Viongozi kumi (10) Bora Tanzania

Wewe unaonekana hukuwa mjini wakati wa utawala wa Mwinyi ulikuwepo huko kijijini kwenu kolomije

Hayo uliyoandika umekopy na kupest kutoka katika makala zilizoandikwa na watu waliokua na chuki dhidi ya Mzee Ruksa

Ila sisi watoto wa mjini tuliokuwa tuliokuwa tunayashuhudia anayo yafanya Mwinyi hatuwezi kukuelewa sana sana tutakuona mshamba tu
 
Nimeshampa darsa kijana, kama hajatuelewa basi itakuwa ana lake jambo
 
Hatuwezi kuelewana kwa kuwa sisi wengine tumeyaishi maisha ya utawala wa Mwinyi practically na wewe umeujua utawala wa Mwinyi kupitia fasihi simulizi

Ila tambua kitu kimoja Mwinyi ndio aliyeleta Uhuru wa vyombo vya habari yani aliruhusu TV za private , radio za private , magarazet ya private pamoja na mitandao ya simu

Kama sio Mwinyi hata hii JF isingekuwepo hivyo tusingeweza kuona huu utumbo wako unao andika andika
 
Nilisahau ila umenikumbusha kumbe hadi democrasia ya vyama vingi ameileta Mwinyi
 
Nitarejea kwako mkuu
Kijana umemsikia Gwajima anakwambia Nyerere alipoondoka madarakan aliacha viwanda 411, Mwinyi alipoingia hakudili navyo bali alidili na mamb mengine ambayo Gwajima anasema yalikuwa mazuri tu kama nilivyokueleza huko juu. Alipoingia Mkapa akabinafsisha viwanda vyote 411 vilivyoachwa na Nyerere badala ya kuviendeleza. Sasa ukichunguza kwa makini maneno ya Gwajima pamoja na michango iliyotolewa na wachangiaji wengi kuhusu uongozi wa Mwinyi, utakubaliana na mimi kwamba Mwinyi alifanya mamb mengi mazuri kwa kuiletea maendeleo nchi hii bila kubinafsisha viwanda
 
Kwangu Mimi ni Mkapa coz alituliza Uchumi na kujenga Uchumi imara,alifanya Mabadiliko Makubwa katika mifumo ya Serikali Taasisi kama Takukuru, TRA,NHIF,Tanroads,EWURA na Mikakati mbalimbali kama Mkukuta Mkurabita MMEM MMES ilibuniwa kipindi chake.

Pia alishirikiana na Wafadhili hadi nchi kusamehewa Madeni,Mashirika mbalimbali yaliyokufa kama TBL,TCC nk yalibinafsishwa yakaanza kulipa kodi ingawa kwenye zoezi zima la Ubinafsishaji kulikuwa na Changamoto mbalimbali.

Kiongozi mwingine ambaye alikuwa Mzuri ni JK ambaye aliendesha nchi kwa Demokrasia na Uwazi sana tukapata Uwekezaji Mkubwa,heshima duniani,Alijenga Miundombinu na Taasisi nyingi ikiwemo Tume ya Ajira.

To me Nyerere kipindi chake nilikuwa sijitambui ila namsoma nasikia alikuwa Mzalendo,Mwinyi nae nasikia alifungua Milango ya Uchumi huru
 
Vipi kuhusu hayati Magufuli au mengi mazuri aliyoyafanya huyaoni?
 
Hata mtekaji nae anakuwa kiongozi bora
 
Ni kweli mkuu,Ila hata katika kitabu chake amekiri kwamba sera yake ya ubinafsishaji ilikuwa mbaya na ilifungua mianya kwa mafisadi japo iikuwa na nia njema.Ila hilo halimuondolei mazuri mengi aliyoyaasisi.Kumbuka baada ya kushika hatamu alitekeleza mageuzi ya sera za kiuchumi kwa kubana matumizi, kunyanyua sekta binafsi, kuvutia wawekezaji wa nje na ubinafsishaji wa mashirika ya umma.
Matokeo yake yakawa ni kuungwa mkono na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF), na kujenga msingi madhubuti wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa miaka iliyofuata hata baada ya kutoka madarakani.
 
Shukran kwa kunielewesha mkuu. Najua kuna yale ambayo sikuyajua kuhusu Mkapa ukanijuza, na kuna yale ambayo wewe hukuyajua kuhusu Mwinyi mimi na wachangiaji wengine hapo juu tukakujuza. Wote sisi lengo letu ni moja kuijenga Tanzania yenye upendo kwa watu wote bila kubagua yoyote
 
Mh Kassim Majaliwa Kassim Waziri mkuu wa JMT huenda akaingia katika List hii siku zijazo!
 
Upumbavu wako ni mkubwa lini chief Mkwawa aliiongoza Tanzania Iliozaliwa1964 wakati akiwa kaburin8???
 
