Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Nimkatalia kitu Baraka na kumwambia "no yo can't have it" yeye anageuka naa kuniambia "when Jesus says yes nobody can say no" Ikabidi nimpe!
 
Hahahaaa, huyu mdogo wa kike ndiyo huwa ananikata maini, yaani keshanifanya mtumwa kabsaaa mpaka mama yake analalamika kwamba nampendelea! Kana mitego hakooo, na kanamacho ya kubembeleza hakooo...hata ukitaka kukatandika utashuka mwenyewe, sijuwi ndiyo watoto wa kike wote wameumbwa hivyo! 4yo na kako smart vibaya darasani, ila sasa nina mashaka nako sana kakikua itakuwaje, maana kanapenda sana simu, simu iwe ya tochi au smartphone atatafuta game lolote huyu mtoto na atalicheza utashangaa anapata score za ajabu wakati mimi siwezi hata kulicheza, kanapenda simu balaa......haka kakihongwa simu kweli katakataa?!...hapa dawa ni kukapatia kila kanachotaka.
 
Watoto wanafundishika. Ukimkanya kitu kwa karipio, hatathubutu kukirudia. Tabia ya kulea watoto kama mayai ndiyo inayo waharibu.
Kweli kabisa, mtoto umleavyo....
Nakumbuka huyu mdogo alivokuwa na miezi kadhaa alikuwa natabia za kuzira ovyo, mara aanze kulia bila sababu. Siku moja usiku aliamka akaanza kulia, sku hiyo nilkuwa nimechoka sana, mama yake alimbembeleza akachoka ikabidi aniamshe na mimi nimbembeleze, nimembembeleza kidogo haelewi nikaamua kumtolea uvivu....nilimlaza kifudifudi nikamtandika vibao vya makalioni kama vinne hivi, alipopaza sauti tu nikamwambia "KIMYA", kuanzia siku hiyo habari za kulialia kwisha, ukiskia sauti yake analia ujue kuna tatizo kubwa, tofauti na hapo sjuwi ameskumwa namwenzake sjuwi amenyang'anywa nini utaliona chozi tu na jicho lake la huruma...hatoi sauti kamwe. Akifanya jambo lisilofaa nikimkata jicho tu anaacha mara moja. Lakini ndiyo hivo, mtoto wa kike baba hafurukuti, akitaka kitu ana mbinu zake huwa sichomoi, na akionewa na mtu lazima aje kwangu ameinamisha kasura chini kusemelea! Penda sana toto hii.
 
Wa kwangu wa mwaka mmoja na miezi 4 haingii/hapiti mlangoni bila kupiga hodi. Anapiga hodi no matter anaingia au anatoka nje na hataendelea na safari hadi mtu ajibu karibu. Na kama ilikuwa yupo ndani basi wakati wa kutoka viatu ataviacha mlangoni (just kama mtu anayeingia ndani kutoka nje anavyovua viatu).
 
Anajua basi maana ya kuoa au ni hizi TV zinawaharbu watoto.


Nashukuru sasa anashinda shule........ Mazungumzo yake yamehamia ktk maswala ya shule.
Ahhh hapo sawa kabadili maongezi lkn mnaonekana marafiki sana na mtoto wako
 
Mi hadi nilipaka rangi na ubao nikawanunulia lkn bado wanauchora tuu
Nadhani kilicho bora ni kusubiri wakue. Mana hata nami nilikuwa na mpango wa kupaka rangi hivi karibuni. Kumbe itakuwa kazi bure.
 
Wangu 1.5 yrs anapenda kuandika andika kuna sehem yake ukutan ndo hapo hapo kila siku.kinachonishangaza zaid hatakag na hapend tushikiane simu mm na mama yake, nikishika ya mama yake anaichukua na kuitupa ila mama yake akiishika yangu anamnyan'ganya na kuniletea
gender issue!
 
Wangu ana 2.11 yrs ukijifanya umekazima gafla anapanda kifuan kwako huku Amalia anakushindilia makonde ya USO mpka utaamka
Akiona mama yake kaleta kitu anaulizia km baba yake kakinunua ikiwa sivyo kazuma baba nionyeshwe
Na ukimpiga wakat huwa unampa zawad hilo kosa si lako.. Anasingiziwa mwingine
 
Wangu ana 2.11 yrs ukijifanya umekazima gafla anapanda kifuan kwako huku Amalia anakushindilia makonde ya USO mpka utaamka
Akiona mama yake kaleta kitu anaulizia km baba yake kakinunua ikiwa sivyo kazuma baba nionyeshwe
Na ukimpiga wakat huwa unampa zawad hilo kosa si lako.. Anasingiziwa mwingine
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wakwangu ni mapacha (miezi 8). Doto ni m'babe hapendi kumwona mwenzie akinyonya, akiona tu hutambaa mbio mbio na kumvuta mwenzie... Mama yao hulazimika kumnyonyesha kulwa kwa siri pasipo na doto...

Sijui itakuwaje wakikuaaaaa.
 
Hahaaa. I could talk about my kids the whole day.

Yule mkubwa wa almost 5 years ni mpole na ana hurumaaa. Pia anapenda sana ufugaji na ameshajua kuchanganya vyakula vya kuku. Anawajua kuku wake wakiumwa, anajua kuandika numbers kwenye kila yai linalotagwa na kuliondoa bandani. Pia anajua kufatilia aina ya kinyesi cha kuku kama ni cha kawaida ama ni cha kuumwa.

Mdogo wake anaekaribia miaka 3 ni mtundu na mbabe. Yeye anapenda magari na ufundi. Yaani umuoneshe video ya magari kwenye simu imekula kwako huna jinsi ya kujitoa atakavyotupa tantrums.

Wengi hupenda kusema nampendelea yule mkubwa lakini sio kweli. Ni rahisi kumuonea kutokana na sura yake ya kipole na huruma aliyonayo so nikisikiaga nywiiii amelia basi nageukaga chui. Because the lil man can surely take care of himself.
Mpeleke SUA kabisa akagonge BVM tunaweza kuwa na mtu wa peke yake nchini.
 
Back
Top Bottom