Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jembe langu lina miaka3,akimuona mtu flani akiongea kwenye tv,anakimbilia remote na kubadili chanel.Simply ana aleji naye.
Hahaaa. I could talk about my kids the whole day.
Yule mkubwa wa almost 5 years ni mpole na ana hurumaaa. Pia anapenda sana ufugaji na ameshajua kuchanganya vyakula vya kuku. Anawajua kuku wake wakiumwa, anajua kuandika numbers kwenye kila yai linalotagwa na kuliondoa bandani. Pia anajua kufatilia aina ya kinyesi cha kuku kama ni cha kawaida ama ni cha kuumwa.
Mdogo wake anaekaribia miaka 3 ni mtundu na mbabe. Yeye anapenda magari na ufundi. Yaani umuoneshe video ya magari kwenye simu imekula kwako huna jinsi ya kujitoa atakavyotupa tantrums.
Wengi hupenda kusema nampendelea yule mkubwa lakini sio kweli. Ni rahisi kumuonea kutokana na sura yake ya kipole na huruma aliyonayo so nikisikiaga nywiiii amelia basi nageukaga chui. Because the lil man can surely take care of himself.
Jembe langu lina maswali flan ya kichunguzi sana halafu ana kumbukumbu ukimwambia kitu inabidi uwe makini kuna siku atakuumbua,mbaya zaidi au nzuri anapenda sana ishu za kijeshi jeshi, kuna siku tunaangalia maadhimisho ya Muungano gwaride linapigwa ye katulia tuuuliiiii duuh baadae nmkuta nje kashika gongo kaweka begani anapiga kwata na sauti za kikakamavu "mbeeeleeee tembeeeaaaa.....nyumaaaaa geeeukaaaaa"....Watoto katika hatua zao za ukuaji na kujifunza wanakuwa na mambo flani flani ya kufurahisha sana yaani mwanao anaweza kukuvunja mbavu balaa.
Mfano
1. Mwanangu (1.5years) anaweza kuwa anatazama TV akisikia unaongea na simu au umeweka music kwenye simu anakimbia kuja kuangalia simu hata kama TV ilikuwa na TV program ya katuni nzuri kiasi gani[emoji23] [emoji23] [emoji23]
2. Ukitaka alale we nenda kitandani weka music kwenye simu yako atakuja mwenyewe hata kama alikuwa anakwepa kulala[emoji23]
3. Anaheshimu simu yangu kama kituo cha polisi ila ya mama yake kashaipasua ukiiona utajua mama yake anafanya kazi idara ya miamba (geology)[emoji23]
4.Kupenda safari akiona mtu anatoka tu anaanza kuaga bye bye akijua nayeye anahusika na safari[emoji23] [emoji23]
5. Chakula kikiwa tayari, kabla sijaitwa kula yeye akiona mambo yako tayari anakuja kunipigapiga mgongoni(hajajua kuongea) akiashiria msosi tayari basi ukipotezea anaenda anarudi mpaka utakapoinuka[emoji23] [emoji23]
6. Mwanangu anatabia flani kama wivu, akiona naongea na mama yake mara nimemshika mkono tunaongea kama jambo la siri anakuja fasta analia anataka mama yake ambembe[emoji23]
Nadhani hajajua kwamba mama yake ni mke wangu[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hivi ni baadi ya vituko vya watoto mdau ongeza vya mwanao
Watoto wanaleta raha sanaaa
View attachment 521347
Hahaaaa.Huyu mdogo atakuwa amekufanana kwa asilimia kubwa sana...!
Wapo njiani bado. Inshallah...Heaven Sent mtoto wetu mbona ujasema anavyotufanyiaga
Hii ya huyu imetisha wangempa sapp tu.Wangu ana 4yrs last week walikuwa kwenye exam ya midterm kwa elimu yake ya kindergarten sasa mwalimu akaandika vitu amabvyo hawajawahi kusoma aisee aligoma kuufanya huo mtihani mpaka akaenda mama yake siku iliyofuata ikabidi afanye kama special mbele ya mama yake na kumbembeleza kwa sana tu.
Hah ha ha ha haha hah aahha!!!!!! Mkuu walimpa special paper ili asifeli dogo aliogopa kuwekewa mikasi kwenye paper.Hii ya huyu imetisha wangempa sapp tu.
Hahahaaa wangu anapenda kuwaonea sana nyau akimuona popote atamshika masikio na kumnyanua juujuu au mkia afu anamnyanyua hamuogopi hata kidogo..very interesting na mengine kibao afanyayo..watoto rahaWa kwangu akiona paka anawaambia uchindwe kwa jila LA Yesu
dah its so sad .....ila usijali....utapata mwingine...believe ingog onlyWangu sijui angekuaje, ametangulia mbele ya haki, katakua mbinguni kanacheza huko...
Basi ina idi tuanza kuandaa mazingira ili tukianza kufyatua wasije pata shida watoto wetuWapo njiani bado. Inshallah...
Mimi bado sijajipanga sasaata nikizaa na ww haina shida ata kuwa kama Genius
mm nmejipangaMimi bado sijajipanga sasa