Viongozi, Kukosolewa si kukosewa heshima

Viongozi, Kukosolewa si kukosewa heshima

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Pamoja na mambo mazuri ambayo viongozi wetu wamekuwa wakifanya wawapo katika madaraka yapo mengi mabaya pia wanafanya, ikiwa ni pamoja na vitendo au mipango mibaya ambayo haina tija kwa jamii au inayoumiza wananchi.

Kiongozi anayefuata dhana ya utawala bora hataona kero au kakosewa heshima kwa kukosolewa kwani ni moja ya nguzo ya utawala bora. Inabidi akubali kukosolewa na kupokea mchango wa maoni kutoka kwa viongozi wenzake au wananchi wake ili kuweza kuletta tija katika utawala wake.

Jambo hili limekuwa gumu sana kupokelewa na viongozi wengi, wengi wakipata madaraka hujiona kuwa wamemaliza kila kitu katika na wao ndio waamuzi na wasemaji wa mwisho. Hawahitaji mawazo, maoni wala kuambiwa kuwa hapo umekosea, fanya hivi. Kwa mtu atakayethubutu kumkosoa huona kama kamvunjia heshima na kumchukulia kama adui wa utawala wake na kuanza kutafuta namna ya kumnyamazisha au kumuangamiza kabisa.

Kiongozi wa aina hiyoanaua dhana nzima ya utawala bora kwani anakuwa hahitaji kuwajibika katika kuongoza kwake, Hujichukulia kama ana upeo mkubwa kuliko wote anaowaongoza na kwamba mawazo yake ndio yaliyo bora kuliko anaowaongoza na hivyo watu au kundi zima la watu walio chini yake hawapaswi kuwa na maono au mtazamo tofauti na wake.

Kiongozi wa namna hiyo mara nyingi hutumia ukali ili kuweza kujilinda na vitisho kuwa yeyote atakaye thubutu kwenda kinyume na yeye atakiona cha moto, na hutengeneza sheria nyingi ambazo zitawafumba mdomo watu wa chini yake na zitamuweka yeye salama ili asiweze kuhojiwa na watu anaowaongoza.

Ni vyema watawala wakatambua kuwa wao kupata nafasi ya kukalia kiti cha madaraka si kuwa ndio wana upeo na akili nyingi kupita wanao waongoza, wapo wenye maono mapana kushinda wao, hivyo wakiruhusu mlango wa kupokea maonyo, ushauri na kukosolewa bila kuweka chuki wala kinyongo watapata mawazo yaliyo bora ambayo yakitekelezwa yakuwa na tija kwa jamii nzima na kuondoa malalamiko na kuleta usawa katika jamii.

Kukubali kukosolewa kutaondoa malalamiko ya kutekelezw a kwa miradi ambayo haihitaji kwa haraka kwenye jamii na kuacha mahitaji ya haraka kwenye jamii, na hivyo kufanyajamii iendelee kuwa na imani na uongozi huo na kuupa ushirikiano ili uendelee kudumu.

Kiongozi anayeshupaza shingo yake, utawala wake huwa hauna mwishi mzuri. Kubali unapokosea na kuanza kurekebisha makosa.
 
Back
Top Bottom