Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Ana miezi 5 yeye hata akiwa analia jifanye unaongea na simu ananyamaza kusikiliza maongezi ukiacha tuu anashusha kilio....anapenda sana kusikiliza maongezi ya simu hata kama anasinzia ataamka
 
Aisee mie sitaki hata kukumbuka,mwanang alikuwa mtundu balaa at least sasa hivi nimepumua,wakati akiwa na miaka mitano akiwa shuleni (boarding) sijui alitoa wapi mfuko ule wa Salfeti akawachukua watoto wadogo watatu akawafungia kwenye mfuko halaf akawaambia atakayepiga kelele namchapa viboko,akatoka akaenda kucheka bahati nzuri mwalimu akapita pale akaona mfuko unacheza cheza akashangaa kuufungua akakuta watoto walishaanza kuchoka, huku na huku nani kafanya hivi wakamtaja,mwalimu wake ananipigia simu mwanao leo kafanya kosa hili yaani nliishiwa pozi, nkaenda shuleni kwao namuuliza akanambia ahaa niliwaweka watulie maana walikuwa wanasumbua,siku nyingine karudi likizo niko kazini , akaweka Cd tano kwenye radio inayobeba cd tatu, nilivyorudi kanipokea getini akanambia yaani Mom radio yako imegoma kabisaa kuimba leo ahaa itakuwa ulinunua radio ya kichina,nafungua pale kaweka cd kushinda uwezo na sijui alichokonoa nn radio ikafa kabisaaaa
 
Uzi mzuri huu
images(33).jpg
 
Sikubali hakyanani sikubali namfata mwanangu , mama mkwe ntakulipa tu mahari yako nirudishie mke wang na mwanang , ona sasa mi nitaeleza nini hapa' mke wang toka amejifungua huu mwezi wa pili umeisha bado unawang'ang'ania tu aaaaagrahhh!!!???
 
mtoto wa mpangaji mwenzangu 1.5 anaupenda wimbo wa darasa 'muziki' ni balaa...simu yangu but nikiwa home kama yake. muda wote niweke wimbo huo achezee weeh nikizima ni atalia kwa makelele huyo hadi shida.
akilia ukimuuliza nani mkorofi anakwambia mama hata kama mimi ndio nimemkera!!
pia anapenda kupiga selfie yaani hata kama alikuwa analia ukimwambia selfie atakuja mbio na kilio kitaishia hapo.
watoto raha sana jamani
 
Mi wangu aliona utabiri wa hali ya hewa kwamba mji tuliopo kesho utakuwa na mvua kesho yake ilipofika asubuhi ananiambia mama ule utabiri unadanganya mbona hakuna mvua wakati jana walisema kutakuwa na mvua.

Ikabidi nimwambie mji mkubwa huu hivyo mvua haiwezi kunyesha mji mzima kwa wakati mmoja.
Wewe ulimdanganya mwanao.
 
Back
Top Bottom