MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Umesoma vizuri comment za watu humu ukapata darsa kuhusu hao unaowakataa au umeona tu picha zao ukatoa hukumu?
Nawajua wote hakuna aliyefanya Jema.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umesoma vizuri comment za watu humu ukapata darsa kuhusu hao unaowakataa au umeona tu picha zao ukatoa hukumu?
OkNawajua wote hakuna aliyefanya Jema.
Wewe unaonekana hukuwa mjini wakati wa utawala wa Mwinyi ulikuwepo huko kijijini kwenu kolomijeBaadhi yaliyokuwemo katika utawala wa Mwinyi
1. Azimio la Arusha la mwaka 1967 la ujamaa na kujitegemea liliwekwa kando na Azimio la Zanzibar la 1992 la soko huria (Ruksaa)
2. Mfumo wa chama kimoja (1965/1977) uliondolewa na kuwekwa mfumo wa vyama vingi (1992). Wanachi 20%, wakiongozwa na Baba wa Taifa Mwl Nyerere, wakiukubali huku 80% wakiukataa.
3. Kiliundwa cheo kisicho cha kikatiba cha naibu waziri mkuu na wakati huo alikuwa Lyatonga Mrema.
4. Viongozi na familia zao, wakageuka kuwa wafanya biashara wakubwa na wasiolipa kodi. Rasilimali za nchi zikaanza kutoroshwa nje kama dhahabu iliyokamatwa airpoti ya JNIA.
"Ikulu isigeuzwe pango la wanyanganyi"(NYERERE).
5. Muungano ulipata msukosuko mkubwa haswa kwa kitendo cha Zanzibar kutaka kujiunga na umoja wa nchi za kiislam (OIC) na vuguvugu la kutaka kujitenga la G55.
6. Sarafu ya shilingi ikashushwa thamani kufuatia maelekezo ya IMF na tukaanza kuona noti mpya za shilingi 200, 500, 2000, 5000 na 10000 zinazodunda hadi leo.
7. Pesa ikawa rahisi kupatikana, biashara kedekede, watu wakawa na fedha kuliko serikali yao. Wakati huo serikali ilikuwa inakusanya Shilingi bilioni 25 kwa mwezi.
8. Wanyama mwalimu aliocha Ikulu kama Swala, Mbuni na Tausi wakaanza kupungua kwa kasi.
9. Wafanya biashara wakubwa kina Bakhresa, Mengi na Raza wakaibuka kipindi hiki.
10. Vyombo huru vya habari, TV, Radio Fm na Magazeti vikashamiri.
11. Mwalimu Nyerere akawa raisi mstaafu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa, huku akisimama na kukemea mambo mbalimbali aliyoyaona hayapo sawa
12. Shule za Sekondari za serikali zilikuwa zinafungwa mara wa mara kwa kukosa chakula.
13. Ada ya shule za Sekondari ya Serikali ilipanda kutoka elfu nne hadi nane kwa mwaka.
14. Michael Jackson alitembelea Tanzania huku kajifunika puani kuzuia harufu mbaya na vumbi la Dar es salaam na alifika hadi Ikulu wakati huo Ikulu hakuna masofa [emoji3]
15. Nyerere alimuita Rais Mwinyi ni dhaifu ukiangalia kwenye kitabu cha Mwl Nyerere cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania cha Mwaka 1994 ukurasa wa 66 Mwl aliandika hivi Nanukuu "Rais Mwinyi ni mtu mwema na mpole lakini ni kiongozi dhaifu; na upole wake na udhaifu wake unatumiwa na watu ambao sio wema"
Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Nimeshampa darsa kijana, kama hajatuelewa basi itakuwa ana lake jamboWewe unaonekana hukuwa mjini wakati wa utawala wa Mwinyi ulikuwepo huko kijijini kwenu kolomije
Hayo uliyoandika umekopy na kupest kutoka katika makala zilizoandikwa na watu waliokua na chuki dhidi ya Mzee Ruksa
Ila sisi watoto wa mjini tuliokuwa tuliokuwa tunayashuhudia anayo yafanya Mwinyi hatuwezi kukuelewa sana sana tutakuona mshamba tu
Hatuwezi kuelewana kwa kuwa sisi wengine tumeyaishi maisha ya utawala wa Mwinyi practically na wewe umeujua utawala wa Mwinyi kupitia fasihi simuliziBaadhi yaliyokuwemo katika utawala wa Mwinyi
1. Azimio la Arusha la mwaka 1967 la ujamaa na kujitegemea liliwekwa kando na Azimio la Zanzibar la 1992 la soko huria (Ruksaa)
2. Mfumo wa chama kimoja (1965/1977) uliondolewa na kuwekwa mfumo wa vyama vingi (1992). Wanachi 20%, wakiongozwa na Baba wa Taifa Mwl Nyerere, wakiukubali huku 80% wakiukataa.
