Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Mimi wa kwangu nilikuwa nadownload katuni namwekea kwenye simu anaangalia sasa siku moja nikamnyima akaniambia siku nikifa simu yangu itakuwa yake, sema tulikuwa wawili angelikuwa na mtu ningejua ameambiwa na hapo ana miaka 4 tu.
 
Mwanangu nakaa mbali nae ULA hakuna MTU anampenda kama Mimi hata kama hatujaonana mwezi mzima akiniona tu he is happy to the fullest,hahaha shobo na watu wengine,unaweza kumbeba na atabki amekuangalia tu anacheka akiamua Mwenyewe..
 
Wangu ana mwaka na nusu ila ana vituko vingi sana na pia anajitahidi kuongea. Mama yake kaendanaye kijijini kwa bibi siku ya pili kaaza kulia anadai tv. yeye huwa anaita tii
 

Huyu mdogo atakuwa amekufanana kwa asilimia kubwa sana...!
 
Jembe langu lina maswali flan ya kichunguzi sana halafu ana kumbukumbu ukimwambia kitu inabidi uwe makini kuna siku atakuumbua,mbaya zaidi au nzuri anapenda sana ishu za kijeshi jeshi, kuna siku tunaangalia maadhimisho ya Muungano gwaride linapigwa ye katulia tuuuliiiii duuh baadae nmkuta nje kashika gongo kaweka begani anapiga kwata na sauti za kikakamavu "mbeeeleeee tembeeeaaaa.....nyumaaaaa geeeukaaaaa"....

Moja ya maswali aliyowahi kuniuliza nilienda nae benk ATM kutoa hela akaangalia mchakato ulivyo baadae akaniuliza "hivi baba zile hela kuna mtu ndani anazitoa au zinatokaje?" hahahahaaa

Siku nyingine Aliuliza hivi mvua inatoka wapi? au Mungu anamwaga maji? daah

Kubwa kuliko alikua anacheza na wenzake wakamtania "mwangalie kichwa chake" duuh karudi amekasirika analia anasema "baba hiki kichwa sikitaki niletee kingine" Ilibidi niuvae ubaba kumtuliza.

kua na mtoto au watoto ni faraja sana....
 
Wangu ilikuwa nikivaa mzura(boshori/kofia ya baridi) huwa ananikimbia na hataki hata kuniona. Anajilaza kifuani kwa mamayake anaficha uso kabisa. Akiulizwa nini, ananyoosha kidole na kusema mtu...mtu. Nikiwa bize sitaki anisumbue naivaa tuu. Kuna kipindi nikaiweka kitandani akawa kila akitaka kuingia chumbani anachungulia na akiiona haingii. Alivyokuwa mkubwa mkubwa (3yrs) akawa kila akiiona anaichukua na kwenda kuitupa. Hata soksi zangu kama zina rangi nyeusi kama lile boshori akiziona anaenda kuzitupa nje.
 
Na dogo ana miaka 4..... Huchoki kuwa nae ana penda story anapenda compyuter zaidi ya kula.... Amesoma mwaka mmoja tu kaacha shule...... Wame mpeleka shule ya mambo ya IT... Shule za kawaida anakwambia haelewi chochote
 
Hakuna raha duniani kama mtoto. 0.8yrs lakini akiona tangazo lolote itv hata kama alikuwa anafanya nini, ataacha na kuangalia. Tangazo la tigo akimuona Joti lazima acheke, ukiongea na simu hata kama alikuwa analia, lazima atanyamaza, ukiweka loud speaker atacheka hadi raha..
 
ni 4yrs ..akiudhiwa tuu... ni kilio na kilio chake anakuangalia usoni huku machozi yanamwagika.....anasubiri umbembeleze....ukijifanya kumpotezea anaongeza sauti ya juu zaidi...[emoji1] [emoji1] [emoji1] ...lazima umbembelee....hakawii kunyamaza....
 
Hii ya huyu imetisha wangempa sapp tu.
 
Wa kwangu akiona paka anawaambia uchindwe kwa jila LA Yesu
Hahahaaa wangu anapenda kuwaonea sana nyau akimuona popote atamshika masikio na kumnyanua juujuu au mkia afu anamnyanyua hamuogopi hata kidogo..very interesting na mengine kibao afanyayo..watoto raha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…