MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Tukitoa changamoto zingine zinawaandama vijana wa kiume ila hili la kuwa dhaifu (simp) kwa wapenzi wao ni changamoto inayozidi kuwa kubwa. Vijana wengi wamepoteza mwelekeo na kujikuta kwenye majuto baada ya kuingia kwenye mahusiano na wanawake makatili. Huku mtandaoni kumekuwa na wanaharakati wanaowaita vijana kama hao kwa jina baya la SIMP.
Kwa kiasi fulani nakiri kuwa kuna vijana wapumbavu wasioutumia vyama uanaume wao kwenye uhusiano. Ila wengi hujikuta kwenye matatizo baada ya mitishamba kufanya kazi (kulogwa).
Vijana wengi wanafanyiwa mambo ya kishirikina na kujikuta wanakuwa kama mazezeta mbele ya wanawake. Ukitoa wachungaji, mitume na manabii feki kuna kundi kubwa la waganga wa jadi wanaojitafunia hela za wanawake wanaoenda kuloga wanaume zao.
Kwa wale mnaojidanganya uchawi haupo endeleeni hivyohivyo hadi pale mtakapojikuta mikononi mwa hawa maharamia wa mapenzi. Kijana kama huwezi kufuata misingi ya dini yako ya Kikristo au kiislamu hakikisha unaenda huko Kigoma katikati ya Ziwa Tanganyika kujiweka sawa kimila ili kuepusha kuchezewa kijinga.
Kuna dogo mmoja hapa akiambiwa mwanamke wake kakutwa gesti na mwanaume mwingine yeye huenda kumuuliza huyo manzi kama ni kweli alivyoambiwa. Manzi humjibu kuwa hizo ni habari za uchonganishi. Dogo naye hukubaliana naye kiduwanzi.