3. Kiliundwa cheo kisicho cha kikatiba cha naibu waziri mkuu na wakati huo alikuwa Lyatonga Mrema.
4. Viongozi na familia zao, wakageuka kuwa wafanya biashara wakubwa na wasiolipa kodi. Rasilimali za nchi zikaanza kutoroshwa nje kama dhahabu iliyokamatwa airpoti ya JNIA.
"Ikulu isigeuzwe pango la wanyanganyi"(NYERERE).
5. Muungano ulipata msukosuko mkubwa haswa kwa kitendo cha Zanzibar kutaka kujiunga na umoja wa nchi za kiislam (OIC) na vuguvugu la kutaka kujitenga la G55.
6. Sarafu ya shilingi ikashushwa thamani kufuatia maelekezo ya IMF na tukaanza kuona noti mpya za shilingi 200, 500, 2000, 5000 na 10000 zinazodunda hadi leo.
7. Pesa ikawa rahisi kupatikana, biashara kedekede, watu wakawa na fedha kuliko serikali yao. Wakati huo serikali ilikuwa inakusanya Shilingi bilioni 25 kwa mwezi.
8. Wanyama mwalimu aliocha Ikulu kama Swala, Mbuni na Tausi wakaanza kupungua kwa kasi.
9. Wafanya biashara wakubwa kina Bakhresa, Mengi na Raza wakaibuka kipindi hiki.
10. Vyombo huru vya habari, TV, Radio Fm na Magazeti vikashamiri.
11. Mwalimu Nyerere akawa raisi mstaafu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa, huku akisimama na kukemea mambo mbalimbali aliyoyaona hayapo sawa
12. Shule za Sekondari za serikali zilikuwa zinafungwa mara wa mara kwa kukosa chakula.
13. Ada ya shule za Sekondari ya Serikali ilipanda kutoka elfu nne hadi nane kwa mwaka.
14. Michael Jackson alitembelea Tanzania huku kajifunika puani kuzuia harufu mbaya na vumbi la Dar es salaam na alifika hadi Ikulu wakati huo Ikulu hakuna masofa [emoji3]
15. Nyerere alimuita Rais Mwinyi ni dhaifu ukiangalia kwenye kitabu cha Mwl Nyerere cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania cha Mwaka 1994 ukurasa wa 66 Mwl aliandika hivi Nanukuu "Rais Mwinyi ni mtu mwema na mpole lakini ni kiongozi dhaifu; na upole wake na udhaifu wake unatumiwa na watu ambao sio wema"
Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Kijana umemsikia Gwajima anakwambia Nyerere alipoondoka madarakan aliacha viwanda 411, Mwinyi alipoingia hakudili navyo bali alidili na mamb mengine ambayo Gwajima anasema yalikuwa mazuri tu kama nilivyokueleza huko juu. Alipoingia Mkapa akabinafsisha viwanda vyote 411 vilivyoachwa na Nyerere badala ya kuviendeleza. Sasa ukichunguza kwa makini maneno ya Gwajima pamoja na michango iliyotolewa na wachangiaji wengi kuhusu uongozi wa Mwinyi, utakubaliana na mimi kwamba Mwinyi alifanya mamb mengi mazuri kwa kuiletea maendeleo nchi hii bila kubinafsisha viwandaNitarejea kwako mkuu
Ha haaa Mkuu kwani ulitaka wasife???Na wote wamekufa?. Malipo ni hapa hapa dunian watendeee wema binadamu wenzio bila dhuluma utaishi umri mrefu
Vipi kuhusu hayati Magufuli au mengi mazuri aliyoyafanya huyaoni?Kwangu Mimi ni Mkapa coz alituliza Uchumi na kujenga Uchumi imara,alifanya Mabadiliko Makubwa katika mifumo ya Serikali Taasisi kama Takukuru, TRA,NHIF,Tanroads,EWURA na Mikakati mbalimbali kama Mkukuta Mkurabita MMEM MMES ilibuniwa kipindi chake.
