Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni Taasisi inayojitegemea chini ya Ofisi ya Rais iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kutekeleza Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.
Jukumu lake kubwa ni kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yanazingatiwa.
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inautangazia umma kuwa imepeleka malalamiko kwenye Baraza la Maadili kuhusu tuhuma mbalimbali za ukiukwaji wa maadili kwa viongozi wa umma ikiwemo kushindwa kuwasilisha Tamko la Raslimali na Madeni kwa Kamishna wa Maadili. Viongozi wa Umma wanaolalamikiwa ni:
1. Mhe. Sakina Jumanne Mohamed- Mkuu wa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
2. Bw. Idefonce Arthur Columba Meneja wa Tanesco wilaya ya Kaliua, Tabora
3. Mhe. Cleophas John Mziray Hakimu Mahakama ya Mwanzo Puge, Tabora.
4. Bw. Jacobo Juliu Rombo -Katibu Tawala wilaya ya Arusha.
5. Bi. Mwajuma Abas Kihiyo -Msajili wa Hati Msaidizi, Tanga.
6. Mhe. Edward Reuben Mhina -Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Halsmashauri ya wilaya Korogwe
7. Mhe. Mwandei Mwachuma Mohamed-Diwani Halmashauri ya wilaya ya Mkinga.
8. Mhe. Mussa Bohero Jangwa-Diwani Kata ya Mayomboni, Tanga.
9. Mhe. Eligius Adrian Mbena -Diwani Kata ya Kolero, Morogoro.
Aidha, Baraza hilo linatarajia kufanya kikao cha uchunguzi wa kina wa malalamiko hayo tarehe 27 na 28 Mwezi Machi, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Sekretarieti ya Maadili Mtaa wa Tambukareli jijini Dodoma.
Jaji (Stahiki) Sivangilwa S. Mwangesi
KAMISHNA WA MAADILI
26 Machi, 2025