Viongozi CHADEMA kubalini ushauri

Mkuu unaumri Gani maana kama umeshushwa Leo duniani kwani wizi wa kura umeanza mwaka huu mpaka useme wameshafahamu si Kila mwaka wa UCHAGUZI chadema wanashiriki na wanalalamika kuibiwa kura unaona hao watu wanaakili timamu
Then, kama wizi unafanyika miaka yote, je ungeshauri wasusie/wasishiriki kabisa? Maana watajuaje kama watakaposhiriki hawataibiwa? Then, wakisusia indefinetely wana'cease' kuwa chama cha siasa.
 
Then, kama wizi unafanyika miaka yote, je ungeshauri wasusie/wasishiriki kabisa? Maana watajuaje kama watakaposhiriki hawataibiwa? Then, wana'cease' kuwa chama cha siasa.
Akili Yako haipo timamu kiufupi hujielewi kwahiyo unataka washiriki Ili baadae waanze kulialia wameibiwa kura sio halafu wasubiri tena UCHAGUZI ujao washiriki halafu baada ya UCHAGUZI walie wameibiwa kura kwahiyo Kila mwaka wawe wanalia kuibiwa kura
 
Akili Yako haipo timamu kiufupi hujielewi kwahiyo unataka washiriki Ili baadae waanze kulialia wameibiwa kura sio
OK, mkuu. Sijielewi na sina akili timamu. Tufanye hivi: weka CV yako hapa na mimi nitaweka ya kwangu, halafu wachangiaji wengine wataamua nani mwenye akili timamu na anayejitambua kati yangu na wewe. Najizuia kutumia lugha kama unayoifumia, lakini ili twende sawa tuanze na CV.
 
Cv yangu nimeanza na hiyo 10M weka yako niweke nyingine kuzidi hiyo
 

Attachments

  • Screenshot_20241129-210222.jpg
    106.6 KB · Views: 1

..Tanganyika tulidai uhuru na tukaupata bila mtu yeyote yule kuumizwa na Waingereza.

..Sasa kwanini suala la Tume Huru ya uchaguzi, na Katiba Mpya, watu wanataka nguvu utumie?

..Kwanini CCM / Serikali / Mama Samia hawasikilizi kilio cha wananchi cha Tume Huru, na Katiba Mpya?
 
Wanafaidika sana na mfumo uliopo ndo maana hawawezi kuruhusu hilo litokee. Sasa wamefika hatua wamejihalalishia kabisa kuiba. Uchaguzi wa juzi kulikuwa na watu wanaitwa ARO wa mtaa, kitongoji na kijiji kazi yao kubwa ilikuwa ni kuweka kura za wagombea wa Ccm zilizopigwa tayari kwahiyo hao watu walikuwa wanawaamuru wasimamizi wa vituo hiyo blunder ifanyike.

Hii nchi ni kama imekuwa mali ya Ccm wanaiamulia wanavyotaka.
 
Wewe ni adui wa chama hicho. Sidhani kuwa kweli upo ndani ya CHADEMA wewe.
Mambo ya CHADEMA yanakuuma nini kwani wamekuzuia kufanya siasa,? Mtu anakurupuka anataka CHADEMA wafanye anavyowaza.
 
Namkumbuka Mchungaji Mtikila aliposhinda shauri la mgombea binafsi mahakama kuu.Ingawa serikali ilishinda rufaa.
Hoja ya Mchungaji Mtikila ina mashiko hadi leo.Kuna wakati maamuzi ya chama yanakinzana na matarajio ya wanachama.
 
Za chini chini inadaiwa mbowe kapewa na mama yenu tilion moja ali asikache uchaguzi mpaka 2030,wewe mwenyewe huoni maghumashi yalivyojaa hata usingethubutu kupiga kula
 
Mambo ya CHADEMA yanakuuma nini kwani wamekuzuia kufanya siasa,? Mtu anakurupuka anataka CHADEMA wafanye anavyowaza.
Kwani wewe ndiye CHADEMA auni mali yako?

Hivi huoni unavyo jionyesha kuwa juha, au mpaka uelezwe pointi kwa point jinsi ujuha wako ulivyoi?
 
Za chini chini inadaiwa mbowe kapewa na mama yenu tilion moja ali asikache uchaguzi mpaka 2030,wewe mwenyewe huoni maghumashi yalivyojaa hata usingethubutu kupiga kula

..Mama Abduli anafanya biashara gani mpaka awe na trillioni 1 ya kuhonga?

..mjue hayo mapesa yanayochezewa yanatokana na kodi zetu, au rasilimali zetu zilizouzwa.

..Mama Abduli sio wa kumchekea, au kumkenulia meno.
 
Namkumbuka Mchungaji Mtikila aliposhinda shauri la mgombea binafsi mahakama kuu.Ingawa serikali ilishinda rufaa.
Hoja ya Mchungaji Mtikila ina mashiko hadi leo.Kuna wakati maamuzi ya chama yanakinzana na matarajio ya wanachama.
Kwenye wengi kupata consensus ni vigumu, maana wakati mwingine mambo yanatokea si kwa sababu ya shida ya maamuzi, bali wenye mamlaka. Unakumbuka kule Zanzibar wakati ule Tume ya Uchaguzi iliposema uchaguzi urudiwe na CUF wakajitoa, CCM ikashinda uchaguzi asubuhi na mapema. Kwa jinsi mambo yalivyo hapa kwetu na wakati mwingine pia kutokana na malalamiko vyama vya siasa vilivyonayo kuhusu baadhi ya hukumu za mahakama, matatizo kama haya yanaendelea bila kupata ufumbuzi wake hadi hapo wananchi watakapokuwa na political consciousness. Maana ili chama fulani cha siasa kipate ushindi kinategemea kwa kiasi kikubwa support ya wananchi ambao ndio wengi.
 
Hao wananchi wanakuungaje mkono kipindi cha uchaguzi ambapo wagombea wako wameenguliwa?
 
Wanaolazimisha CHADEMA kushiriki ni wale wanaotaka ubunge 2025. Wakiunga mkono kutoshiriki uchaguzi serikali za mitaa watazodolewa pindi wakishinikiza kushiriki uchaguzi wa 2025
 
Siku kikiibuka chama kipya chenye nguvu kipesa ambacho ni Cha kizalendo kweli kweli na sio maigizo ndio mwanzo wa chadema kukosa wafuasi
Too bad kitaingia kwenye mifumo ile ile iliyowekwa na serikali na kitakuwa weaked, aka chadema 2.0

Until mifumo ya uchaguzi na mazingira yatakapo badilishwa for good, haijalish chama gani kipya kitakuja. Hakutakuwa na changes
 

Wananchi washajionea vya kutosha Magumashi ya chafuzi chini ya CCM toka mwaka 2019, wamejionea magumashi kwenye process nzima tangu utunzi wa sheria mbovu za uchaguzi. Wananchi wanahitaji kuongozwa ili kupuuza haya maigizo ya chafuzi. Sasa unfortunately Chadema inaflip flop, mara itoe tamko la kamati kuu kuwa bila katiba mpya haitashiriki chaguzi, mara ibadili gia angani. Sasa flipflop hizi wananchi wabayumbishwa na wengine wanapoteza imani hata na CHADEMA yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…