Viongozi kumi (10) Bora Tanzania

Mwinyi ndio raisi bora kabisa kuwahi kutokea katika nchi hii na ubora wake hautafutika hadi dunia inaisha maana waliomfuata wote wanaendelea na mfumo wa uchumi aliyo uacha Mwinyi yani CAPITAL RISIM hakuna aliyethubutu kurudi katika mfumo wa uchumi wa SOCIAL RISIM

Ila Mimi nilichogundua watu ambao hawajui Mwinyi alifanya nini katika nchi hii

1) Alikuwa hajazaliwa hivyo hajui tofauti ya maisha ya watanzania kabla Mwinyi hajawa raisi na baada ya Mwinyi kuwa raisi

2) Alikuwa anaishi kijijini maana mabadiriko ya kiuchumi ukiwa mjini especially Dar unayaona vizuri na unayaishi kila siku tofauti na mtu aliyeko kijijini

KWA UFUPI TU
Kipindi Mwinyi anakabidhiwa nchi Watanzania

1)walikua hawana nguo za kuvaa na viatu / akaleta nguo za mitumba na viatu

2)kulikua hakuna chakula yani unga wa mahindi, ngano na mchele / akafungua milango waganya biashara walete ndipo walipo ibuka kina Dewji na Bakharesa

3) kulikua hakuna mafuta ya taa na ilikua siku mkisikia yanakuja katika duka la mtaani kwenu mnakaa foleni kutwa nzima na chupa zenu mkononi / Mwinyi alienda Queite tazizo la mafuta likaisha kabisa

3) kulikua hakuna sukari alipaingia zikaanza kuja gali za ugawaji kila kata kwa wiki Mara moja gali likija mnakaa foleni na mgambo anakusimamieni na kuchukua mwisho kilo mbili nakumbuka zamu yetu ilikua J5 mwisho tatizo likaisha kabisa

4) kulikua hakuna viwanda na makampuni ya watu binafsi wakaruhusiwa kuanzisha

5) kulikua hakuna shule za private akaruhusu wenye uwezo wanzishe shule za private
Kabla ya shule za private ilikuwa mwanao akikosa nafasi za shule za serikali hata kama unayo pesa mwanao hawezi kusoma

6) kama mnaendesha vi private car sasa hivi basi mjue Mwinyi ndio aliyeruhusu vije

Sasa mlivyo mambumbu mnamsifia mkapa kwamba alikusanya kodi vizuri bira ya kujua kwamba hiyo miundombinu iliyomfanya Mkapa aweze kukusanya kodi Mwinyi ndio aliyeijenga

Binafsi nawaheshimu na nawakubali maraisi wote walifanya ambacho walitakiwa wafanye katika vipindi vyao ila Mwinyi ndio mbora wao sidhani kama kuna mtu anaweza kushangilia barabara na madaraja wakati akiwa hana basic need
 
Watu walioishi vipindi vyote vya utawala kama ss nawashangaa sana kutothamini juhudi za mzee Mwinyi .
Mzee Mwinyi alianza kuchafuliwa nyota na mtangulizi wake kwa kumdhihaki, kumponda na kumkejeli kwa kila alilolifanya iwe baya au zuri. Na kwa vile wengi walimuheshimu na kumuamini mtangulizi huyo basi yakajengeka mazoea na propaganda za kuonesha kuwa Mwinyi hakufanya kitu. Mabaya yote ya mtangulizi wake pamoja na yale machache ya kwake mwenyew Mwinyi( kama binadam) akabebeshwa Mwinyi, alafu yale yote mazuri aliyofanya/leta Mwinyi akapewa Mkapa ndio maana mleta mada anakwambia eti Mkapa ndio kafanya mambo makubwa zaidi ya Mwinyi na kwamba Mwinyi hakustahili kuwepo ktk list hii. Ukweli ni kwamba mtangulizi alitaka Mwinyi aongoze nchi kupitia mawazo yake yeye, kitu ambacho Mwinyi alikikataa. Mwinyi aliona kuongoza nchi kwa style ya mtangulizi wake huenda kungesababisha mapinduzi kama jinsi alivyotaka kupinduliwa huyo mtangulizi.
 
