Vikwazo kwa Urusi; Sarafu ya ruble ya Urusi yapanda thamani dhidi ya dola ya Marekani

Muda huu

Screenshot_2022-03-27-17-47-04-85.jpg
 
Hahahah umenirudisha Google tarehe 22 Feb 2022 1 Usd was 78 Ruble today 1Usd is 102 Ruble hata Tanzania Usd imepanda mpaka 2303 purchase rate
 
VIKWAZO KWA URUSI;SARAFU YA RUBLE YA URUSI YAPANDA THAMANI DHIDI YA DOLA YA MAREKANI.

Leo 15:30pm 27/03/2022

Respect for Russia,who dare to stand up against the West,Baada ya vikwazo vingi vya Ulaya na Marekani kwa Urusi,Urusi imetangaza kuuza mafuta na Gesi kwa sarafu yake ya ruble,Masaa 24 baada ya Urusi kutangaza kuuza mafuta na Gesi kwa ruble, sarafu hiyo imepanda maradufu na kuifanya iwe na nguvu mbele ya dollar na Euro,Juzi thamani ya ruble kwa dola ilikuwa hivi,$1 sawa na Ruble 139 na leo $1 sawa na Ruble 97 huku ni kuimarika kwa hali ya juu kwa sarafu ya ruble,Uarabuni napo wameanza mchakato wa kuanza kuuza mafuta kwa kutumia sarafu ya Yuan ya China.

Thamani ya pesa ni matumizi yake,uhitaji wa sarafu ya ruble ya Urusi ili kuweza kununua mafuta na Gesi kunapandisha matumizi ya pesa hiyo ya ruble,kwa sasa thamani ya dola ipo juu sababu ya uhitaji wake katika kununua vitu nje ya nchi,hamani ya dola inakuja kwenye upande wa kufanya miamala,Telegraphic transfer (TT) kupitia mfumo wa SWIFT,kwa siku kuna miamala mingi ya dola hapa duniani kwa sasa,lakini punde tutaiona miamala mingi ya sarafu ya ruble kwa ajili ya kuagiza mafuta na Gesi,tukumbuke pia tunaweza kuanza kuona miamala ya sarafu ya yuan ya China ikiagiza bidhaa mbalimbali iwapo China itaamua hivyo,Tanzania inaongoza kwa 80% kununua bidhaa mbalimbali toka China.

Kwa namna moja ama nyingine uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ulikuwa ni mpango mkakati wa kumdhoofisha kiuchumi Marekani and the so-called NATO,kiwango cha mfumuko bei ni kikubwa Ujerumani ni 12% haijawahi kutokea tangu vita vya Hitler, Ujerumani wanategemea mafuta na Gesi ya Mrusi,Hispania 9% haijawahi kushuhudia kwa zaidi ya miaka 40, Uingereza bei ya mafuta inakaribia kufumuka kwa 80% kuelekea 100%

Tayari Urusi imechukua hatua mpya ya kuondoa kabisa utegemezi kwa sarafu ya dola ili kukabiliana na mashinikizo ya vikwazo vya Marekani na utumiaji mbaya wa sarafu ya dola unaofanywa na Washington kama nyenzo ya kuiwekea mashinikizo Moscow,punde si punde sarafu ya ruble itaingia kwenye mfumo wa kimataifa wa fedha na kuwa sarafu mbadala wa dola,Baada ya mgogoro wa Ukraine wa mwaka 2014,Russia imekuwa ikiandamwa kwa kupewa vikwazo vikali vya Marekani na Umoja wa Ulaya,

Siku zote Marekani imekuwa ikiitumia dola, ambayo ndiyo sarafu kuu ya kigeni inayotumika katika miamala ya kimataifa, kama silaha ya kuziwekea mashinikizo nchi zingine,imeutumia vibaya mara kadhaa na kwa maslahi yake kwenye utegemezi wa makampuni, mabenki na mifumo ya fedha ya kimataifa kwa sarafu ya dola kama nyenzo na silaha ya kuzilazimisha nchi zingine zifuate matakwa yake au kuzibana zisifuate siasa na sera zisizoipendeza nchi hiyo. Jambo hili limezikera si nchi pinzani pekee bali hata nchi waitifaki wa Ulaya na Washington na kupelekea kujitokeza taratibu fikra ya pamoja kimataifa ya kuzuia mwendelezo wa utumiaji kimaslahi wa sarafu ya dola unaofanywa na Marekani kwa ajili ya kuzishinikiza kiuchumi, kibiashara na hata kifedha nchi zingine hasa zilizo wapinzani au washindani wa nchi hiyo.

