Viongozi hawa wamesema Hayati Magufuli aliongoza nchi vibaya sana, wewe je?

Shujaa wa Africa kwa kinywa chake mwenyewe amewahi kiri kwamba ni kichaa sasa Diallo hana kosa gani kurudia yaliyomo.
 
Mkuu tatzo lako unawaza Kama unaendesha gari lenye site mirror 1 utagongwa aukugonga jifunzi kuendesha gari lenye site mirror zote mbili..

Magu alikuwa na mapungufu yake ila alikuwa na mazr x1000000 Zaid ya huo unaouita ubaya..

By the way Kuna mambo alifanya kwa manufaa ya nchi.. umeona lkn? Nchi ilikuwa kdg tu tungesahau kabisa kuwa na bajet inayotegemea wawekezaji...

Lkn unaona kinachokuja?? Vuta pepsiiii bariiidiiii utakiona tu.. ilimlad uwe na site mirror 2
 
Kila siku kuna at least Uzi mpya kuhusu JPM Wengine Legacy Wengine Uchwala wa utawala wake na blah blah kibao
Uhalisia ni kwamba
1. JPM ni mfu na kwa mujibu wa imani yangu mfu hajui neno
2. JPM Alifanya madudu na alifanya Mazuri mengi hakuna exemption katika hili kwake kama mwanadamu
3. JPM atahukumiwa kwa matendo yake sio mtazamo/fikra zako

Kipindi cha vuguvugu za kuwania uteuzi (2015) mimi binafsi niliamini nchi hii ingehitaji kuwa na mtu kama JPM hasa katika kurejesha nidhamu na kudhibiti ufisadi niliamini kuwa out of many JPM alikuwa ni pekee ambae angefiti hiyo post Na hapa Leo hata Dunia nzima inipinge nitasimama kusema kuwa JPM aliyafikisha matarajio yangu kwenye climax

Naamini kifo chake kimekuja baada ya kutimiza alichopangiwa

Kitu muhinu Sana kufanya katika matumizi ya muda huu ni kutathimini tunakokwenda na huyu mrithi wa JPM
 
My best President

Namkubali sana

Nilimpigia kura

Hata akifufuka leo nampigia tena

Pumzika salama rais wangu Tutaonana Paradiso
Ikitokea Kama wakafanya tu kupiga kura waweke picha ya jpm huku harafu wawakusanye wamaowaamin wawake upande mwingne.. nakuhakikishia Kama watapata 1% yaan tume itakuwa imewapa tu ili wasipate aibu..

Tena ili wasilete kisingizio walete tume wanayoiona wao.. JPM is another level ever ever...
 
Tatizo la mwendazake alikuwa mzuri lakini kilichomharibia ni ubabe wa kuvuruga maisha ya watu. Angewaacha watu waendeleae na maisha yao akaanza utawala wake bila kumkera mtu angetawala na upinzani ungekufa. Kuvumiliana ni Jambo la hekima zaidi kuliko kujifanya unajua zaidi.

Kuna mambo ya kurekebisha lakini sio kibabe. Kumuharibia mtu maisha lazima akuone adui. Lakini ukiishi nae vizuri atajisikia maisha haya sio atajirekebisha hata yeye mwenyewe atatafuta jinsi ya kurekebisha. Eti tumbua, vunja nyumba, chukua he'll za watu bank, funga biashara za watu n.k.
 
Yule mwehu alikuwa yupo tayari kumtoa mama yake mzazi zawadi kwa jamaa baada ya kupewa jogoo
 
Alafu sisi wananchi millioni 60 tunasema Magufuli aliongoza vizuri.

Ikiwekwa picha ya Magufuli vs hao viongozi tumchague nani bado picha ya Magufuli itawaacha mbali sana.
Labda wewe na wa Mirembe wenzako ndo mtamchagua " mwenzenu"
 
Kuna kundi la boda boda,machinga,na watu wasio na kipato wengi wao walikuwa pro Magufuli kwa kuwa bodaboda hawakamatwi na traffic, wala machinga hawabughuziwi kufanya biashara kokote.
Kundi la akina mama hasa wa vijijini walimpenda Magufuli kwa kusogeza huduma za maji,vituo vya afya na elimu bila malipo,umeme REA
Lakini kundi la wanasiasa wa upinzani hawana hamu kabisa,aliwaondolea haki za msingi za kufanya siasa.
Pia wafanyabiashara aliua biashara, hawataki kumsikia.
Wafanyakazi wa umma nao aliwanyima stahiki zao
Vyeti fake,mishahara hewa hawezi kumpenda aliwaondoa lakini Bashite hakumgusa.
CCM nayo walikuwa wanamwogopa kama Simba, hata pale alivyowapendelea kuwapa nyadhifa mbali mbali wahamiaji haramu kutoka vyama pinzani akiwaacha makada wa CCM nao kiundani hawakupenda kabisa.
 
Mwendazake aliiharibu mno nchi hii, wewe acha tu!
 
Huyu namba 2 nadhani ni yule mweiz wa escrow maana alikuwa na wasiwasi mda wote anngewwfuata akina sesi 'lakini inashangaza eti wezi ndo wanaona furaha imerudi hii inafikirisha kidogo
 
Swala ni moja Tu .Manyangumi wa uporaji ufidadi na kila takataka vilikuwa vimekita mizizi CCM. it's clear majority ya hawa hawa CCM, JPM hakuwa upande wao. Ukweli mchungu
Saa mtu Kama werema anakipi cha maana Kama sio mweiz tu Kama wezi wengine maana aliishi kwa wasiwasi kweli alidhani jpm angemuunganjsha na akina seth
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…