila mengi sana afrika ila sasa
 
Mtoto asikuogope, akuheshimu.

Walioishi kwa heshima na wazazi wao wana raha sana utu uzima wao.
 
Chungu kumeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…