Viongozi kumi (10) Bora Tanzania

Mkuu sidhani kama ni kweli Mwinyi amefanya mengi kama aliyemfuatia.Jaribu kupeleleza utakubaliana nami.Pia sidhani Mwinyi anaweza kuwa amefanya mambo makuu zaidi ya Chifu Mkwawa,Au Nyerere au Magufuli.Mwinyi huenda akafaa nafasi nyingine lakini kwa hapo hajawafikia.Jaribu kuchunguza,Utakubaliana nami.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
 
Pole MATAGA wakurudi shule ni wewe sio mimi...

Nikuombe urudie kusoma tittle vizuri ndio utajua namaanisha nini
MATAGA inahusiana nini na post hii? Title ni Tatu Bora ila hao wawili ni Nyongeza katika List itakayofuata ya 10 Bora, Usichokielewa ni nini? Umeshawahi kuangalia List za kumi bora au zinginezo jinsi zinavyopangwa? Au hii ndiyo mara yako ya kwanza kuona list ya tatu bora?.Una shida nyingi sana.
 
Kama hayupo Chalamila na Ndugai hio list ni fake
 
Hakuna cha 10 bora wala nini yote yanafanywa kumtafutiwa Jiwe room aonekane kwenye rank za juu!

Kwa matendo dhalimu aliyofanya jiwe hastahili hata kuwemo top 10! Taratibu mtazoea tu kuwa hatunaye tena na hatutakuja kupata kiongozi evil kama yeye!

Poleni sana MATAGA
 

Hiiiiii yaani Sokoine Amedumu kwenye Serikali kama Kiongozi kwa Miaka 6 amzidi Hayati Magufuli aliyefanya Miaka 26 kwa kuchapa kzn vzr usiku na mchana Nashauri Magu awe wa Pili then Sokoine
 
Kwangu mini kama historia haikuwa manipulated Mzee Mwinyi ndio kiongozi bora wa muda wote nchi hii.

Aliikuta nchi kwenye depression kubwa lakini akaisongesha na hakuwa na ujivuni wala visasi na pengine ndio sababu Mungu amempa maisha marefu.

Mzee Mwinyi Mungu wangu ninayemwabudu katika Kristo Yesu akutunze akushibishe siku akujalie afya.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Umeharibu ulipoweka na majizi na madikteta kwenye hiyo list
 
Ondoa yule aliyeshinda uchaguzi kwa 99.99999%, nafikiri hizo kura alikuwa anapigia na kuhesabia chumbani kwake...
 
Tatizo mawazo yako biased.....kidini zaidi. Yaani Mwendazake umpime kwenye mizani na Jakaya au Mwinyi?.......

Anyway sijui huu msamiati MATAGA' unahusu 'wazarendo' kwa mujibu wa Jiwe mnapambana nini kum-upgrade mtu 'aliyechafua'
 
B
Hiiiiii yaani Sokoine Amedumu kwenye Serikali kama Kiongozi kwa Miaka 6 amzidi Hayati Magufuli aliyefanya Miaka 26 kwa kuchapa kzn vzr usiku na mchana Nashauri Magu awe wa Pili then Sokoine
Barabara za lami nchini by 75% zina historia na Magufuli. This is the true legacy anastahili no 2
 
Mkuu bila shaka ww ni uzao wa miaka ya 90 kuja juu kwahiyo ulichokiona kwa Mkapa kutokana na umri wako haukukiona kwa Mwinyi. Mwinyi alikuta nchi hii watu wakitaka kwenda kazini tena maofisini wanagombania "chai maharage" bila shaka huo usafiri haukuukuta, Mwinyi alipoingia yakaletwa mabasi. Alikuta hospitalini hazina madawa na dawa chache zilizokuwepo zilitolewa kwa wale waliojigusa mfukoni, Mwinyi alipoingia madawa yakaanza kujaa mahospitalini pia hospitali zikajengwa nyingi tu. Ilikuwa watu wanashindia na kulalia mlo mmoja tena wa uji wa chumvi na kipande cha muhogo au ugali uliosongwa na unga wa "yanga" na maharage yanayokaa siku nzima jikoni ili yawive, Mwinyi alipoingia vyakula vikajaa madukani walanguzi wakakamatwa (hapa nazungumzia wale waliokuwa wanaishi kwa kuuzia watu masikini vitu vya serikali ambavyo walihitaji wapewe kama msaada) Mwinyi alikuta shule nyingi hazina walimu walikimbia kutokana na ukata wa pesa, Mwinyi alipoingia walimu wakaanza kulipwa vizuri kwa thamani ya hela ya wakati huo na kusababisha walimu kuongezeka mashuleni na pia ikasababisha shule za serikali na binafsi kujengwa kwa wingi. Barabara nyingi zilianza kujengwa wakati wa utawala wa Mwinyi, Tv wengi walianza kuziona wakati wa utawala wa Mwinyi. Hela mtaani ilianza kuonekana wakati wa utawala wa Mwinyi, Mkapa aliapishwa mwaka 1995 watu tunamuona kwenye TV yote ilikuwa juhudi ya Mwinyi, watanzania wengi tulianza kuonekana tunajua kuvaa wakati wa utawala wa Mwinyi, kabla ya hapo watu walikuwa wanashindia misuli kama fasion kumbe ni ukata wa nguo madukani. Mwinyi kaleta mengi ikiwemo demokrasia ambapo kabla yake haikuwepo. Nchi ikaanza kujulikana kimataifa. Nchi za jirani zikaanza kuwa zinakuja kununua bidhaa au kwetu badala ya sisi kununua kwao nk. Sasa ukisema Mkapa kafanya makubwa zaidi ya Mwinyi ni vigumu kueleweka. Maana kila alilolifanya Mkapa lilikuwa na mtelezo tu kwan alikuta ashatengenezewa mazingira mazuri ya kufanya hayo unayoyasema. Labda kubwa alilofanya Mkapa ni kubinafsisha mashirika ya serikali tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…