Namba 4 tupa mbali haituhusu labda kama ulilenga hii thread isomwe na kabila fulani
 
Kama kigezo ni lazima tuchague kutoka hiyo list basi mimi ninao wawili tu

Mwalimu pamoja na Sokoine - Huyo number 3 mtoe hapo hastahili kuwepo !!

Mkwawa alikuwa kiongozi wa Wahehe, hakuwahi kuwa kiongozi wa kitaifa - yeye ataingia kwenye kinyanganyiro cha WATEMI hodari - tunao wengi tu kama kina Kijigitile, Mirambo, Isike, Lugusha nk
 
Mkuu umemaliza kila kitu na naludia kusema 80% wanaomuona Mzee Mwinyi mbaya ni watoto/vijana waliozaliwa miaka ya tisini na kuendelea lakini kiukweli Mwinyi aliikuta Nchi hii ina hali mbaya kwelikweli
Nakumbuka mwaka1983 nilikoswakoswa kukamatwa na (JKT) kwa kosa la kuuza Dawa ya mbu(tena vipande vipande) kwa kuonekana mlanguzi vijana walikuwa wanakamatwa na kupigwa(mpaka wanajeruhiwa) kwa kosa kuuza sigara tu(SM,SPORTSMAN,EMBASSY au SIGARA KALI) alikuwa akikutwa na paketi mbili za hiyo bidhaa atakiona cha mtema kuni

Ninachokiona sasa ni nguvu kubwa inayotumika sasa kumsifu Magufuli hata kwenye mabaya na nguvu hiyo ndio imetumika sana kwa Nyerere kumsifu sana hata kwenye mabaya
 
Viongozi bora ambao hawakuwahi kuwa Marais

Oscar Kambona

Edward Sokoine

Salim Ahmed Salim

Mark Mwandosya
Nashangaa, huyo Salim Ahned Salim hatajwi tajwi, sijui kwa vile VIJANA WA LEO hawakushuhudia utumishi wake!?
Hata Nyerere alikuwa anamkubali sana, mpaka kufikia kupewa Uwaziri Mkuu. (Kwa vile ni Mzanzibari, sijui kama alistahili kuwa Waziri Mkuu wa JMT! )
 
Ni kweli bro nakubaliana na wewe wale wasio jua nchi hii aliitoa wapi na akaifikisha wapi aidha walikuwa hawajazaliwa au walikuwa wanaishi kolomije

Hilo la foleni ya mafuta ya taa na sukari nalikumbuka vizuri sana maana kipindi hicho ndio nilikua katika umri wa kutumwa tumwa sukari

Siku ya kuja mafuta dukani Kwa mpemba zinapangwa chupa kuanzia dukani hadi mtaa wa pili mafuta yakisha fika Kila mtu anasimama ilipokua chupa yake
 
Madhara ya kumpa Zito au Lisu akushikie akili ndio haya
 
Kaikosea hii 3 Bora, ilibidi iwe hivi

01. Nyerere
02. Mwinyi
03. Dr. JK
 
Du!
 
Mleta mada ni mzaliwa wa miaka ya 90 ukijumlisha na matango pori aliyolishwa huko alipoandikia uzi huu, ndio maana hakuweza kuuona mchango wa Mwinyi. Hapo ilitakiwa Mwinyi awe nafasi ya pili kwa vile ya kwanz siku zote huwa anapewa Nyerere. Mkapa angepokezwa kijiti na Nyerere huenda mpk miaka ya 2000 watu wangekuwa bado wanapiga miswaki ya miti, wanafulia majani ya mipapai, redio au taarifa ya habari watu wangekuwa bado wanaenda kusikiliza kwa mjumbe, chai ya mkono mmoja nk. Mkapa alikuwa na chembe chembe ya utawala wa Nyerere kwahiyo mengi ambayo angeyakuta kwa Nyerere na yeye angeyafanya yale yale au kwa lugha nyingine angetawala kwa style ile ile ya Nyerere. Ndo maana nasema Mkapa leo kuonekana amefanya mazuri ni kwa sababu alikuta Mwinyi ashamtengenezea na kumpa yeye amalizie vichache vilivyobaki
 
Mkuu Je, Unadhani Salim Ahmed Salim alikuwa bora kuliko Sokoine?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