Vikwazo kwa Urusi; Sarafu ya ruble ya Urusi yapanda thamani dhidi ya dola ya Marekani

Vikwazo kwa Urusi; Sarafu ya ruble ya Urusi yapanda thamani dhidi ya dola ya Marekani

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
VIKWAZO KWA URUSI;SARAFU YA RUBLE YA URUSI YAPANDA THAMANI DHIDI YA DOLA YA MAREKANI.

Leo 15:30pm 27/03/2022

Respect for Russia,who dare to stand up against the West,Baada ya vikwazo vingi vya Ulaya na Marekani kwa Urusi,Urusi imetangaza kuuza mafuta na Gesi kwa sarafu yake ya ruble,Masaa 24 baada ya Urusi kutangaza kuuza mafuta na Gesi kwa ruble, sarafu hiyo imepanda maradufu na kuifanya iwe na nguvu mbele ya dollar na Euro,Juzi thamani ya ruble kwa dola ilikuwa hivi,$1 sawa na Ruble 139 na leo $1 sawa na Ruble 97 huku ni kuimarika kwa hali ya juu kwa sarafu ya ruble,Uarabuni napo wameanza mchakato wa kuanza kuuza mafuta kwa kutumia sarafu ya Yuan ya China.

Thamani ya pesa ni matumizi yake,uhitaji wa sarafu ya ruble ya Urusi ili kuweza kununua mafuta na Gesi kunapandisha matumizi ya pesa hiyo ya ruble,kwa sasa thamani ya dola ipo juu sababu ya uhitaji wake katika kununua vitu nje ya nchi,hamani ya dola inakuja kwenye upande wa kufanya miamala,Telegraphic transfer (TT) kupitia mfumo wa SWIFT,kwa siku kuna miamala mingi ya dola hapa duniani kwa sasa,lakini punde tutaiona miamala mingi ya sarafu ya ruble kwa ajili ya kuagiza mafuta na Gesi,tukumbuke pia tunaweza kuanza kuona miamala ya sarafu ya yuan ya China ikiagiza bidhaa mbalimbali iwapo China itaamua hivyo,Tanzania inaongoza kwa 80% kununua bidhaa mbalimbali toka China.

Kwa namna moja ama nyingine uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ulikuwa ni mpango mkakati wa kumdhoofisha kiuchumi Marekani and the so-called NATO,kiwango cha mfumuko bei ni kikubwa Ujerumani ni 12% haijawahi kutokea tangu vita vya Hitler, Ujerumani wanategemea mafuta na Gesi ya Mrusi,Hispania 9% haijawahi kushuhudia kwa zaidi ya miaka 40, Uingereza bei ya mafuta inakaribia kufumuka kwa 80% kuelekea 100%

Tayari Urusi imechukua hatua mpya ya kuondoa kabisa utegemezi kwa sarafu ya dola ili kukabiliana na mashinikizo ya vikwazo vya Marekani na utumiaji mbaya wa sarafu ya dola unaofanywa na Washington kama nyenzo ya kuiwekea mashinikizo Moscow,punde si punde sarafu ya ruble itaingia kwenye mfumo wa kimataifa wa fedha na kuwa sarafu mbadala wa dola,Baada ya mgogoro wa Ukraine wa mwaka 2014,Russia imekuwa ikiandamwa kwa kupewa vikwazo vikali vya Marekani na Umoja wa Ulaya,

Siku zote Marekani imekuwa ikiitumia dola, ambayo ndiyo sarafu kuu ya kigeni inayotumika katika miamala ya kimataifa, kama silaha ya kuziwekea mashinikizo nchi zingine,imeutumia vibaya mara kadhaa na kwa maslahi yake kwenye utegemezi wa makampuni, mabenki na mifumo ya fedha ya kimataifa kwa sarafu ya dola kama nyenzo na silaha ya kuzilazimisha nchi zingine zifuate matakwa yake au kuzibana zisifuate siasa na sera zisizoipendeza nchi hiyo. Jambo hili limezikera si nchi pinzani pekee bali hata nchi waitifaki wa Ulaya na Washington na kupelekea kujitokeza taratibu fikra ya pamoja kimataifa ya kuzuia mwendelezo wa utumiaji kimaslahi wa sarafu ya dola unaofanywa na Marekani kwa ajili ya kuzishinikiza kiuchumi, kibiashara na hata kifedha nchi zingine hasa zilizo wapinzani au washindani wa nchi hiyo.

