Mabunge mengi hata ya weupe mtifuano ni mkali tu.Kuna wakati hisia huzidi na mieleka, ngumi, karate,judo,kutupiana chupa, kutukanana, kuzomeana kumeshuhudiwa Taiwan, Korea Kusini, Uingereza,Israel,Nepal, New Zealand, Venezuela n.k. Ni mabunge machache tu yenye utulivu wa kweli mathalani Uswisi. Yale ya Korea Kaskazini na China ya zidumu fikra za Mwenyekiti ambayo ni ya ndiyo mzee kuliko ya kwetu huwa na utulivu wa kukwepa adhabu na mara nyingi mambo huwa yameamuliwa kwenye kamati mbalimbali hivyo ni mwendo wa kutulia tu usionekane mtata. Sishabikii hayo mambo ya kina Lugola na vituko vingine vingi visivo tija ila bunge kwa namna moja linaakisi 'sehemu' ya jamii linalowakilishwa.