Pia alishirikiana na Wafadhili hadi nchi kusamehewa Madeni,Mashirika mbalimbali yaliyokufa kama TBL,TCC nk yalibinafsishwa yakaanza kulipa kodi ingawa kwenye zoezi zima la Ubinafsishaji kulikuwa na Changamoto mbalimbali.
Kiongozi mwingine ambaye alikuwa Mzuri ni JK ambaye aliendesha nchi kwa Demokrasia na Uwazi sana tukapata Uwekezaji Mkubwa,heshima duniani,Alijenga Miundombinu na Taasisi nyingi ikiwemo Tume ya Ajira.
To me Nyerere kipindi chake nilikuwa sijitambui ila namsoma nasikia alikuwa Mzalendo,Mwinyi nae nasikia alifungua Milango ya Uchumi huru
Hata mtekaji nae anakuwa kiongozi boraTanzania imebahatika kuwa moja ya nchi iliyopata kuwa na viongozi bora kabisa Afrika na hata duniani kwa ujumla.Viongozi hao wamepata kuwa na mchango mkubwa Tanzania na hata kwa bara la Africa. Tunaona mifano ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye amepigania uhuru si kwa nchi ya Tanzania tu bali amekuwa na mchango mkubwa katika harakati za uhuru kwa nchi jirani kama Afrika Kusini, Zambia na Msumbiji.
Tanzania pia imepata kuwa na wanaharakati na wapigania uhuru mahiri walioweza kuitwaa nchi kutoka katika kucha za wakoloni. Tunaona wapigania uhuru na wanaharakati kama Kinjekitile Ngwale, Bwana Abushiri na Bibi Titi Mohammed. Viongozi kama Mtemi Isike, Chifu Mirambo, Mangi Meli na wengineo wengi ambao walikuwa viongozi wa kimila walikuwa mstari wa mbele katika mapambano ya uhuru na hatimaye kuikomboa na kutupatia Tanzania hii tunayoifurahia leo.
Bila kupoteza muda, Naomba niweke orodha fupi ya viongozi waliopata kuongoza Tanzania walioacha alama kubwa na historia ya kipekee kwa ubora wao na uwezo wao wa kiuongozi ambao pasi na shaka uliacha alama kubwa kwa watanzania.
Kwa sasa nitaweka orodha tu kwa kifupi ila nitarejea kuelezea kila mmoja kwa undani zaidi.Pamoja na kuongeza orodha mpaka kufikia kumi (10) Bora.
Updates; Moderators naomba mnibadilishie Title iwe Kumi (10) Bora badala ya Tatu (3) Bora. Ahsante
Viongozi Kumi (10) bora kuwahi kuwepo Tanzania.