Upumbavu wako ni mkubwa lini chief Mkwawa aliiongoza Tanzania Iliozaliwa1964 wakati akiwa kaburin8???
Usijifanye mjuaji sana kiongozi Tunaposema Tanzania tunazungumzia eneo hili kijiografia regardless ya jina! Kwa maana ya Tanganyika ya mjerumani.Na hapo list inazungumzia viongozi wote mashuhuri haijalishi ni wa kimila au wa kiserikali ila uongozi wowote kiujumla ambao uliacha alama muhimu katika jamii kwa mfano hapo palikuwa na viongozi wengi wa kimila kama kina Mangi Sina,Mangi Meli na wengineo lakini katika wote hakuna aliyemfikia Chifu Mkwawa.Kwa hiyo tunapozungumzia Tanzania hapa tunazungumzia eneo lote kiujumla pre & post colonial era.
 
Bila unafiki wala kujipendekeza kwangu top 10 ya viongozi bora Tanzania ni kama ifuatavyo.

1. Mh. Ali Hassan Mwinyi
Huyu alikabidhiwa nchi ikiwa na ukata wa kutosha. Chumvi mnapanga foleni kuipata lakini kwa busara usiku na hofu ya Mungu aliweza kuiongoza nchi na kutoka kwenye mkwamo. Pia alianzisha vyama vingi 1992

2. J.K .Nyerere
Ni bora kama mwanaharakati wa uhuru na pia kama kiongozi wa kisiasa sifa kubwa kwake ni jinsi alivyojali utu wa mwafrika bila kujali nchi anayotoka. Nyerere was a true son of Africa soil.

3. J.M.Kikwete
Atakumbukwa kwa demokrasia na ujenzi wa miundombinu. J.K ndie aliyejenga shule za kata nchi nzima ndie aliepeleka umeme wa rea vijijini, ndie alijenga kilometa nyingi za lami kuliko Rais yeyote kwenye nchi hii.Kipindi chake wahitimu wa kada ya ualimu hawakuwahi kulia ajira. Itoshe kusema J.K wewe ni zaidi ya kiongozi

4. Maalim Seif
Huyu alishikiria amani ya Zanzibar miaka yote ya uhai wake. hakuwa mbinafsi na zaidi ya yote aliipenda Zanzibar kuliko yeye mwenyewe. Mzee Seif Mungu akupe amani kama ulivyodumisha amani ya nchi yetu.

5. F.A.Mbowe
Wengi unajiuliza kwa nini Mbowe? Ndio ni Mbowe. Kama kuna mtu ambaye anastahili tuzo ya amani Tanzania basi ni Sef, Mbowe na Lowassa. Kama upinzani wa nchi hii ungekuwa chini ya Lissu, Slaa, Lipumba, au kiongozi mwingine yeyote yule basi inawezekana tungekuwa tunaongea mengine saa hizi.Uyu jamaa Mungu kampa hekima na uvumilivu wa kiongozi. Ni mvumilivu kweli kweli.


6. J.P.Magufuli
Misimamo na utekelezaji wa mipango hasa linapokuwa suala la utekezaji wa miradi ya kimkakati. J.P.M alikuwa level nyingine sana kwenye kusimamia miradi na maamuzi yake.
Hakuna kiongozi mwenye uthubutu kama J.P.M kidogo Lowassa ila bado hajamfikia J.P.M linapokuja suala la uthubutu na kusimamia maamuzi.

7. B.W.Mkapa
Ukweli na uwazi. Muongeaji mzuri ukimtoa Mwalimu Nyerere kwenye kujieleza na kueleza jambo likaeleweka huyu anafuata. Aliasisi mpango wa shule za kata. Alifuta ada shule za msingi na ilijua kuibua vipaji vya uongozi mfano. J.P.M ambaye alimpa Uwaziri kwa mara ya kwanza kwenye selikari yake.

8. Amani Karume
Muasisi wa selikari ya umoja wa kitaifa Zanzibar. Alipenda majadiliano akiamini ndugu wanapokuwa na tofauti hukaa mezani kuzungumza kumaliza tofauti.

9. Samuel Sitta
Ni mfano wa kuigwa kwa upande wa bunge. Alipachikwa jina la Spika wa viwango. Aliiutendea haki muhimili wa Bunge na kuupa hadhi na heshima iliyo stahili.

10. E.N.Lowassa
Naamini Lowassa ni mwanasiasa bora wa kizazi chake. Hana siasa za maji taka, visasi wala vijembe. Mchapa kazi na mtendaji mzuri. Kilichonifanya kumuweka kwenye kundi hili ni namna alivyosimamia ujenzi wa bomba la maji kutoka ziwa Victoria kuja Shinyanga na ujenzi wa chuo cha UDOM.
Siasa sio umasikini jamani, na umasikini sio sifa nzuri hata kidogo.

Hawa ndio viongozi bora kwangu mimi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo mkuu kwa mtazamo wako E.N. Lowasa alikuwa bora kuliko E.M. Sokoine? na F.A Mbowe ni bora kuliko Kambona na Kawawa?
 
Mbowe ni kiongozi mvumilivu na mwenye haiba kubwa sana kati ya viongozi wote wa upinzani. Hata ongea yake ni ya kipekee. Bravo kamanda Mbowe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…