Kutokana na vikwazo vikali ilivyowekewa urusi , ikiwa ni pamoja na kuteneganishwa rasmi na dola na euro, taasisi za kifedha za Urusi kama mabenki yamemelazimika kugeukia sarafu yao ya ruble na sarafu ya yuan ya China,Benki ya VTB inayomilikiwa na serikali ya Urusi imewapa wateja wake fursa ya kufungua akaunti ya akiba ya Ruble na Yuan ya Uchina ambayo inatoa kiwango cha juu cha riba cha asilimia 8%.ni dhahiri kama wataunda 'coalition' katika maswala ya kisarafu kwa kuachana na dola, basi wazi marekani itaanguka kiuchumi,Combination ya Mchina na Mrusi ni jinamizi kwa nchi za magharibi,mmoja atafanya kazi ya kutandika magharibi kijeshi, upande mwingine utamtandika magharibi kiuchumi,kazi ipo kwa Ulaya na Marekani,wao kapu la mayai limebebwa na taifa moja la Marekani, Mmarekani akianguka kijeshi basi hata na kiuchumi anapotea,

Nimalizie kwa kutanabaisha ya kwamba kuiondoa sarafu ya dola ni process,na hiyo wanayofanya Urusi ndio process yenyewe,tumetoka kwenye dola dola dola kila upande,kila kitu kina mwisho,mataifa yamechukua muda mrefu kutafuta namna ya kuiangusha dola,huwezi kutaka kuiangusha dola kwa mwaka mmoja au miezi ni muongo kama sio miongo mpaka karne,hata uchina walitolewa katika masuala ya anga ya kituo kinachomilikiwa na US ila mpaka kua na kituo chao ilichukua miongo kadhaa iliyokaribia karne,hivyo basi suala la dolar kuondoka ni suala la muda tuu na tayari dalili zimeanza kuonekana.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Marekani asiponunua mafuta yako,hakuna mnunuzi mwingine duniani wa kukupa faida. Ndio maana akitaka kuyumbisha Bei ya mafuta anasimama kununua halafu anatumia reserve yake. Haya umewekewa vikwazo hayo mafuta yanapitia wapi? Kwa ni upunguani kushabikia vita ambayo kwetu inatupa maumivu. Ni mpumbavu tu wa kiwango chako anayeweza kushabikia vita hii ya kishenzi.
 
Hata ikipanda nani ataitumia hiyo pesa kufanya manunuzi yake kimataifa.

Sehemu kubwa ya Dunia bado inategemea Dola.
Ndg. Stroke unamatatizo sana ya kupinga mambo kabla hujasoma, mara nyingi umekua hodari wakupinga maono ya wenzio kumbe ni kwa sababu ya uvivu kusoma na si kupinga kwa hoja za uchambuzi katika uelewa wa mambo mbalimbali.

Sijajua kiwango chako cha uelewa na ujuzi wa mambo ya kidunia ila nahisi unamatatizo katika uelewa wako kwa kudhani kuwa wewe ni mjuvi wa mambo na kumbe ni zwazwa tu mkurupukia hoja usie jua lolote Mxieuzzzsss!!!

Mleta mada hajasema kuwa dola tayari imeanguka ndio maana kaongelea process

Jaribu kuappriaciate maoni ya wenzio kwa kutoa hoja kwa manufaa ya wana jukwaa wa JF sio kupinga tu ilimradi unapinga wakati hujui hata unachokipinga ni kitu gani.

Mleta Mada aliweka bayana katika maandishi yake, namnukuu kama ifuatavyo:

".... kuiondoa sarafu ya dola ni process,na hiyo wanayofanya Urusi ndio process yenyewe ..."

"... mataifa yamechukua muda mrefu kutafuta namna ya kuiangusha dola ..."

"... huwezi kutaka kuiangusha dola kwa mwaka mmoja au miezi ni muongo kama sio miongo mpaka karne ..."

" ... suala la dolar kuondoka ni suala la muda tuu na tayari dalili zimeanza kuonekana ..."

Mwisho wa kunukuu.

Ndg. Stroke siku zote MJUAJI ASIE JUA HATOJUA MAISHA YAKE YOTE [emoji849][emoji849][emoji849]
 
Putin ananyooshwa kisawasawa hakosi propaganda, damu za watu atazilipa tu.

Ananyooshwa na nani? Putin ndiye kiboko wa nchi za Magharibi na Kibwengo wenu Marekani. Mpaka leo ameshindwa kuifunga anga ya Ukraine! Sababu ni nini? Si wanamuogopa mbabe Putin!

