Vinicius Junior: La Liga imetawaliwa na ubaguzi wa rangi

Dogo aache mbambamba. Kuwa mchezaji bora ni gharama na gharama moja wapo ni wapinzani wako kukubagua emu huyu dogo aangalie wachezaji bora wameputia mkondo gani hadi kupata tuzo kama fifa bestau baloon dior. Modric alionekana floppy ndani ya kikosi cha madrid hata madhabiki wakamuona ni mzigo. But he went against the odds to lift 5 UCL Baloon dior and fifa best
 
Huo mdomo anao La Liga tu? Etoo na Neymar nao walikuwa na mdomo?!
Hamjaelewa concept ya ubaguzi, mchezaji akijitapa na kujikuza ndio wanajaribu kumshusha chini kwa matusi na kejeli. Na sio tu kwa weusi hata Christiano alikua akizomewa na hao hao washabiki wa Real, Courtouis akikanyaga Atletico Madrid ni zomea zomea na matusi mechi nzima lakini sababu ni weupe hatuoni ni ubaguzi.

Waafrika tuache inferiority complex, hiyo tabia ya kucheza cheza akifunga, kujiangusha, kulia Lia na refa ndio inasababisha azomewe. Hiyo fact alipewa na "Koke" ila akaishia kuitwa mbaguzi.

So avune alichopanda. Ila kamwe huwezi sikia Tchouameni au Camavinga wanafanyiwa ubaguzi.
 
La Liga wajitafakari, watu wanasema kwanini kila siku Vini tu na sio weusi wengine. Hapohapo wajiulize kwanini haya matukio hayamtokei kwenye mechi za UEFA?!
Dogo ana uchokozi wa kitoto saa nyingine, japo haihalalishi ubaguzi ila naye anatakiwa kujirekebisha
 
Vini hatokuja hata kuwania top 3 ya ballon dor
That being said, hivi hao kina rudiger na Camavinga na Rodrygo hawakusimama kumtetea mweusi mwenzao alipokuwa anazomewa??
Au ndo ngozi nyeusi hatuna ushirikiano
 
Huo mdomo anao La Liga tu? Etoo na Neymar nao walikuwa na mdomo?!
Vini kwa sasa ni winger bora kabisa dunian... Kwa hiyo timu pinzani zinapocheza na Madrid wanajitaid kumtoa mchezoni ili wapate matokeo

Dogo ana maudhi kwa mashabiki wa upinzani,

La Ligq ina wachezaji wengi weusi, hapo Madrid kwenyewe kuna wachezaji kama 7 weusi wanaocheza mara kwa mara ila husikii wakibaguliwa

Yupo kama Baloteli
 
Acha mashara wewe ubaguzi wa rangi na kidini unaumiza sana
 
Dogo ana maudhi kwa mashabiki wa upinzani,

La Ligq ina wachezaji wengi weusi, hapo Madrid kwenyewe kuna wachezaji kama 7 weusi wanaocheza mara kwa mara ila husikii wakibaguliwa

Yupo kama Baloteli
View attachment 2630958
Hicho ndo kinamponza kila siku.
Akiguswa kidogo anaacha mpira, afu anaenda mlalamikia refa
 
Well said, Dejan alibaguliwa sana afisa habari wa timu yake anamtabulisha "mlete mzungu" ingekua mtu mweusi kwa wazungu waseme mlete mweusi pasinge kalika
 
Hivi, ikiwekwa Sheria Kwamba mashabiki watakaofanya vitendo vya kibaguzi timu yao itafyekwa point 3, si itasaidia jamani?
 
"Waafrika tuache inferiority complex, hiyo tabia ya kucheza cheza akifunga, kujiangusha, kulia Lia na refa ndio inasababisha azomewe. Hiyo fact alipewa na "Koke" ila akaishia kuitwa mbaguzi."
Pamoja na yote Ila dogo jana hakutendewa haki kabla ya kupewa umeme kuna tukio alifanyiwa..
 
Me nadhani Ni udhaifu tu
Kulalamika ubaguzi ni kujibagua mwenyewe
Dume zima utalalamika ati unabaguliwa
Kijana akomae ajipe thamani
Asijipe unyonge ati atakaa mtu ambague
Atajibagua kwanza akilini
Mbona wazungu wenyewe wanakuja Africa hawajawahi kulalamika popote kubaguliwa
 
Daah...! Huyu dogo wakimpoteza Madrid watakuwa wamepoteza kifaa.

Japo mimi ni Madrid damuni,lakini vitendo vya kibaguzi pale Spain ni vya ovyo sana,tangu enzi. Pomoja na kuipenda Madrid,lakini wapo pia wachezaji wanaonivutia na waliowahi kunivutia toka kipindi cha akina Stiv Mackmanaman. Akina Callos. Wakatokea akina Figo mtaalam wa mipira ya faulo,akina Zinedin Zidan baadae akaja kuwa kocha na kuchukua makombe kibao. Akina Ronaldo de Lima. Wakaja akina Ronaldo wa sasa.

Kwa kizazi hiki namkubali sana huyu dogo Vinicius Junior. Kuchezea Spain kunahitaji mioyo migumu ya kuvumilia,fuata ulichojia. Uvumilivu kama alivyovumilia. Nisingependa aondoke.
 
Akapiga kona kali sana
 
Kuna umewahi fanya kazi na Nigerian's

Utaelewa Waafrica tulivyo na mambo yetu kwa kichwa.

Il siri pekee ya ubaguzi,rangi,kabila na mengineyo kaa kimya piga kazi zako.

Muda upo ni mfupi sana wabaguzi watajichuja tu mdogo mdogo na kuja upande wako.

Makazini huku hizi mambo zipo sana , sana.
Ukisema uishi nazo unakufa chaap.
Hapa Bongo kuna makabila ukiwa nayo ofisini aisee kama hujajipanga kiakili unaweza kimbia.

Lakini hiyo ni mifumo ya maisha.Dunia ina mambo mengi mno muda hautoshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…