1. Mwl.Julius Kambarage Nyerere (Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
View attachment 1752017
2. Edward Moringe Sokoine ( Waziri Mkuu wa Tanzania 1977–1980 na 1983 - 1984)
View attachment 1752018
3. John Pombe Magufuli (Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
View attachment 1752024
4. Chief Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga (Mkwawa) - Chifu wa kabila la Wahehe
View attachment 1752828
5. Benjamin William Mkapa (Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
View attachment 1752030
6. Rashidi Mfaume Kawawa ( "Simba wa Vita" - Waziri mkuu wa Tanzania 1972 - 1977" )
View attachment 1752641
7.Ali Hassan Mwinyi ( Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1985 - 1995 )
View attachment 1752648
NB; Inaendelea...
Ni kweli mkuu,Ila hata katika kitabu chake amekiri kwamba sera yake ya ubinafsishaji ilikuwa mbaya na ilifungua mianya kwa mafisadi japo iikuwa na nia njema.Ila hilo halimuondolei mazuri mengi aliyoyaasisi.Kumbuka baada ya kushika hatamu alitekeleza mageuzi ya sera za kiuchumi kwa kubana matumizi, kunyanyua sekta binafsi, kuvutia wawekezaji wa nje na ubinafsishaji wa mashirika ya umma.Kijana umemsikia Gwajima anakwambia Nyerere alipoondoka madarakan aliacha viwanda 411, Mwinyi alipoingia hakudili navyo bali alidili na mamb mengine ambayo Gwajima anasema yalikuwa mazuri tu kama nilivyokueleza huko juu. Alipoingia Mkapa akabinafsisha viwanda vyote 411 vilivyoachwa na Nyerere badala ya kuviendeleza. Sasa ukichunguza kwa makini maneno ya Gwajima pamoja na michango iliyotolewa na wachangiaji wengi kuhusu uongozi wa Mwinyi, utakubaliana na mimi kwamba Mwinyi alifanya mamb mengi mazuri kwa kuiletea maendeleo nchi hii bila kubinafsisha viwanda
Shukran kwa kunielewesha mkuu. Najua kuna yale ambayo sikuyajua kuhusu Mkapa ukanijuza, na kuna yale ambayo wewe hukuyajua kuhusu Mwinyi mimi na wachangiaji wengine hapo juu tukakujuza. Wote sisi lengo letu ni moja kuijenga Tanzania yenye upendo kwa watu wote bila kubagua yoyoteNi kweli mkuu,Ila hata katika kitabu chake amekiri kwamba sera yake ya ubinafsishaji ilikuwa mbaya na ilifungua mianya kwa mafisadi japo iikuwa na nia njema.Ila hilo halimuondolei mazuri mengi aliyoyaasisi.Kumbuka baada ya kushika hatamu alitekeleza mageuzi ya sera za kiuchumi kwa kubana matumizi, kunyanyua sekta binafsi, kuvutia wawekezaji wa nje na ubinafsishaji wa mashirika ya umma.
Matokeo yake yakawa ni kuungwa mkono na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF), na kujenga msingi madhubuti wa ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa miaka iliyofuata hata baada ya kutoka madarakani.
Usijifanye mjuaji sana kiongozi Tunaposema Tanzania tunazungumzia eneo hili kijiografia regardless ya jina! Kwa maana ya Tanganyika ya mjerumani.Na hapo list inazungumzia viongozi wote mashuhuri haijalishi ni wa kimila au wa kiserikali ila uongozi wowote kiujumla ambao uliacha alama muhimu katika jamii kwa mfano hapo palikuwa na viongozi wengi wa kimila kama kina Mangi Sina,Mangi Meli na wengineo lakini katika wote hakuna aliyemfikia Chifu Mkwawa.Kwa hiyo tunapozungumzia Tanzania hapa tunazungumzia eneo lote kiujumla pre & post colonial era.Upumbavu wako ni mkubwa lini chief Mkwawa aliiongoza Tanzania Iliozaliwa1964 wakati akiwa kaburin8???
Kwa hiyo mkuu kwa mtazamo wako E.N. Lowasa alikuwa bora kuliko E.M. Sokoine? na F.A Mbowe ni bora kuliko Kambona na Kawawa?Bila unafiki wala kujipendekeza kwangu top 10 ya viongozi bora Tanzania ni kama ifuatavyo.
