Vijana wenzetu Kaskazini wanateketea kwa ulevi, Serikali lione hili kuokoa hiki kizazi

Mzee Kimamingo

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2024
Posts
2,293
Reaction score
5,418
Habari za muda wana JF

Nipo Moshi huku kuna Msiba wa Ndugu yangu Mmoja.

Ujue Nikijaga Moshi mara nyingi ni December na huwa ni Muda wa Sherehe sikunotice hiki kitu.

Nimekuja sasa hivi nimegundua Moshi vijana wengi nadiriki kusema zaidi ya 70% ni walevi wa hizi Pombe maarufu kama Vichungu au visungura au Highlife.

Serikali Msipoingilia kati tutapoteza nguvu kazi huku kaskazini hali ni mbaya sana.

Serikali serikali Futeni hizi pombe haraka sana.
 
Nimekuja saivi nimegundua Moshi vijana wengi nadiriki kusema zaido ya 70% ni walevi wa hizi Pombe maarufu kama Vichungu au visungura au Highlife.

SHida ya watanzania ni ulimbukeni wa kufakamia kila jambo jipya linaloingia nchini bila kutafakari hasara zake
 
...na msipokuwa makini ,Huko Uchagani sasa kutakuwa na Wachaga Macho Tara,kwa kuwa vijana wanaotoka mikoa mingine kwenda kumtafuta kazi ...ndio wanapiga miti mabinti zenu....na wengine wanawaoa kabisa kwa baraka nyingi za wazazi ! Na vihampa wanapewa !
 
Si huwa mnajishadadia mnajiita USA, ngojeni kiwalambe!, mkuu mbona kama umechelewa sana kulijua hili wengine hatukai huko lkn kwa data tu zimetosha kutuambia kuwa huko mpo kwenye hali mbaya!
 
Habari za muda wana JF

Nipo Moshi huku kuna Msiba wa Ndugu yangu Mmoja.
Ujue Nikijaga Moshi mara nyingi ni December na huwa ni Muda wa Sherehe sikunotice hiki kitu.
Nimekuja saivi nimegundua Moshi vijana wengi nadiriki kusema zaido ya 70% ni walevi wa hizi Pombe maarufu kama Vichungu au visungura au Highlife.
Serikali Msipoingilia kati tutapoteza nguvu kazi huku kaskazini hali ni mbaya sana.
Serikali serikali Futeni hizi pombe haraka sana.
Jukumu la wazazi hilo
Wazazi wao pia ni chapombe hatari
Na wanafundisha kunywa pombe watoto wao toka wadogo.Mtoto mdogo kabisa unakuta ananyweshwa pombe na mzazi

Kuna mtoto alilalamika kuwa mchungaji kanisani akiwafundisha mafundisho ya kipaimara aliwaambia watoto kuwa mtoto lazima awe mtii kwa mzazi kuwa unatumwa na mzazi nenda kaniletee mbege halafu ukakataa.Mzazi akaja kushtaki Hupati kipaimara mtoto wewe sababu huna utii kwa mzazi

Sasa kwenye mazingira hayo unataka serikali ifanye nini?
Jamii imeamua kuwa Chapombe kuanzia Wazazi watoto na viongozi wao wa dini
 
Niliwahi kuandika humu kuhusu hili mkuu siyo huko tu ni sehemu zote. Ilitokea siku moja hapa kazini tukaletewa pombe za kujipimia kwenye mitungi asee sikuamini kabisa vijana miaka17 na hata chini ya hapo ni walevi kupindukia mbaya zaidi pombe zilikuwa zabure sio konyagi wala k van zote buree Tani yako ukipenda unabeba chupa zisizo zidi 3 kubwa na 5 ndogo aisee sikuamini.

Kuna vijana wadogo wanakunywa sijawahi Ona.

Sasa ukifika mtaani hizo pombe za ovyo ovyo kama ulivyotaja zimejaa vibaya mno wanasema unanujuaje bia buku2 ili hali ukinuni roboti Visungura unalewa kwa buku2 hapo sasa ukilinganisha na uchumi wao wanakunywa mbaya mno.

Nikweli serkali iwanusuru vijana
 
Bro kwani hizo pombe zinauzwa Kaskazini peke yake?ulimbukeni wao ndio utawaua.Unataka serikali ifungie hizo pombe.sasa vipi kuhusu viwanda vinavyozalisha hizo pombe,ushawaza ni watu wangapi watapoteza ajira?
Vipi kodi zinazolipwa serikalini?Hujui kuwa bilionea Mulokozi atashuka kwenye chati😀😀
 
Huna unalolijua hujui kuwa serikali ilishawahi kufungia baadhi ya pombe
 
Habari za muda wana JF

Nipo Moshi huku kuna Msiba wa Ndugu yangu Mmoja.

Ujue Nikijaga Moshi mara nyingi ni December na huwa ni Muda wa Sherehe sikunotice hiki kitu.

Nimekuja sasa hivi nimegundua Moshi vijana wengi nadiriki kusema zaidi ya 70% ni walevi wa hizi Pombe maarufu kama Vichungu au visungura au Highlife.

Serikali Msipoingilia kati tutapoteza nguvu kazi huku kaskazini hali ni mbaya sana.

Serikali serikali Futeni hizi pombe haraka sana.
Kwa utafiti wako kati ya yule jamaa mlevi anaitwa Pierre Liquid na hao jamaa wa Kaskazini ni nani mlevi zaidi?
Mbona serikali haingilii kati ulevi wa Pierre Liquid pamoja na kutangaza ulevi wake kwenye mitandao ya kijamii?
 
Habari za muda wana JF

Nipo Moshi huku kuna Msiba wa Ndugu yangu Mmoja.

Ujue Nikijaga Moshi mara nyingi ni December na huwa ni Muda wa Sherehe sikunotice hiki kitu.

Nimekuja sasa hivi nimegundua Moshi vijana wengi nadiriki kusema zaidi ya 70% ni walevi wa hizi Pombe maarufu kama Vichungu au visungura au Highlife.

Serikali Msipoingilia kati tutapoteza nguvu kazi huku kaskazini hali ni mbaya sana.

Serikali serikali Futeni hizi pombe haraka sana.
Kitu cha Moshi hiko
 
Back
Top Bottom