Wazolee
JF-Expert Member
- Sep 1, 2018
- 3,183
- 3,660
Mwinyi ndio raisi bora kabisa kuwahi kutokea katika nchi hii na ubora wake hautafutika hadi dunia inaisha maana waliomfuata wote wanaendelea na mfumo wa uchumi aliyo uacha Mwinyi yani CAPITAL RISIM hakuna aliyethubutu kurudi katika mfumo wa uchumi wa SOCIAL RISIMMkuu sidhani kama ni kweli Mwinyi amefanya mengi kama aliyemfuatia.Jaribu kupeleleza utakubaliana nami.Pia sidhani Mwinyi anaweza kuwa amefanya mambo makuu zaidi ya Chifu Mkwawa,Au Nyerere au Magufuli.Mwinyi huenda akafaa nafasi nyingine lakini kwa hapo hajawafikia.Jaribu kuchunguza,Utakubaliana nami.
Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Ila Mimi nilichogundua watu ambao hawajui Mwinyi alifanya nini katika nchi hii
1) Alikuwa hajazaliwa hivyo hajui tofauti ya maisha ya watanzania kabla Mwinyi hajawa raisi na baada ya Mwinyi kuwa raisi
2) Alikuwa anaishi kijijini maana mabadiriko ya kiuchumi ukiwa mjini especially Dar unayaona vizuri na unayaishi kila siku tofauti na mtu aliyeko kijijini
KWA UFUPI TU
Kipindi Mwinyi anakabidhiwa nchi Watanzania
1)walikua hawana nguo za kuvaa na viatu / akaleta nguo za mitumba na viatu
2)kulikua hakuna chakula yani unga wa mahindi, ngano na mchele / akafungua milango waganya biashara walete ndipo walipo ibuka kina Dewji na Bakharesa
3) kulikua hakuna mafuta ya taa na ilikua siku mkisikia yanakuja katika duka la mtaani kwenu mnakaa foleni kutwa nzima na chupa zenu mkononi / Mwinyi alienda Queite tazizo la mafuta likaisha kabisa
3) kulikua hakuna sukari alipaingia zikaanza kuja gali za ugawaji kila kata kwa wiki Mara moja gali likija mnakaa foleni na mgambo anakusimamieni na kuchukua mwisho kilo mbili nakumbuka zamu yetu ilikua J5 mwisho tatizo likaisha kabisa
4) kulikua hakuna viwanda na makampuni ya watu binafsi wakaruhusiwa kuanzisha
5) kulikua hakuna shule za private akaruhusu wenye uwezo wanzishe shule za private
Kabla ya shule za private ilikuwa mwanao akikosa nafasi za shule za serikali hata kama unayo pesa mwanao hawezi kusoma
6) kama mnaendesha vi private car sasa hivi basi mjue Mwinyi ndio aliyeruhusu vije
Sasa mlivyo mambumbu mnamsifia mkapa kwamba alikusanya kodi vizuri bira ya kujua kwamba hiyo miundombinu iliyomfanya Mkapa aweze kukusanya kodi Mwinyi ndio aliyeijenga
Binafsi nawaheshimu na nawakubali maraisi wote walifanya ambacho walitakiwa wafanye katika vipindi vyao ila Mwinyi ndio mbora wao sidhani kama kuna mtu anaweza kushangilia barabara na madaraja wakati akiwa hana basic need