vijana wengi wakristo kuogopa na kuchelewa kuoa hadi wafike 30+, zinaa inaepukika ?

Kwahiyo kuoa imekuwa suala la udini?. Vipi Ommy dimpozi ana mke?.
 
Mkuu ukiristo unapotosha watu wengi acha ufunuliwe watu wajue ukweli

JF is where we talk openly
Na wakristo nao watasema uislamu unapotosha wengi. Kwahiyo kwa mtazamo wangu, nafikiri ni bora tungejikita katika mambo ambayo yanaweza kujadilika katika jamii yetu bila kuleta madhara makubwa kama haya ya kiimani.
 
Uongo mtupu ulichoandika

Vijana wengi vijijini waliomaliza vyuo huoa mapema na wa mijini wanaotoka familia bora huoa mapema sana sababu mahari na sherehe hugharimiwa na wazazi na ndugu

Mleta mada utakuwa unatoka familia ya masikini wa kutupwa wa mijini au kama umezaliwa kijijini porini huko badala ya kuoa kwenu maporini huko unataka kuoa mtoto wa kike wa familia bora wa mjini

Kaoe watoto wa kike toka familia za maskini wenzio mahari kuku na mayai tu unapata mke ndani .

Shona nguo inayofanana na size yako
 
Duh!...
 
Moderators hebu njooni mfute hizi thread zenye milengo ya dini. Nyingi zina lengo la kuharibu umoja, upendo na mshikamano wetu kama Taifa.

Ni vizuri tubishane kwenye siasa, michezo nk lakini sio dini.
Hebu fikiri tena mkuu ingawa najua una idea nzuri. Hakuna jambo lililopo na linaloletwa na wanaojiita watawala Dunia ambalo linania ya kukuunganisha wewe na wenzio. Hiyo siasa pia ina nia hiyo, michezo nk.

Usipokuwa tofaut na mwenzio kimpira utakuwa tofauti kichama. So no way mwaweza kuwa na umoja kamili na mshikamano imara. No way..

Na kwa system ya maisha hamna jingine utaongea lenye kuongeleka na kujadilika kama sio hayo mambo. Ambayo nia ya ndani ni kuleta mpasuko ili tutawalike. Haijalish ww ni waziri au Rais wote tunahitaji kutawalika.

Ova.
 
Kwa kweli ni hatari sana mkuu.
 
Mtoa mada sidhani kama upo sahihi kusema "vijana wa kikristu" badala yake ungesema "vijana wa sasa" sio wakristu wala waislamu,they are all sailing in the same boat.
Sijui research yako umeifanya vipi.

Tufanye research ya chap chap hapa,ebu tukusanye celebraties wawe kama sample,coz ndo vioo vyetu vya jamii.
Mtoa mada ukifanya hii research nadhan vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…