Kutokana na vikwazo vikali ilivyowekewa urusi , ikiwa ni pamoja na kuteneganishwa rasmi na dola na euro, taasisi za kifedha za Urusi kama mabenki yamemelazimika kugeukia sarafu yao ya ruble na sarafu ya yuan ya China,Benki ya VTB inayomilikiwa na serikali ya Urusi imewapa wateja wake fursa ya kufungua akaunti ya akiba ya Ruble na Yuan ya Uchina ambayo inatoa kiwango cha juu cha riba cha asilimia 8%.ni dhahiri kama wataunda 'coalition' katika maswala ya kisarafu kwa kuachana na dola, basi wazi marekani itaanguka kiuchumi,Combination ya Mchina na Mrusi ni jinamizi kwa nchi za magharibi,mmoja atafanya kazi ya kutandika magharibi kijeshi, upande mwingine utamtandika magharibi kiuchumi,kazi ipo kwa Ulaya na Marekani,wao kapu la mayai limebebwa na taifa moja la Marekani, Mmarekani akianguka kijeshi basi hata na kiuchumi anapotea,

Nimalizie kwa kutanabaisha ya kwamba kuiondoa sarafu ya dola ni process,na hiyo wanayofanya Urusi ndio process yenyewe,tumetoka kwenye dola dola dola kila upande,kila kitu kina mwisho,mataifa yamechukua muda mrefu kutafuta namna ya kuiangusha dola,huwezi kutaka kuiangusha dola kwa mwaka mmoja au miezi ni muongo kama sio miongo mpaka karne,hata uchina walitolewa katika masuala ya anga ya kituo kinachomilikiwa na US ila mpaka kua na kituo chao ilichukua miongo kadhaa iliyokaribia karne,hivyo basi suala la dolar kuondoka ni suala la muda tuu na tayari dalili zimeanza kuonekana.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Hainipi shida kusema
emoji1666.png
, wewe ni mchambuzi
 
Sasa imekuaje Putin ameomba mataifa ya ulaya kununua mafuta ya urusi kwa pesa za urusi ili kuokoa sarafu yake isishuke thamani. kitu ambacho nimeona tayari rais wa ufaransa amekipinga
 
No matter how strong the strategies they have [Russian and Chinese block], they'll not make it to lead the World economically, socially or militarily.... the fate is not on their side....

I don't see the future for China, Russia or even the USA as the world leader and Super power... it seem there changes in dynamics of Global leadership...

Let us wait to witness if we're luck enough...
 
Mrusi wa buzza katika ubora wako,,

Achen kushangilia Vita visivyo na msingi,, watu wanauawa ,, watu wanakimbia makazi yao kisa Vita nyinyi mnaleta propaganda zenye mahaba yasiyo na tija!!

Inaonekana ulifurahi kuona Iddi Amin akitunishia msuli Tanzania sio!!?
 
No matter how strong the strategies they have [Russian and Chinese block], they'll not make it to lead the World economically, socially or militarily.... the fate is not on their side....

I don't see the future for China, Russia or even the USA as the world leader and Super power... it seem there changes in dynamics of Global leadership...

Let us wait to witness if we're luck enough...
👍
 
Acha uongo
Dola bado ipo juu
Huyu Leslie Mbena, Ukweli ataujulia wapi??

Alisifu na kuabudu mwendakuzimu, na hakuwahi kupata uteuzi!
Akajaribu kugombea ubunge. Wajumbe vichwa vyao wakafanya Yao!

Sasa huenda Central Bank ya Russia ikamuona! Ikamlipa kwa propaganda hizi!
 
At this time and age are you still supporting a demonic nation like Russia? I feel super sorry for you my dear amigo, Rise and fall of Russian empire is at hand , wake up from the splendo!Puttin has opened a pandora box yet it is unknown size, why dare you say Rubbo is superior over Dolla? You are the most excellent liar the Tanzanians have ever heard!
 
Sijui unatoa wapi taarifa zako!
Leo hii 27/03/22 Russian ruble moja sawa na senti 20 za USA au TSH 20 za bongo!
emoji41.png
emoji851.png
emoji857.png
 
Hata ikipanda nani ataitumia hiyo pesa kufanya manunuzi yake kimataifa.

Sehemu kubwa ya Dunia bado inategemea Dola.
uchumi wa ruble ,wanaita uchumi wa PUTO. Muda wowote unapasuka.
 
Back
Top Bottom