Mwanangu (5): Baba mbona unapunguza mwendo??
Mimi: Kuna askari mbele
Mwanangu: Sasa usipopunguza mwendo atakufanyaje?
Mimi: Atanikamata
Mwanangu: Akikukamata atakufanyaje?
Mimi: Atanifunga kamba anipeleke gerezani kunifunga.
Mwanangu: Police kazi yake kufunga kamba watu?
Mimi: Ndiyo, ila wale wakorofi tu.
Mwanangu: Hata watoto wadogo anawakamata na kuwafunga?
Mimi: Ndiyo, lakini wale watoto wakorofi wasiopenda kufanya H/W
Mwanangu: Mimi si mkorofi na nafanya HW, si ndiyo baba
Mimi: eeeee mwanangu.
(Tunawakaribia Police wa usalama barabarani tunawapita)
Mwanangu: Police nimewaona watatu pia kuna Mwanamke, baba hata Police Mwanamke yupo
Mimi: Ndiyo
Mwanangu: Na yeye anaweza kukamata watu na kuwafunga?
Mimi: Ndiyo:
(Ukimya dakika 2)
Mwanangu: Baba weka speed One hundred tumeshawapita ma police. (huku akiangalia mshale wa speed-meter)
-------------