1. Mh. Ali Hassan Mwinyi
Huyu alikabidhiwa nchi ikiwa na ukata wa kutosha. Chumvi mnapanga foleni kuipata lakini kwa busara usiku na hofu ya Mungu aliweza kuiongoza nchi na kutoka kwenye mkwamo. Pia alianzisha vyama vingi 1992
2. J.K .Nyerere
Ni bora kama mwanaharakati wa uhuru na pia kama kiongozi wa kisiasa sifa kubwa kwake ni jinsi alivyojali utu wa mwafrika bila kujali nchi anayotoka. Nyerere was a true son of Africa soil.
3. J.M.Kikwete
Atakumbukwa kwa demokrasia na ujenzi wa miundombinu. J.K ndie aliyejenga shule za kata nchi nzima ndie aliepeleka umeme wa rea vijijini, ndie alijenga kilometa nyingi za lami kuliko Rais yeyote kwenye nchi hii.Kipindi chake wahitimu wa kada ya ualimu hawakuwahi kulia ajira. Itoshe kusema J.K wewe ni zaidi ya kiongozi
4. Maalim Seif
Huyu alishikiria amani ya Zanzibar miaka yote ya uhai wake. hakuwa mbinafsi na zaidi ya yote aliipenda Zanzibar kuliko yeye mwenyewe. Mzee Seif Mungu akupe amani kama ulivyodumisha amani ya nchi yetu.
5. F.A.Mbowe
Wengi unajiuliza kwa nini Mbowe? Ndio ni Mbowe. Kama kuna mtu ambaye anastahili tuzo ya amani Tanzania basi ni Sef, Mbowe na Lowassa. Kama upinzani wa nchi hii ungekuwa chini ya Lissu, Slaa, Lipumba, au kiongozi mwingine yeyote yule basi inawezekana tungekuwa tunaongea mengine saa hizi.Uyu jamaa Mungu kampa hekima na uvumilivu wa kiongozi. Ni mvumilivu kweli kweli.
6. J.P.Magufuli
Misimamo na utekelezaji wa mipango hasa linapokuwa suala la utekezaji wa miradi ya kimkakati. J.P.M alikuwa level nyingine sana kwenye kusimamia miradi na maamuzi yake.
Hakuna kiongozi mwenye uthubutu kama J.P.M kidogo Lowassa ila bado hajamfikia J.P.M linapokuja suala la uthubutu na kusimamia maamuzi.
7. B.W.Mkapa
Ukweli na uwazi. Muongeaji mzuri ukimtoa Mwalimu Nyerere kwenye kujieleza na kueleza jambo likaeleweka huyu anafuata. Aliasisi mpango wa shule za kata. Alifuta ada shule za msingi na ilijua kuibua vipaji vya uongozi mfano. J.P.M ambaye alimpa Uwaziri kwa mara ya kwanza kwenye selikari yake.
8. Amani Karume
Muasisi wa selikari ya umoja wa kitaifa Zanzibar. Alipenda majadiliano akiamini ndugu wanapokuwa na tofauti hukaa mezani kuzungumza kumaliza tofauti.
9. Samuel Sitta
Ni mfano wa kuigwa kwa upande wa bunge. Alipachikwa jina la Spika wa viwango. Aliiutendea haki muhimili wa Bunge na kuupa hadhi na heshima iliyo stahili.
10. E.N.Lowassa
Naamini Lowassa ni mwanasiasa bora wa kizazi chake. Hana siasa za maji taka, visasi wala vijembe. Mchapa kazi na mtendaji mzuri. Kilichonifanya kumuweka kwenye kundi hili ni namna alivyosimamia ujenzi wa bomba la maji kutoka ziwa Victoria kuja Shinyanga na ujenzi wa chuo cha UDOM.
Siasa sio umasikini jamani, na umasikini sio sifa nzuri hata kidogo.
Hawa ndio viongozi bora kwangu mimi.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app