Vipi kuhusu damu za watu walio uwawa na Marekani kule Vietnam, Iraqi, Syria, Afghanstan, Libya, na kwingineko duniani! Zitalipwa na nani?
 
Aisee yaani MTU anapost utumbo kama na bado anapata wafusia wanaomsapoti? Tanzania tunahitaji elimu zaidi Kwa watoto wetu.
nchi zote ambazo Russia ameingia nao mikataba ya ununuzi WA mafuta wamegoma kufanya biashara Kwa kutumia ruble,kutokana na mikataba Yao inavyodai Russia ameshindwa na Hana namna...siku nyingine jaribu kuuliza Kwanza kabla ya kupost

Sijui unatoa wapi taarifa zako!
Leo hii 27/03/22 Russian ruble moja sawa na senti 20 za USA au TSH 20 za bongo! [emoji41][emoji851][emoji857]
Soma tena nahisi hauujaelewa
amesema
1 USD ilikuwa 139
kwa sasa 1 USD ni 97 baada kutolewa tangazo mafuta yatanunuliwa kwa rubble
hvyo kama viwango ni kweli basi URUSI inashangilia ushindi

sasa hizo figure ulizokuja nazo wewe hazina mashiko mbele ya mada iliyokuja mezani
soma tena uelewe
 
Hata ikipanda nani ataitumia hiyo pesa kufanya manunuzi yake kimataifa.

Sehemu kubwa ya Dunia bado inategemea Dola.

Acha kula bange kama matembele mkuu! Utaishia kutembea uchi mtaani.

Wenzio wanavuta sasa wewe unakula majani mabichi kama mbuzi! Dah!
 
Hahahaha

Alafu kwanini watu wakitokaga masomoni Russia dishi zinayumbaga au vodka nini
Wanawafanyia nini

Ova
Dr. Shika angekuwepo umaarufu ungepanda tena kwani angekuwa mchambuzi pekee wa kuaminika wa vita hii katika media zetu.
 
VIKWAZO KWA URUSI;SARAFU YA RUBLE YA URUSI YAPANDA THAMANI DHIDI YA DOLA YA MAREKANI.

Leo 15:30pm 27/03/2022

Respect for Russia,who dare to stand up against the West,Baada ya vikwazo vingi vya Ulaya na Marekani kwa Urusi,Urusi imetangaza kuuza mafuta na Gesi kwa sarafu yake ya ruble,Masaa 24 baada ya Urusi kutangaza kuuza mafuta na Gesi kwa ruble, sarafu hiyo imepanda maradufu na kuifanya iwe na nguvu mbele ya dollar na Euro,Juzi thamani ya ruble kwa dola ilikuwa hivi,$1 sawa na Ruble 139 na leo $1 sawa na Ruble 97 huku ni kuimarika kwa hali ya juu kwa sarafu ya ruble,Uarabuni napo wameanza mchakato wa kuanza kuuza mafuta kwa kutumia sarafu ya Yuan ya China.

Thamani ya pesa ni matumizi yake,uhitaji wa sarafu ya ruble ya Urusi ili kuweza kununua mafuta na Gesi kunapandisha matumizi ya pesa hiyo ya ruble,kwa sasa thamani ya dola ipo juu sababu ya uhitaji wake katika kununua vitu nje ya nchi,hamani ya dola inakuja kwenye upande wa kufanya miamala,Telegraphic transfer (TT) kupitia mfumo wa SWIFT,kwa siku kuna miamala mingi ya dola hapa duniani kwa sasa,lakini punde tutaiona miamala mingi ya sarafu ya ruble kwa ajili ya kuagiza mafuta na Gesi,tukumbuke pia tunaweza kuanza kuona miamala ya sarafu ya yuan ya China ikiagiza bidhaa mbalimbali iwapo China itaamua hivyo,Tanzania inaongoza kwa 80% kununua bidhaa mbalimbali toka China.

