Itachukua muda, ila kushiriki kwao ndiko kutakaowafanya wananchi wawaunge mkono. Wasiposhiriki CCM itatumia huo mwanya kuwaonyesha wananchi kwamba wasichague chama kinachoogopa uchaguzi. Lakini wakishiriki na kufanyika madudu wananchi watazinduka na kusema ngoja wawaunge mkono. Hata kwenye mashindano ya michezo ni heri timu ishiriki na ifanyiwe faulo, maana mashabiki wataona, kuliko ile ambayo haishiriki maana mashabiki hawataelewa - wanahitaji waone. Kushiriki uchaguzi na kufanyiwa madudu ndiko kunskoleta support ya wananchi. Siku moja nili'share' na watu niliosoma nao kwenye group letu kwamba sijawahi kushiriki uchaguzi wowote tangu mwaka 2020. Wadau walinipakia sana, wakisema "watu wote wangekuwa kama wewe Botswana chama cha upinzani kingrdhinda?" Nikatafakari, nikaona ni kweli, maana unaweza kususia uchaguzi kumbe mwaka huo ndio wananchi wsmesmua wakuunge mkono, sasa utashindaje kama hudjiriki uchaguzi? Upo hapo?