Kwa namna moja ama nyingine uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ulikuwa ni mpango mkakati wa kumdhoofisha kiuchumi Marekani and the so-called NATO,kiwango cha mfumuko bei ni kikubwa Ujerumani ni 12% haijawahi kutokea tangu vita vya Hitler, Ujerumani wanategemea mafuta na Gesi ya Mrusi,Hispania 9% haijawahi kushuhudia kwa zaidi ya miaka 40, Uingereza bei ya mafuta inakaribia kufumuka kwa 80% kuelekea 100%

Tayari Urusi imechukua hatua mpya ya kuondoa kabisa utegemezi kwa sarafu ya dola ili kukabiliana na mashinikizo ya vikwazo vya Marekani na utumiaji mbaya wa sarafu ya dola unaofanywa na Washington kama nyenzo ya kuiwekea mashinikizo Moscow,punde si punde sarafu ya ruble itaingia kwenye mfumo wa kimataifa wa fedha na kuwa sarafu mbadala wa dola,Baada ya mgogoro wa Ukraine wa mwaka 2014,Russia imekuwa ikiandamwa kwa kupewa vikwazo vikali vya Marekani na Umoja wa Ulaya,

Siku zote Marekani imekuwa ikiitumia dola, ambayo ndiyo sarafu kuu ya kigeni inayotumika katika miamala ya kimataifa, kama silaha ya kuziwekea mashinikizo nchi zingine,imeutumia vibaya mara kadhaa na kwa maslahi yake kwenye utegemezi wa makampuni, mabenki na mifumo ya fedha ya kimataifa kwa sarafu ya dola kama nyenzo na silaha ya kuzilazimisha nchi zingine zifuate matakwa yake au kuzibana zisifuate siasa na sera zisizoipendeza nchi hiyo. Jambo hili limezikera si nchi pinzani pekee bali hata nchi waitifaki wa Ulaya na Washington na kupelekea kujitokeza taratibu fikra ya pamoja kimataifa ya kuzuia mwendelezo wa utumiaji kimaslahi wa sarafu ya dola unaofanywa na Marekani kwa ajili ya kuzishinikiza kiuchumi, kibiashara na hata kifedha nchi zingine hasa zilizo wapinzani au washindani wa nchi hiyo.

Kutokana na vikwazo vikali ilivyowekewa urusi , ikiwa ni pamoja na kuteneganishwa rasmi na dola na euro, taasisi za kifedha za Urusi kama mabenki yamemelazimika kugeukia sarafu yao ya ruble na sarafu ya yuan ya China,Benki ya VTB inayomilikiwa na serikali ya Urusi imewapa wateja wake fursa ya kufungua akaunti ya akiba ya Ruble na Yuan ya Uchina ambayo inatoa kiwango cha juu cha riba cha asilimia 8%.ni dhahiri kama wataunda 'coalition' katika maswala ya kisarafu kwa kuachana na dola, basi wazi marekani itaanguka kiuchumi,Combination ya Mchina na Mrusi ni jinamizi kwa nchi za magharibi,mmoja atafanya kazi ya kutandika magharibi kijeshi, upande mwingine utamtandika magharibi kiuchumi,kazi ipo kwa Ulaya na Marekani,wao kapu la mayai limebebwa na taifa moja la Marekani, Mmarekani akianguka kijeshi basi hata na kiuchumi anapotea,

Nimalizie kwa kutanabaisha ya kwamba kuiondoa sarafu ya dola ni process,na hiyo wanayofanya Urusi ndio process yenyewe,tumetoka kwenye dola dola dola kila upande,kila kitu kina mwisho,mataifa yamechukua muda mrefu kutafuta namna ya kuiangusha dola,huwezi kutaka kuiangusha dola kwa mwaka mmoja au miezi ni muongo kama sio miongo mpaka karne,hata uchina walitolewa katika masuala ya anga ya kituo kinachomilikiwa na US ila mpaka kua na kituo chao ilichukua miongo kadhaa iliyokaribia karne,hivyo basi suala la dolar kuondoka ni suala la muda tuu na tayari dalili zimeanza kuonekana.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.

[emoji635][emoji3577]
 
Huyu Leslie Mbena, Ukweli ataujulia wapi??

Alisifu na kuabudu mwendakuzimu, na hakuwahi kupata uteuzi!
Akajaribu kugombea ubunge. Wajumbe vichwa vyao wakafanya Yao!

Sasa huenda Central Bank ya Russia ikamuona! Ikamlipa kwa propaganda hizi!

Ukweli mchungu ila ndio dawa inawabidi muinywe hamna namna
 
Sijui unatoa wapi taarifa zako!
Leo hii 27/03/22 Russian ruble moja sawa na senti 20 za USA au TSH 20 za bongo! [emoji41][emoji851][emoji857]
Nchi ina viazi hii sio poa, umeambiwa rubble ilishuka hadi $1 = руб.139, leo $1 = руб.101. kwamba huoni kuwa ruble imekuwa strong against dollar kwa kipindi kifupi?
Screenshot_20220327-201039~2.jpg
 
Back
Top Bottom